Stori ya kusisimua - Taxi

Stori ya kusisimua - Taxi

Taxi - (109)

ILIPOISHIA

Tunu alilitazama lile gari kwa makini huku akijiuliza kuwa watu wale ni akina nani na kwa nini wamfuatilie. Je, ni watu wa Mr. Oduya? Akaanza kushikwa na wasiwasi, hata hivyo aliamua kuachana nao na kuyakaza macho yake kutazama mbele huku akajitahidi kulisahau gari lile kwa muda, aliipa utulivu akili yake ianze kufanya kazi.

Tayari muda wa dakika takribani kumi na tano ulikwisha yeyuka tangu Tunu alipotoka pale hospitali ya Amana, aligundua hivyo baada ya kuitazama saa yake ya mkononi iliyoonesha vizuri kupitia mishale yake ya dhahabu ilivyokuwa ikimetameta.

Baada ya sekunde chache alifikia uamuzi wa kuwapoteza kwa kuwa hakutaka watu wale wafahamu ni wapi alipokuwa akielekea. Akapanga kubadilisha mwelekeo. Aliutazama mshale wa mafuta ukamwonesha kuwa alikuwa na mafuta ya kutosha kuweza kuzunguka jiji la Dar es Salaam mpaka jioni bila kusimama. Akatabasamu na kuongeza mwendo.

* * * * *

Katika hospitali ya Amana, Sammy alikuwa ametulia nje ya chumba alimolazwa Joyce, alikuwa akitafakari kuhusu mazungumzo yake na Tunu huku akijaribu kujiuliza maswali yaliyokosa majibu. Alitamani sana kufahamu kilichotokea kwa Tunu, alikuwa wapi siku zote? Anafanya kazi gani?

Alikuwa na hamu kubwa ya kutaka kufahamu mengi kuhusu Tunu, ni wapi alikuwa katika kipindi hiki chote cha miaka kumi na moja tangu walipoachana! Pamoja na kupotezana miaka yote hiyo lakini bado Tunu aliendelea kuonekana mrembo sana. Alikuwa bado ni Gift yule yule mwenye mvuto wa ajabu.

Wakati akizidi kuwaza mara akawaona watu wawili wakija na walipofika karibu akawatambua mara moja, walikuwa wazazi wake Joyce, Bwana na Bibi Jengo. Akasimama na kuwalaki.

ENDELEA...

Bi. Pamela alipomwona Sammy alishindwa kujizuia, alifungua mdomo wake kutaka kusema lakini maneno hayakutoka, akabaki mdomo wazi akimkodolea macho Sammy huku donge la fadhaa likimkaba kooni. Akaangua kilio kwa uchungu.

“Mama Davie, usilie tafadhali. Joyce anatuhitaji sana hivyo tunatakiwa tuwe na ujasiri,” Jengo alisema huku akimkumbatia mkewe na kumpigapiga mgongoni.

“Baba Davie, hujui tu ninapitia kipindi gani kwa sasa, mwenyewe unajua tangu nilipopata taarifa hizi nimeshindwa hata kula...” Bi. Pamela alisema na kuchukua kitambaa laini, akafuta machozi.

“Mama, Joyce ni jasiri, naamini atashinda vita hii ya kupigania maisha yake, cha msingi tu tumuombee,” Sammy alisema huku akiwatazama wakwe zake kwa makini.

“Najua mwanangu, lakini nina uchungu, kwa nini wamfanyie hivi kwani kawakosea nini jamani!” Bi. Pamela alisema kwa huzuni. Kikatokea kitambo kifupi cha ukimya, Sammy akawataka waketi kwenye benchi lililokuwepo pale.

“Nataka kufahamu tukio hili limetokeaje?” Rafael Jengo alimuuliza Sammy baada ya kuketi.

“Ni kama nilivyokueleza kwenye simu, mimi sikuwepo nyumbani ila kwa maelezo ya mdogo wangu Winifrida, watu wawili walifika na kuwaweka chini ya ulinzi, shida yao kubwa ilikuwa ni mimi. Hadi sasa sijajua nani aliwapa polisi taarifa, ila wale watu walipogundua askari wameizingira nyumba ndipo wakampiga risasi Joyce na kutoroka,” Sammy alisema kwa huzuni.

