Taxi - (101)
ILIPOISHIA
Pamoja na kuendelea kumfuata yule dereva lakini Tunu bado alikuwa katika mawazo kumuhusu yule dereva. Alikuwa anajiuliza yule nin nani hasa? Kwa nini amemwokoa toka kwa wale watu wakati inasemekana yeye pia ni mmoja wao? Je, katumwa na nani aje amwokoe? Au yeye pia ni
undercover? Tunu alijiambia kuwa alikwisha hisi tangu mwanzo kuwa yule dereva hakuwa wa kawaida kama walivyo madereva wengine, alionekana mwelewa sana wa mambo na mwepesi wa kushika maelekezo.
Waliendelea kukimbia kwa kasi, yule dereva akiwa mbele na Tunu akiwa nyuma ingawa kwa upande fulani alianza kumwogopa sana. Jasho jingi lilikuwa linamtoka kwa kukimbia. Baada ya dakika kadhaa za kukimbia wakatokea kwenye kichochoro kimoja na kuikuta ile taxi ikiwa imeegeshwa hapo. Yule dereva akageuka kumtazama Tunu kwa macho makali.
“Pole sana, huo ndiyo uzalendo kwa nchi yako,” yule dereva alisema lakini Tunu hakumjibu. Alimtazama usoni kwa makini.
SASA ENDELEA...
“Panda tuondoke, hapa pia si mahala salama. Bado tunakabiliwa na hatari kubwa,” yule dereva alisema huku akifungua mlango na kuingia ndani ya gari. Tunu naye akaingia na gari likaondoka kwa mwendo wa kasi.
* * * * *
Saa saba usiku katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala, ya Amana, Sammy alikuwa amesimama jirani na mlango wa chumba cha upasuaji uliokuwa umefungwa na hakuruhusiwa mtu asiyehusika kuingia ndani ya chumba kile, aliamua asubirie pale nje huku akijaribu kuchungulia mle ndani kupitia kioo kikubwa cha mlangoni.
“Ee Mungu, naomba umponye mke wangu, Joyce,” Sammy alikuwa akiomba Mungu kimoyomoyo na aliendelea kuyatamka maneno hayo mara kwa mara.
Elli alikuwa ameketi kando kwenye benchi akiwa amejiinamia kwa huzuni, mambo mengi yalipita kichwani kwake akijaribu kuwaza na kuwazua hili na lile pasipo kupata majibu.
“Maskini mke wangu, tafadhali usiniache... Tafadhali usiondoke na kuniacha na mtoto!” Sammy aliwaza huku akichungulia ndani ya kile chumba cha upasuaji kupitia kile kioo.
Hadi muda ule hali ya Joyce iliendelea kuwa tete na Sammy hakuwa ameketi wala kubanduka pale karibu na mlango, alikuwa akifuatilia kwa karibu sana kila hatua akihofia hali ya mkewe.
Alianza kujiuliza, ni nani waliomshambulia Joyce? Je, shida yao ilikuwa kuiba au kuna kitu walikuwa wakikihitaji? Nini walikuwa wanakihitaji kutoka kwake? Je, kulikuwa na uhusiano wowote kati ya simu aliyopigiwa na Joyce kuwa Pendo amezidiwa na tukio lile la kuvamiwa na kupigwa risasi? Kilichomshangaza ni pale alipofika nyumbani akamkuta Pendo mzima wa afya akiwa hana dalili yoyote ya kuumwa.
“Hii inaweza kuwa nini maana yake?” Sammy akajiuliza. Akiwa ametulia akitafakari mara akaona mlango wa kile chumba cha upasuaji ukifunguliwa na mhudumu mmoja wa chumba cha upasuaji akatoka. Alikuwa mwanamke mrefu aliyekuwa amevaa mavazi rasmi ya hospitali. Alipotaka kupiga hatua Sammy na Elli wakamkabili ili kujua hali ya Joyce.
“Bado yuko kwenye upasuaji. Endeleeni kusubiri hadi upasuaji ukimalizika mtajulishwa kila kitu,” yule mhudumu alisema na kuendelea na safari yake.
Sammy alishusha pumzi na kushika kiuno chake kwa mikono yote miwili, ni wazi alionekana kukata tamaa. Elli alimtazama Sammy kwa huzuni na kumshika kwenye bega.
“Sammy, hebu kaa utulie, ukiendelea kusimama hapa utachoka sana kwani hatujui upasuaji utachukua muda gani, yawezekana ukachukua muda mrefu,” Elli alimsihi Sammy.
“Nashindwa kukaa, Elli. Ninapata wakati mgumu sana ni kwa vile hujui tu,” Sammy alijibu huku machozi yakimlengalenga machoni na mara akakumbuka jambo na kuchukua simu yake, akatafuta namba fulani na kupiga, kisha akaweka simu kwenye sikio lake. Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokewa hadi ikakata. Akapiga tena, simu ikaita mara moja tu na kupokewa.
