Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,711
😷😷🏃♂️🏃♂️Wewe kijana, acha upekupeku 🤣🤣🤣...
Hee...!Usijali shem langu. Ni kweli the_legend anamiliki duka la mikate lakini mimi namiliki bakery...
Litro.... Litro...
Bishop ee naomba basi nyingine...
Teh teh teh 😂😂Litro.... Litro...
.. ..
🤣 a beeLitro.... Litro...
.. ..
❤️Taxi - (118)
“Pole sana, Madame... poleni kwa mkasa huu wa kusikitisha!” Mr. Oduya alisema huku akimkumbatia Madame Norah katika hali ya kumfariji kisha akaanza kumpetipeti mgongoni.
“Nashukuru sana, Mr. Oduya. Nawashukuruni nyote kwa kuja kunifariji katika kipindi hiki kigumu sana. Kwa kweli tukio hili limeniumiza mno kuliko maelezo!” Madame Norah alisema huku machozi yakimlengalenga machoni.
Mr. Oduya na Madame Norah wakaachiana na wote wakaketi kwenye viti. Madame Norah akamtambulisha Bi. Pamela kwa Mr. Oduya na Mafuru, kuwa ni mdogo wake na ndiye mama aliyemlea Joyce tangu utoto wake.
“Okay! Nice to meet you, poleni sana kwa mkasa huu, naamini Mungu atamsaidia mgonjwa aweze kupata nafuu” Mr. Oduya alisema huku akimpa mkono Bi. Pamela.
“Amen, baba!” Bi. Pamela aliitikia huku akimpa mkono Mr. Oduya. Wakasalimiana.
“Vipi kuhusu hali ya mgonjwa? Inaendeleaje?” Mr. Oduya alimuuliza Madame Norah huku sura yake ikionesha simanzi ingawa moyoni mwake hali ilikuwa tofauti.
“Hadi sasa hali yake siyo nzuri, bado hajaweza kuamka,” Madame Norah alisema kwa huzuni huku akilengwa na machozi.
“Nimekufahamu kwa miaka mingi lakini sikujua kama una mtoto!” Mr. Oduya alimwambia Madame Norah huku akimtazama kwa makini. “Kwani alikuwa anaishi hapa hapa Dar es Salaam?”
“Hapa hapa Dar es Salaam, kwa sasa ndiye ninayemwandaa kwenye shughuli zangu zote, na hata lile tamasha letu ni yeye anapaswa alisimamie. Kwa sasa nimechanganyikiwa wala sijui itakuwaje!” Madame Norah alisema kwa huzuni huku akifuta machozi yaliyoanza kumtoka kisha akashusha pumzi.
“Oh! Pole sana...” Mr. Oduya akasema kisha akaendelea. “Ni nani hasa waliofanya unyama huu?”
“Hadi sasa bado haijajulikana, lakini naamini siku zao zinahesabika,” Madame Norah alisema kwa uchungu mkubwa huku akionekana kutoneshwa kidonda cha majonzi.
“Kwa vyovyote hawa waliofanya hivi hawana roho ya ubinadamu hata chembe. Hivi umejaribu kutafakari lengo lao hasa lilikuwa nini?” Mr. Oduya aliuliza ili kutaka kujua huku akiyatuliza macho yake kwenye uso wa Madame Norah.
“Kwa inavyoonekana mlengwa wa tukio lile alikuwa ni mumewe Joyce, Sammy, bahati yake hakuwepo nyumbani muda huo,” Madame Norah alisema kisha akayapandisha juu mabega yake na kuyashusha papo hapo.
“Kwani huyo Sammy kawakosea nini hao watu! Jeje hajakwambia kama ana fununu zozote kuhusiana na jambo hili?”
“Anasubiri ripoti ya polisi. Hata hivyo kama kuna watu kawakosea au hajawakosea siyo ishu maana katika hii dunia tunayoishi mtu huwezi kukosa adui hata kama hujamkosea mtu yeyote. Mwingine anaweza kukuchukia tu bila sababu,” Madame Norah alisema na kuinamisha kichwa chake chini.
“Inasikitisha sana kwa ukatili huu kufanyiwa mtu asiye na hatia kama Joyce...” Mr. Mafuru alisema kwa huzuni huku akimtupia jicho la chati Mr. Oduya.
“Kwa kweli hawa watu wanatakiwa wasakwe hadi wapatikane na wafundishwe adabu. That’s why I’m here to help you,” Mr. Oduya akadakia kumwambia Madame Norah kwa sauti tulivu.
“Msijali, shemeji zangu... nawahakikishia hawa watu watapatikana tu wherever they are. Kama walizoea kuwafanyia wengine mambo haya basi hapa wamekanyaga waya wa umeme wakiwa pekupeku, hawatachukua hata round,” Madame Norah alisema kwa hasira huku akipigapiga ngumi juu ya paja lake na kuwafanya Mr. Oduya na Mafuru waangaliane. Macho yao yaliweza kuongea mengi zaidi ya ambavyo angeongea kwa mdomo.