“Muda huu nilijaribu kupiga tena simu polisi kujua kama kuna hatua yoyote waliyopiga au kuna mtu yeyote aliyekamatwa lakini mpaka sasa hawajafanikiwa na uchunguzi bado unaendelea,” Sammy alisema.

“Lakini, vipi hali ya Joyce?” Rafael Jengo aliuliza kwa wasiwasi.

“Tuendelee tu kumwombea aweze kupata nafuu maana hadi sasa hajazinduka, usiku walimfanyia oparesheni na kufanikiwa kutoa risasi mbili...” Sammy alisema na kusita kidogo. “Daktari ameniambia ukweli kwamba hali aliyo nayo sasa kupona ni hamsini kwa hamsini hivyo tujiandae kwa lolote litakalotokea,” Sammy alisema huku machozi yakimlengalenga machoni.

“Joyce wangu jamani!” Bi. Pamela alisema kwa uchungu mkubwa huku akishika kichwa, alionekana kusononeka sana. Mara kikohozi kidogo kikamtoka na nyuma yake wimbi la machozi lilikuja mbio. Alishindwa kujizuia na akapiga yowe dogo la kilio. Rafael Jengo na Sammy wakawa na kazi ya kumbembeleza.

Kwa muda wa dakika kadhaa hali ya mahali pale ikageuka kuwa ya simanzi kubwa. Kilio cha Bi. Pamela kikawafanya Rafael Jengo na Sammy wajikute wakitokwa na machozi pasipo kupenda.

“Mama Davie, tafadhali piga konde moyo ujizuie kumwaga machozi. Nimekwambia tunahitaji sana kuwa watu jasiri kwani Joyce anatuhitaji,” Rafael Jengo alimwambia mkewe huku akimfuta machozi. Akamshika bega, “Listen, ninamfahamu Joyce ni mpambanaji. She’ll fight this!

I know, and I’m trying my best... lakini sina uhakika na hali ya mwanangu hadi nimuone. Oh jamani mimi!” Bi. Pamela alisema huku akiendelea kulia.

Please, Mama Davie, eneo hili halihitaji kelele! Please!” Rafael Jengo alisema kwa ukali kidogo. “Usikate tamaa kirahisi hivi, naamini Mungu atamsaidia, si vyema kumwaga machozi eneo hili. Ningejua hali itakuwa hivi ningekuacha Tanga, na kama hautakuwa na ujasiri nitakurudisha Tanga leo hiihii!” Rafael Jengo alisema huku akishusha pumzi.

“Samahani, Baba Davie, nimekuelewa. Nitajitahidi ingawa inaniwia vigumu,” Bi. Pamela alisema huku akifuta machozi. “Ah, machozi yangu yawe dawa ya mwanangu na Mungu amponye,” alisema kwa sauti ya chini huku akishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani.

“Kwa hiyo, wanasemaje? Tunaweza kumwona mgonjwa?” Rafael Jengo alimuuliza Sammy.

“Mpaka sasa madaktari hawajaanza kuruhusu mtu kumwona, nadhani wanafanya utaratibu wa...” Sammy alikatishwa na simu ya Joyce aliyoishika iliyoanza kuita.

Aliitazama kwa makini na kuliona jina la Madame Norah kwenye kioo cha simu. Akashusha pumzi za ndani kwa ndani. “Samahani, ngoja nipokee kwanza hii simu,” Sammy alisema na kuipokea ile simu, akaipeleka kwenye sikio lake. “Hallo, Madame!”

“Hallo, baba, tayari nimeshafika hapa hospitali, sijui uko kwa wapi?” Madame Norah aliuliza.

“Njoo moja kwa moja huku chumba cha wagonjwa mahututi walio katika uangalizi maalumu.”

Okay, nipe dakika moja tu siko mbali na hapo,” Madame Norah alisema na kukata simu.

Sammy alishusha pumzi na kuitazama ile simu kwa makini kisha akairudisha mfukoni. Kabla hajajua aseme nini mara akamwona Madame Norah akipiga hatua zake haraka haraka kuelekea pale walipokuwa.

Madame Norah alionekana nadhifu sana akiwa amevaa suti ya rangi ya zambarau ya kitambaa ghali toka nchini Italia; suruali na koti, na ndani alikuwa amevaa blauzi nzuri ya rangi ya samawati. Usoni alivaa miwani mikubwa ya jua iliyoyafunika macho yake, mkufu wa dhahabu shingoni na miguuni alivaa viatu vya zambarau vyenye visigino virefu.