“Hallo!” sauti ya mwanamume upande wa pili wa simu ikasikika mara baada ya simu kupokewa. Sammy aliitambua sauti ile, ilikuwa sauti ya Rafael Jengo, baba’ake Joyce.
“Shikamoo, mzee wangu!” Sammy alisalimia kwa unyenyekevu, hata hivyo uso wake haukuficha wasiwasi wake.
“Marhaba, mwanangu, vipi mbona usiku sana, kwema huko?” sauti ya upande wa pili wa simu ikasikika ikiuliza kwa wasiwasi.
“Kuna tatizo, mzee wangu... niko hapa hospitali, Joyce amepigwa risasi na watu wasiojulikana...” Sammy alianza kuelezea lakini sauti upande wa pili wa simu ikamkata kauli.
“Tafadhali usinitanie,” Mzee Jengo alisema kwa sauti ya kutetemeka akionekana kushtushwa sana na taarifa zile.
“Si utani, baba’angu, ni kitu cha kweli kabisa. Tupo hapa hospitali ya Amana na Joyce yupo katika chumba cha upasuaji,” Sammy alisema huku hofu ikimtambaa mwilini mwake.
“Mungu wangu!” Mzee Jengo alimaka kwa mshtuko, alihisi moyo wake ukipoteza mapigo yake. Kikatokea kitambo fulani cha ukimya. “Amepigwa risasi saa ngapi na imetokeaje?” hatimaye Mzee Jengo aliuliza baada ya kile kitambo cha ukimya.
“Mimi sikuwepo nyumbani, ilikuwa
around saa nne usiku kuelekea saa tano, watu wawili walivamia nyumbani wakiwa na pikipiki, inasemekana walikuwa wamevaa mavazi yaliyoficha sura zao zisiweze kutambulika...” Sammy alisema na kushusha pumzi, akafuta machozi yaliyokuwa yakimlengalenga machoni.
Kikapita tena kitambo kingine cha ukimya, kisha Mzee Jengo akashusha pumzi ndefu, “Ahsante sana kwa taarifa hii. Ngoja nimwambie na mama’ake, kesho mchana tutakuwa hapo,” alisema na kukata simu.
Sammy alibaki akiitazama simu yake kana kwamba alikuwa akiiona kwa mara ya kwanza. Hata hivyo, mawazo hayakuwa kwenye ile simu. Baada ya kitambo aliirudisha simu yake mfukoni kisha wakaendelea kukaa pale nje kwa muda mrefu. Ilipotimia saa kumi na moja alfajiri ndipo daktari mmoja alitoka na kuwapa taarifa.
Aliitwa Daktari Mshana, alikuwa mtu mzima, mrefu wa futi sita na ushee, mweupe na mwembamba aliyekuwa na macho ya upole. Aliwatazama Sammy na Elli kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.
“Vipi, daktari, vipi hali ya mgonjwa wetu?” Elli aliuliza kwa wasiwasi.
“Poleni sana kwa kusubiri. Upasuaji umefanikiwa kwa asilimia mia moja, tumeweza kuondoa risasi mbili mwilini mwake zilizopigwa mgongoni lakini hazikuleta madhara makubwa kwake wala kwa mapacha aliowabeba tumboni. Kwa sasa atapelekwa katika chumba cha uangalizi maalumu huku tukiangalia hali yake kwa ukaribu zaidi,” yule daktari alisema.
Sammy na Elli wakatazama, ulikuwa mtazamo wa matumaini. Hata hivyo, suala la Joyce kuwa na mimba ya mapacha lilikuwa geni kwa Sammy. Alifumba macho yake na kushusha pumzi.
“Daktari tunakushukuru sana kwa kazi kubwa mliyoifanya, sijui tunaruhusiwa kumwona?” Sammy alisema huku akiwa bado ameyafumba macho yake. Machozi ya furaha yalionekana machoni pake.
Inaendelea...
CC
the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater Bigjahman moneytalk marybaby nipo2 ram kisukari Smart911 Madame S carbamazepine Astelia culture gal Prisoner of hope Mine eyes kuku mweus Thad hearly Shunie Tumosa Mine eyes Kudo swahiba92 ludist Toyota escudo Clkey macson3 boga la kiangazi LEGE Smart911 Richard irakunda skfull popie Krizy Beat hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Mlenge Kacheda mjasiliamali Laki Si Pesa cocochanel kinusikwetu big jambo mludego Shupavu Kacheda mjasiliamali Mweweso Songa Heri esiankiki mnadhimu mkuu wa jf red apple the-sniper MR KUO