“They will all pay! They must pay for what they did to my daughter!” Madame Norah aliongeza huku akiyasaga magego yake kwa hasira.
“Brave woman, you and me we’ll meet later and have a nice talk,” Mr. Oduya aliwaza huku akimtazama Madame Norah kwa hisia kisha akalazimisha tabasamu.
“Unajua wewe kwa sasa ni mshirika wangu, yeyote anayekufanyia ubaya basi kanifanyia mimi pia. Kuanzia sasa tuko vitani kuhakikisha hawa watu wanapatikana. Kwa hiyo naomba ukipata taarifa zozote nyeti nijulishe, nitatumia hata rasilimali zangu kuhakikisha wanatiwa nguvuni na kuozea jela,” Mr. Oduya alisema kwa uchungu.
Muda huo huo simu yake ya mkononi ikaanza kuita. Aliitazama kwa makini na kukunja sura yake kisha akamtupia jicho Mafuru na kushusha pumzi huku akisimama na kujitenga kidogo na wengine ili aweze kuongea kwa uhuru na simu ile aliyodai ni ya muhimu sana.
Baada ya dakika mbili za kuongea na simu sura yake ilibadilika sana, alionekana ni mtu mwenye wasiwasi mkubwa tofauti na alivyokuwa mwanzo. Alirudi pale kwenye meza na kuwaaga Madame Norah na Bi. Pamela akiwaeleza kuwa kulikuwa na jambo la dharura lililojitokeza na alitakiwa kwenda kulishughulikia haraka.
Wakaaga na kuondoka wakimwahidi Madame Norah kuendelea kuwasiliana ili kujua maendeleo ya mgonjwa.
* * * * *
Honi ya gari aina ya BMW X6 xDrive 50i ililia mara mbili mbele ya geti la nyumba moja iliyopo katika mtaa wa Sonega eneo la Shaurimoyo, Ilala. Kijana mmoja mtanashati mwenye mwili wa kimazoezi akachungulia nje na kuliona lile gari kisha akaachia tabasamu na kufungua geti haraka, lile gari likazama ndani. Yule kijana ni Tom.
Muda huohuo wanaume wengine wawili wakatokea wakiwa tayari wameshika vifaa maalumu kwa ajili ya kuanza kazi ya uchunguzi, wakamtazama Tunu kwa macho ya kuuliza.
“Ninahisi gari hili limewekwa GPS device ili kuni-track waweze kujua kila ninapokwenda,” Tunu alisema.
Wale wanaume wakaanza kulikagua gari wakianzia kwenye sehemu za ndani ambazo magurudumu hufungwa kuona kama vifaa vya GPS vilikuwa vimepachikwa lakini hawakuona kitu, inaaminika kuwa kwa vyovyote mtu mtaalamu wa mambo hayo asingeweza kufunga kifaa kama hicho sehemu hiyo.
Wakafungua boneti la gari na kuchunguza kila sehemu kwa uangalifu sana, walikagua injini nzima kwa kutumia kioo maalumu na tochi lakini hawakuona chochote. Wakachunguza chini ya gari wakiiangalia injini kutokea chini hadi juu lakini hakukuwa na kifaa chochote cha GPS. Wakafungua siti za gari na kuangalia chini, pia hakukuwa na chochote.
Walipokosa maeneo yote hayo wakaondoa redio kwenye dashbodi na kuchunguza kwa ndani na kila sehemu, hakukuwa na kitu. Kisha wakaondoa paneli za milango na kava za spika na kuchunguza. Walipokosa wakaangalia kwenye mikono ya milango (handles) na kwenye vifungo vyake, wakakiona kifaa kimoja cha GPS kilichokuwa kimewekwa kitaalamu sana kwenye kifungo cha mkono wa mlango wa kushoto, kiasi cha kumfanya mtu asiye mjuzi wa mambo hayo asiweze kugundua.
Mambo yanazidi kunoga... Ili kujua nini kitaendelea endelea kuwemo kwenye safari hii ya kusisimua...
NB: Litro 👩🦱
Wacha wee 😂 😂🤣 a bee
Bishop ... ...
Thanks bishop, kweli nimeamini wauaji Mara nyingi hurudi kwenye eneo LA tukio, au msibani kama mtu baki, ili kusoma mchezo, ndo anachofanya Mr Oduya.Taxi - (118)

Kila navyosoma ndo hamu inaongezeka ya kutaka kujua kilichoendelea.... Duuh.... Uko vema braza.... Nenda hollywood we ni asset adimu sanaTaxi - (118)

huwa naangalia sana kipindi cha crime investigation, huwa wanasema hilo neno kuwa muuaji hurudi kwenye tukio ili kuona kinachoendeleaThanks bishop, kweli nimeamini wauaji Mara nyingi hurudi kwenye eneo LA tukio, au msibani kama mtu baki, ili kusoma mchezo, ndo anachofanya Mr Oduya.
Amnaaaaaa wapi hapooHalafu kama nimeona sehemu Bishop kaandika NB: Litro, ni wewe au?