Akiwa takriban hatu kumi kabla hajawafikia, alisimama ghafla baada ya kuwaona watu wengine wawili wakiwa na Sammy, kilichomshtua zaidi ni yule mwanamume aliyekuwa amevaa suti nadhifu ya rangi ya kijivu na shati jeusi.

“Jengo?” Madame Norah alijiuliza kwa sauti ndogo huku akihisi miguu yake ikiishiwa nguvu. Aliivua miwani yake na kuishika mkononi. “Ni yeye kweli au nimemfananisha? Ni yeye, naamini macho yangu bado yana nguvu ya kutosha na sina shaka na kile ninachokiona,” Madame Norah alizidi kuwaza huku akimtazama Rafael Jengo kwa makini.

Sammy alishangaa kumwona Madame Norah akiwa amesimama akishangaa kama aliyeona kitu kigeni. “Vipi, mama, mbona unashangaa?” Sammy aliuliza kwa mshangao na kuwafanya Rafael Jengo na Bi. Pamela wageuze shingo zao kutazama kule ambako macho ya Sammy yalikuwa yanaangalia.

INAENDELEA...

CC the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater Bigjahman moneytalk marybaby nipo2 ram kisukari Smart911 Madame S carbamazepine Astelia culture gal Prisoner of hope Mine eyes kuku mweus Thad hearly Shunie Tumosa Mine eyes Kudo swahiba92 ludist Toyota escudo Clkey macson3 boga la kiangazi LEGE Smart911 Richard irakunda skfull popie Krizy Beat hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Mlenge Kacheda mjasiliamali Laki Si Pesa cocochanel kinusikwetu big jambo mludego Shupavu Kacheda mjasiliamali Mweweso Songa Heri esiankiki mnadhimu mkuu wa jf red apple the-sniper MR KUO dan oseko
🙏🙏shukran lakin kwa hasira za arosto fanya kama unatuma hata 3 kwa mkupuo🙄😇🤭
 
Taxi - (110)

They must,” Madame Norah alisema huku akiwaashiria wamfuate. Walielekea moja kwa moja kwenye ofisi ya wauguzi. Madame Norah akagonga mlango mara moja na kuufungua, akachungulia ndani ya ofisi na kuachia tabasamu, kisha akaingia akiwaacha akina Sammy wakisubiri nje ya ofisi.

Mle ndani ya ofisi aliwakuta wauguzi waliokuwa wanaongea na Daktari Mshana. Madame Norah alikuwa akifahamiana na Dk. Mshana na baadhi ya wauguzi, hivyo hakupata taabu kujieleza. Baada ya dakika chache za maongezi walitoka nje na kuelekea moja kwa moja katika chumba cha wagonjwa mahututi walio katika uangalizi maalumu.

Jengo na mkewe Bi. Pamela walifuata nyuma kimyakimya, hakuna aliyesema neno kati yao hadi muda ule. Sammy alikuwa bado anashangaa. Walipofika kwenye kile chumba cha wagonjwa mahututi walio katika uangalizi maalumu, wote walivalishwa mavazi maalumu mfano wa majoho, ya rangi ya samawati, kofia maalumu na vitambaa vya kufunika mdomo na pua, kisha wakaingia ndani.

Kilikuwa chumba kikubwa chenye vitanda viwili maalumu kwa wagonjwa mahututi, kikiwa na mitambo maalumu ya kupima mwenendo wa mapigo ya moyo, mashine maalumu za kuwasaidia wagonjwa kupumua na vifaa vingine vingi.

Walisimama wakimtazama Joyce aliyekuwa amelala kitandani kama mfu akiwa amevalishwa mashine maalumu ya kumsaidia kupumua huku skrini kubwa ya ukutani ikionesha mwenendo wa mapigo ya moyo wake. Mwili wake ulikuwa umezingirwa na nyaya mbalimbali zilizounganishwa na kompyuta kubwa. Kutokana na hali aliyokuwa nayo Joyce, watu wote walijikuta wakipatwa na simanzi kubwa.

Madame Norah alimsogelea Joyce, akamtazama kwa kitambo huku akilengwa na machozi, alijitahidi kuangua kilio na kushusha pumzi. “Please God, help her. We still need her,” Madame Norah aliomba kimya kimya huku akiyatuliza macho yake kumtazama Joyce na kuvuta pumzi ndefu kisha akazishusha taratibu.

“Joyce, najua unanisikia. Ni mimi Madame Norah... ni mimi mwandani wako, mama’ako, rafiki’ako na mentor wako. Najua wewe ni mpiganaji na hutakubali kushindwa. Najua bado unayo ndoto ya kufikia mafanikio yako katika maisha. Tafadhali usiondoke ukatuacha. Utakapoamka na kutoka hapa nitakueleza kwa nini tangu siku ya kwanza nilijihisi nina mzigo mkubwa sana wa kukusaidia kufanikisha ndoto yako, sikuwa najua lakini sasa najua. Ninakuhtaji sana mwanangu...” Madame Norah alisema kwa huzuni. Alishindwa kuendelea kumtazama Joyce na kuinamisha kichwa chake.

Kidevu chake kilianguka kifuani kwake, msirimbi wa kipaji cha uso wake ukaumuka, milizamu ikatutusika chini ya masikio yake kama iliyopulizwa, shingo yake ikavimba, mara kikamtoka kikohozi kikubwa na michirizi ya machozi ikapasuka machoni mwake. Sasa Madame Norah alishindwa kabisa kujizuia, akalia japo alijaribu sana kuyazuia machozi yasitoke lakini hakuweza. Sauti ya kilio chake ikaongezeka na sauti kubwa ya kilio ikasikika na kuwafanya wengine pia waanze kulia.

Kwa kitambo kifupi hali ndani ya kile chumba cha wagonjwa mahututi ilibadilika na kuwa ya simanzi kubwa, chumba kizima kikachakatika vilio vya kwikwi na nyuso zikafirigiswa katika viganja vya mikono.

Madame Norah alitoa leso yake iliyokunjwa kwa umaridadi na kupangusa macho yake akifuta machozi yaliyokuwa yakimtoka utadhani milizamu iliyopasuka. Alikuwa hajiwezi, alipenga kamasi zilizoanza kumtoka na kushusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani.

Dk Mshana hakupenda hali ile iendelee ndani ya kile chumba kilichohitaji utulivu wa hali ya juu, alimshika mkono Madame Norah na kumtoa nje ya kile chumba huku akiwata na wengine kutoka. Akina Sammy pia walishindwa kuidhibiti fadhaa iliyowajaa katika mioyo yao, walitoka nje ya kile chumba huku wakilia.

Kule nje ya kile chumba Madame Norah alisimama huku akiendelea kufuta machozi yaliyoendelea kumtoka. Dk. Mshana alimtazama kwa makini. “Ndiyo maana sikupenda kuruhusu watu kwa sasa kuingia mle ndani,” Dk. Mshana alisema huku akimtazama Madame Norah kwa makini.

“Dah! Imeniumiza sana... kwa kweli hali ya mwanangu inakatisha tamaa sana lakini naamini ni mpiganaji, nimemwambia apambane aamke ili tuendelee na miradi tuliyoianzisha, ninaamini amenisikia!” Madame Norah alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Hata mimi naamini kuwa ataamka muda si mrefu kutokana na ujasiri wake,” Sammy alisema huku akifuta machozi.

“Hivi ni nani hasa waliompiga risasi?” Madame Norah aliuliza.

“Mpaka sasa haifahamiki,” Sammy akajibu.

“Siku nikimjua aliyefanya hivi, nitakachomfanya naomba Mungu anisamehe...” Madame Norah alisema kwa hasira huku akipitisha kidole chake cha shahada shingoni na kukikung’uta hewani, kisha akamtazama Dk. Mshana. “Dokta, nakuomba fanya kila uwezalo kuhakikisha anaamka. Kama unadhani anahitaji kupelekwa Muhimbili utaniambia...” mara simu yake ya mkononi ikaanza kuita. Madame Norah aliitazama kwa makini na kushusha pumzi kisha akaipokea na kuiweka kwenye sikio.

“Hello, Mr. Mafuru, nipigie baadaye siko kwenye mood,” Madame Norah alisema kwa sauti yenye kitetemeshi.

“Madame... lakini tulikubaliana kukutana saa hizi kwa ajili ya kuandaa ile...” Mr. Mafuru alianza kujieleza lakini Madame Norah akamkatisha.

“Nisikilize, siwezi kufanya lolote kwa sasa wakati mwanangu yupo kitandani anapigania uhai wake. Sijui umenielewa?” Madame Norah aliongea kwa sauti kali iliyoonesha kukerwa.

“Oh samahani, sikujua. Kwani nani anaumwa maana sina taarifa?” Mr. Mafuru aliuliza kwa sauti iliyoonesha mshangao.

“Binti’angu, anaitwa Joyce. Walivamia nyumbani usiku na watu waliokuwa wanamtaka mumewe kisha wakampiga risasi. Hali yake siyo nzuri hivyo siwezi kufanya lolote kwa sasa...”

Oh my God!” Mr. Mafuru alisema na kuongeza, “Dah, ngoja nimweleze Mr. Oduya. Umesema yupo hospitali gani?”

“Amana.”

Okay, nashukuru kwa taarifa. See you later,” Mr. Mafuru alisema na kukata simu.

Mambo yanazidi kunoga, ni 🔥🔥🔥 kwelikweli. Je, nini kitafuata baada ya hapo? Itakuwaje pindi Mr. Oduya akijua kuwa aliyepigwa risasi ni mtoto wake Madame Norah na Sammy na mkwewe? Mimi sitii neno, endelea kufuatilia hadi mwisho...
 
Taxi - (109)

Macho ya Madame Norah yakagongana na yale ya Rafael Jengo na kumfanya Madame Norah ashushe pumzi na kuanza kupiga hatua taratibu kuwasogelea huku akiwa ameyatuliza macho yake usoni kwa Jengo.

“Mungu wangu! Nuru!” Rafael Jengo alimaka kwa mshtuko mkubwa. Alikuwa ameshika simu mkononi, ikamponyoka. Wakabaki wametazamana kwa sekunde kadhaa.

Bi. Pamela pia alionesha mshtuko mkubwa sana kumwona Madame Norah akiwa pale, alikuwa akimfahamu, siyo kwa kumwona kwenye runinga tu bali alishawahi kuambia habari zake na mumewe, Jengo. Bi. Pamela aliminya midomo yake yenye maki na mashavu yake yakapiga misingi, pembe za midomo zikafinya, akajitahidi kuficha wivu ulioanza kumkaba kooni.

Ni Sammy pekee ambaye hakujua kilichokuwa kinaendelea pale, alikuwa katika mshangao mkubwa.

Madame Norah aliwatazama Jengo na mkewe Bi. Pamela kwa zamu huku akihisi donge la fadhaa likianza kumkaba kooni. Kwa dakika kadhaa alishindwa kabisa kuongea na badala yake alisimama akiwa kimya kama aliyekuwa akisubiri kusomewa hukumu yake, machozi yalikuwa yanamlengalenga machoni.

“Hallo Nuru! Au sijui nikuite Madame Norah?” Jengo alisema baada ya kumwona Madame Norah akiwa amesimama kimya, uso umesawajika.

“Je-je-jeng…” Madame Norah alitaka kuita lakini akashindwa kutamka, mdomo wake ulikuwa unatetemeka. Kikapita kitambo kingine cha ukimya. “Dah! huu kwangu ni muujiza mkubwa sana, sikuwa nimetarajia kabisa kukukuta hapa!” Madame Norah alimudu kusema akiwa bado katika mshangao.

“Hukutarajia! Basi karibu. Kuna nini mbona uko hapa?” Jengo alimuuliza Madame Norah huku akimkazia macho.

“Nimekuja kumwona mwandani wangu Joyce. Na wewe unafanya nini hapa?” Madame Norah alimuuliza Jengo huku akimkazia macho.

“Joyce! Inamaana tayari mnafahamiana?” Jengo aliuliza kwa mshangao mkubwa.

Of course! Ni mwandani wangu na mshirika wangu, kwani vipi! Kuna tatizo lolote?” Madame Norah aliuliza huku akishindwa kuuficha mshangao wake.

Jengo alitaka kusema neno lakini akasita na kumtazama mkewe Bi. Pamela, macho yao yakakutana. Hakuna aliyesema neon, Jengo akashusha pumzi za ndani kwa ndani. Alikuwa amepatwa na mshtuko mkubwa sana asioutarajia. Alionekana kama mtu aliyepigwa na shoti kali ya umeme na hakuamini alichokisikia toka kwenye kinywa cha Madame Norah.

Madame Norah aliugundua mshtuko huo, akamtazama Sammy huku akishindwa kuuficha wasiwasi wake. “Kwani kuna nini kinaendelea hapa, baba’angu?”

“Sijui, lakini hawa ndio wazazi wake na Joyce,” Sammy alijibu kwa sauti tulivu huku mshangao ukiwa haujamtoka usoni.

“Jengo ndiye baba’ake na Joyce!” ikawa zamu ya Madame Norah kupatwa na mshangao mkubwa. Sammy alibetua kichwa chake kukubali.

Madame Norah alimtazama Jengo kwa makini pasipo kupepesa macho yake. “Is Joyce our daughter?” alimuuliza huku akihisi kuchanganyikiwa. Alikuwa bado amemtulizia macho usoni.

Not our daughter, she is my daughter,” Jengo alijibu kwa sauti kavu huku akiwa amekunja sura yake.

“Na binti yetu yuko wapi?” Madame Norah akauliza huku akizidi kumkazia macho Jengo. Safari hii alionekana kuwa serious zaidi.

“Huoni aibu kuuliza swali kama hilo! Siye wewe uliyembwaga na kupotelea kusikojulikana? Leo unathubutu vipi kuuliza habari ya mtoto! Shame on you!” Jengo aliongea kwa hasira huku akimkazia macho Madame Norah.

Stop! Ni wewe chanzo cha yote haya. Kumbuka nilikuwa msichana mdogo wakati huo, ni wewe uliyenilaghai na ulipogundua nimepata ujauzito ukanifukuza nyumbani kwako kama mbwa, mbele ya malaya wako. Unajua ni mateso gani niliyoyapata? Unajua kuwa nilikaribia kujiua baada ya kuona dunia yote imenitenga, ukiwemo wewe?” Madame Norah alikuja juu, aliongea kwa uchungu na hasira.

“Nimeteseka miezi tisa na ujauzito, isingekuwa rafiki yangu kunifadhili hadi nikajifungua salama hata sijui ingekuwaje, lakini bado hukujali. Leo hii unaweza kusimama hapa na kunitukana kiasi hiki! Inatosha, naomba tuheshimiane,” Madame Norah alizidi kuongea kwa uchungu na hasira, safari hii kwa sauti ya juu iliyokaribia kupiga kelele.

Jengo alitaka kusema neno lakini akahisi hatia ikimkaba kooni, alishindwa kutamka neno na kugeuza shingo yake kumtazama mkewe kwa wasiwasi. Bi. Pamela alikuwa yupo kimya kabisa muda wote kana kwamba mambo yale yalikuwa hayamhusu kabisa. Uso wake ulionesha kukwazika ingawa alijizuia kusema lolote. Kikatokea kitambo kirefu cha ukimya, kila mmoja alikuwa anawaza la kwake.

“Mzee, samahani... kwani Joyce ni mtoto wa Madame Norah?” Sammy alimuuliza Jengo kwa mshangao huku akionekana kuchanganyikiwa kidogo.

Jengo alishindwa kujibu, alimtazama kwanza mkewe Bi. Pamela kisha akayahamisha macho yake kumtazama Madame Norah na mwisho akamalizia kwa Sammy na kushusha pumzi ndefu, akabetua kichwa chake kukubali na kuinamisha kichwa chake chini.

Oh my God!” Sammy alimaka kwa mshtuko mkubwa. “Dah! Hili kwangu ni jambo jipya kabisa,” Sammy alisema huku akishindwa kabisa kuuficha mshangao wake. Hakuamini kabisa kile alichokishuhudia mbele yake. Kikatokea tena kitambo kifupi cha ukimya kila mmoja akijaribu kutafakari hili na lile.

“Nahitaji kumwona binti’angu. I need to talk to her,” Madame Norah alisema kwa sauti tulivu huku akimwangalia Sammy.

“Sijui kama wataruhusu, hadi sasa hakuna aliyeruhusiwa kumwona...” Sammy alisema kwa wasiwasi.

Inaendelea...
ndo maana nakupenda buree unajua kutukonga nyoyo zetu😊😊😙i
 
Taxi - (110)

They must,” Madame Norah alisema huku akiwaashiria wamfuate. Walielekea moja kwa moja kwenye ofisi ya wauguzi. Madame Norah akagonga mlango mara moja na kuufungua, akachungulia ndani ya ofisi na kuachia tabasamu, kisha akaingia akiwaacha akina Sammy wakisubiri nje ya ofisi.

Mle ndani ya ofisi aliwakuta wauguzi waliokuwa wanaongea na Daktari Mshana. Madame Norah alikuwa akifahamiana na Dk. Mshana na baadhi ya wauguzi, hivyo hakupata taabu kujieleza. Baada ya dakika chache za maongezi walitoka nje na kuelekea moja kwa moja katika chumba cha wagonjwa mahututi walio katika uangalizi maalumu.

Jengo na mkewe Bi. Pamela walifuata nyuma kimyakimya, hakuna aliyesema neno kati yao hadi muda ule. Sammy alikuwa bado anashangaa. Walipofika kwenye kile chumba cha wagonjwa mahututi walio katika uangalizi maalumu, wote walivalishwa mavazi maalumu mfano wa majoho, ya rangi ya samawati, kofia maalumu na vitambaa vya kufunika mdomo na pua, kisha wakaingia ndani.

Kilikuwa chumba kikubwa chenye vitanda viwili maalumu kwa wagonjwa mahututi, kikiwa na mitambo maalumu ya kupima mwenendo wa mapigo ya moyo, mashine maalumu za kuwasaidia wagonjwa kupumua na vifaa vingine vingi.

Walisimama wakimtazama Joyce aliyekuwa amelala kitandani kama mfu akiwa amevalishwa mashine maalumu ya kumsaidia kupumua huku skrini kubwa ya ukutani ikionesha mwenendo wa mapigo ya moyo wake. Mwili wake ulikuwa umezingirwa na nyaya mbalimbali zilizounganishwa na kompyuta kubwa. Kutokana na hali aliyokuwa nayo Joyce, watu wote walijikuta wakipatwa na simanzi kubwa.

Madame Norah alimsogelea Joyce, akamtazama kwa kitambo huku akilengwa na machozi, alijitahidi kuangua kilio na kushusha pumzi. “Please God, help her. We still need her,” Madame Norah aliomba kimya kimya huku akiyatuliza macho yake kumtazama Joyce na kuvuta pumzi ndefu kisha akazishusha taratibu.

“Joyce, najua unanisikia. Ni mimi Madame Norah... ni mimi mwandani wako, mama’ako, rafiki’ako na mentor wako. Najua wewe ni mpiganaji na hutakubali kushindwa. Najua bado unayo ndoto ya kufikia mafanikio yako katika maisha. Tafadhali usiondoke ukatuacha. Utakapoamka na kutoka hapa nitakueleza kwa nini tangu siku ya kwanza nilijihisi nina mzigo mkubwa sana wa kukusaidia kufanikisha ndoto yako, sikuwa najua lakini sasa najua. Ninakuhtaji sana mwanangu...” Madame Norah alisema kwa huzuni. Alishindwa kuendelea kumtazama Joyce na kuinamisha kichwa chake.

Kidevu chake kilianguka kifuani kwake, msirimbi wa kipaji cha uso wake ukaumuka, milizamu ikatutusika chini ya masikio yake kama iliyopulizwa, shingo yake ikavimba, mara kikamtoka kikohozi kikubwa na michirizi ya machozi ikapasuka machoni mwake. Sasa Madame Norah alishindwa kabisa kujizuia, akalia japo alijaribu sana kuyazuia machozi yasitoke lakini hakuweza. Sauti ya kilio chake ikaongezeka na sauti kubwa ya kilio ikasikika na kuwafanya wengine pia waanze kulia.

Kwa kitambo kifupi hali ndani ya kile chumba cha wagonjwa mahututi ilibadilika na kuwa ya simanzi kubwa, chumba kizima kikachakatika vilio vya kwikwi na nyuso zikafirigiswa katika viganja vya mikono.

Madame Norah alitoa leso yake iliyokunjwa kwa umaridadi na kupangusa macho yake akifuta machozi yaliyokuwa yakimtoka utadhani milizamu iliyopasuka. Alikuwa hajiwezi, alipenga kamasi zilizoanza kumtoka na kushusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani.

Dk Mshana hakupenda hali ile iendelee ndani ya kile chumba kilichohitaji utulivu wa hali ya juu, alimshika mkono Madame Norah na kumtoa nje ya kile chumba huku akiwata na wengine kutoka. Akina Sammy pia walishindwa kuidhibiti fadhaa iliyowajaa katika mioyo yao, walitoka nje ya kile chumba huku wakilia.

Kule nje ya kile chumba Madame Norah alisimama huku akiendelea kufuta machozi yaliyoendelea kumtoka. Dk. Mshana alimtazama kwa makini. “Ndiyo maana sikupenda kuruhusu watu kwa sasa kuingia mle ndani,” Dk. Mshana alisema huku akimtazama Madame Norah kwa makini.

“Dah! Imeniumiza sana... kwa kweli hali ya mwanangu inakatisha tamaa sana lakini naamini ni mpiganaji, nimemwambia apambane aamke ili tuendelee na miradi tuliyoianzisha, ninaamini amenisikia!” Madame Norah alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Hata mimi naamini kuwa ataamka muda si mrefu kutokana na ujasiri wake,” Sammy alisema huku akifuta machozi.

“Hivi ni nani hasa waliompiga risasi?” Madame Norah aliuliza.

“Mpaka sasa haifahamiki,” Sammy akajibu.

“Siku nikimjua aliyefanya hivi, nitakachomfanya naomba Mungu anisamehe...” Madame Norah alisema kwa hasira huku akipitisha kidole chake cha shahada shingoni na kukikung’uta hewani, kisha akamtazama Dk. Mshana. “Dokta, nakuomba fanya kila uwezalo kuhakikisha anaamka. Kama unadhani anahitaji kupelekwa Muhimbili utaniambia...” mara simu yake ya mkononi ikaanza kuita. Madame Norah aliitazama kwa makini na kushusha pumzi kisha akaipokea na kuiweka kwenye sikio.

“Hello, Mr. Mafuru, nipigie baadaye siko kwenye mood,” Madame Norah alisema kwa sauti yenye kitetemeshi.

“Madame... lakini tulikubaliana kukutana saa hizi kwa ajili ya kuandaa ile...” Mr. Mafuru alianza kujieleza lakini Madame Norah akamkatisha.

“Nisikilize, siwezi kufanya lolote kwa sasa wakati mwanangu yupo kitandani anapigania uhai wake. Sijui umenielewa?” Madame Norah aliongea kwa sauti kali iliyoonesha kukerwa.

“Oh samahani, sikujua. Kwani nani anaumwa maana sina taarifa?” Mr. Mafuru aliuliza kwa sauti iliyoonesha mshangao.

“Binti’angu, anaitwa Joyce. Walivamia nyumbani usiku na watu waliokuwa wanamtaka mumewe kisha wakampiga risasi. Hali yake siyo nzuri hivyo siwezi kufanya lolote kwa sasa...”

Oh my God!” Mr. Mafuru alisema na kuongeza, “Dah, ngoja nimweleze Mr. Oduya. Umesema yupo hospitali gani?”

“Amana.”

Okay, nashukuru kwa taarifa. See you later,” Mr. Mafuru alisema na kukata simu.

Mambo yanazidi kunoga, ni 🔥🔥🔥 kwelikweli. Je, nini kitafuata baada ya hapo? Itakuwaje pindi Mr. Oduya akijua kuwa aliyepigwa risasi ni mtoto wake Madame Norah na Sammy na mkwewe? Mimi sitii neno, endelea kufuatilia hadi mwisho...
😁 😁 😁 na kanyiongeza kama 3 vinginee🙄🙄🤭 kufidia arostooo😛
 
Mambo yanazidi kunoga, ni kwelikweli. Je, nini kitafuata baada ya hapo? Itakuwaje pindi Mr. Oduya akijua kuwa aliyepigwa risasi ni mtoto wake Madame Norah na Sammy na mkwewe? Mimi sitii neno, endelea kufuatilia hadi mwisho...

You are good.
 
Kitawaka huko mbele, ila nilishatabiri kuwa Joyce na madame huenda wakawa ni mtu na mwanawe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom