Stori ya kusisimua - Taxi

Stori ya kusisimua - Taxi

Dah nilitaka kumwambia Sasa hivi aisee inaboa kinyama.mara kioo.mara shati.mara suluali Mara Nini dsh
Kwani umeitwa hapa au unataka kujishauwa? Unakuja kwa ID tofauti ili iweje? Pumbavu. Usitake kutuchafulia hali ya hewa na roho yako ya kichawi, kama vipi kasome za baba yako.
 
Bahati nzuri au mbaya Mimi sizozani na watu wasionijua au nisiowajua. Ila hujatumia busara kunitukana, usiamini katika matusi ndugu mdau.

Any way naomba tuishie hapa.
 
Taxi - (98)

ILIPOISHIA

Spoiler alikuwa amesimama katika eneo la makaburi ya Vingunguti yaliyopo katika bonde la Mto Msimbazi baada ya kutoka nyumbani kwa Sammy eneo la Tabata Chang’ombe. Eneo lile la makaburi ya Vingunguti lilikuwa moja ya maeneo yaliyotisha sana kutokana na sifa yake ya kuwa eneo hifadhi la wahalifu waliokuwa wakivizia wapita njia ili kuwakaba na kuwaibia mali zao.

Spoiler alifika eneo lile baada ya purukshani nyingi barabarani, laiti kama asingekuwa mzoefu wa harakati kama zile angekamatwa au angeuawa. Nguo zake zilikuwa zimetapakaa damu. Aliutazama mwili wa Dulla Mcomoro ambao haukuwa na uhai wakati huo jinsi ulivyolala kifudifudi juu ya pikipiki. Alitamani kuutupa pale makaburini lakini aliogopa ingeweza kuwaletea shida baadaye kwa kuwa Dulla alikuwa anafahamika kuwa na ukaribu na Mr. Oduya.

ENDELEA...

Spoiler alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiwa makini sana kuhakikisha hakuna mtu aliyekuwa anamwona pale kizani alipokuwa amejificha.

Sasa alianza kumfikiria Tunu. Alikuwa na uhakika kuwa Tunu hakuwa mwanamke wa kawaida. Alikuwa ni zaidi ya vile walivyokuwa wakimchukulia, alikuwa ni shushushu aliyebobea ambaye mara nyingi aliutumia uzuri wake kuwaingia wanaume na kupata taarifa alizozihitaji.

Spoiler aliyakumbuka maneno ya Mr. Oduya kuwa Sammy aliondoka na wanaume wengine wawili ndani ya gari lake baada ya maongezi yake na Tunu, Spoiler akaamini kabisa kuwa sasa kazi ilikuwa ngumu tofauti na alivyodhania mwanzo kwani ingehitajika nguvu ya ziada. Kama mwanzoni walimchukulia Sammy kama mtu mmoja sasa hakuwa peke yake, waliongezeka Tunu na watu wengine wawili ambao hakuwajua.

Spoiler alihisi mwili wake ukimsisimka, kwa hasira akageuka nyuma na kutaka kuanza kuondoka pale alipokuwa amejificha lakini akasita baada ya kukutana na sura za wanaume wawili walioonekana wamebobea kwa uhalifu. Wale wanaume walikuwa na miili iliyojengeka imara na walikuwa wakimtazama Spoiler kwa tabasamu la kifedhuli.

Mmoja alikuwa mrefu na mweusi kama Mjaluo, macho yake yalikuwa makubwa na mekundu yenye uchovu lakini yaliyokuwa makini sana. Alikuwa na kovu kubwa chini ya jicho lake la kushoto. Alivaa suruali ya jeans iliyochanwachanwa sehemu ya mapaja na fulana nyeusi, kichwani alijifunga kitambaa chenye rangi mchanganyiko wa nyekundu, njano na kijani kikiwa na alama ya mche wa bangi.

Mwingine alikuwa mfupi lakini mwenye mwili uliojengeka, alikuwa na uso mrefu uliotulia kama maji mtungini, alivaa magwanda mfano wa kombati na kichwani alikuwa na upara unaowaka na usiokuwa na unywele hata mmoja. Kichwani alikuwa na ngeu na mishipa ya damu ilionekana kutuna na kusambaa kichwani kama mizizi ya mmea wa nafaka. Uso wake pia ulikuwa na makovu.

Spoiler aliwatazama kwa makini huku akijaribu kuwapima. Mapigo ya moyo wake yalianza kumwenda mbio huku baridi nyepesi ikisafiri katika maungo yake. Hali ile ilimfanya ahisi kuwa maficho yale hayakuwa salama tena, hivyo angelazimika kuondoka pale haraka iwezekanavyo na kutafuta chimbo jingine.

Wale watu walimsogelea taratibu, mikononi walikuwa wameshika silaha kama jambia na nondo tayari kwa lolote. Akili ya Spoiler ikafanya kazi haraka, bila kuchelewa alichomoa kisu chake kwenye ala, akakirusha kiustadi na kwenda kumchoma yule mtu mfupi upande wa kushoto wa kifua kwenye moyo. Alianguka chini huku akipiga yowe dogo.

Kabla yule mwanamume mrefu na mweusi kama Mjaluo hajakaa sawa wala kuelewa kilichotokea, Spoiler tayari alishadaka kisu kingine kutoka kwenye begi lake dogo la mgongoni na kuruka sarakasi ya chinichini kisha akamcharanga shingo yake na kukichomoa kile kisu kwa fujo huku akimwacha yule mwanamume akidondoka kama mzigo wa gunia la mahindi akiwa tayari maiti. Spoiler akakifuta damu na kumfuata yule mtu wa pili, akakichomoa kile kisu kilichokita kwenye moyo kwa fujo huku akihakikisha kuwa wote hawataamka tena.

Sasa alikuwa amepandwa na hasira kali ambazo zilimfanya kuanza kuzungukazunguka eneo lile. Mara simu yake ikaanza kutetema. Aliitoa na kuitazama kwa makini, ilikuwa ni simu kutoka kwa Mr. Oduya. Spoiler aliipokea haraka na kuiweka kwenye sikio. “Ndiyo, Boss!” Spoiler alisema huku akishusha pumzi ndefu.

“Una uhakika hapo upo sehemu salama ambayo huwezi kushtukiwa?” Mr. Oduya aliuliza kwa sauti ilionekana kuwa ‘serious’ tofauti na mwanzo, kwa mbali tumbo lake lilikuwa linamuuma.

“Si mahala salama sana, nipo makaburini na nimetoka kupambana na wahalifu wawili sasa hivi waliotaka kunidhuru,” Spoiler alisema huku akishusha pumzi.

“Okay, nimemtuma Job anakuja, atakupigia simu akikaribia hapo ili akupeleke Karakata ukaungane na kina Lisa na Uledi. Uledi kanipigia simu, ameniambia Tunu alikuwa anawafuatilia lakini tayari ameingia kwenye mtego na Lisa ameshamdhibiti,” Mr. Oduya alisema kisha akakata simu.

Mzuka wa unyama ukazidi kumpanda Spoiler, alijikuta akisisimkwa zaidi mwili wake tayari kwa mapambano. Alitamani aote mabawa ili apae angani na kumfikia Tunu kisha amwoneshe kile kilichomnyoa kanga manyoya ya shingoni.

* * * * *

“Tupa chini mkoba wako na ugeuke ukutani wewe kahaba na unyanyue mikono yako juu, utulie hivyo hivyo, ukijitikisa tu nitakifumua kichwa chako,” Lisa alimwonya Tunu huku akiwa ameshika vyema bastola yake akiielekeza kichwani kwake.

“Sawa, kahaba mkubwa!” Tunu alijibu kwa jeuri na kuutupa chini mkoba wake huku akigeuka.

“Sasa utafuata kile nitakachokwambia na usijidanganye kufanya utundu wa namna yoyote kwani sitokuvumilia,” Lisa alifoka.

“Sawa!” Tunu alijibu tena.

Lisa alimsogelea kwa tahadhari huku akiwa yupo makini zaidi, akaanza kumpekua mwilini huku mkono wake mmoja ukiwa bado umeielekeza bastola yake kisogoni kwa Tunu tayari kufyatua risasi endapo angeleta utata. Katika upekuzi wake alipata bastola moja ndogo aina ya Glock 19M ambayo hutumiwa na wapelelezi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI). Bastola hiyo Tunu alikuwa ameifutika kiunoni.

Alipomaliza kumpekua akauchukua ule mkoba na kumwamuru aanze kupiga hatua. Tunu alibaki akiwa amesimama asijue anatakiwa kupiga hatua kuelekea wapi!

“Tembea mbele kahaba mkubwa wewe!”

“Natembea kuelekea wapi? Kwenda kujiuza!” Tunu aliuliza kwa kebehi akijifanya haelewi somo.

“Fuata ninachosema, mimi huwa sipendi maswali maswali ya kijinga. Nataka uelekee ndani, umenielewa?” Lisa alisema kwa kufoka.

Inaendelea...

CC the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater Bigjahman moneytalk marybaby nipo2 ram kisukari Smart911 Madame S carbamazepine Astelia culture gal Prisoner of hope Mine eyes kuku mweus Thad hearly Shunie moneytalk Tumosa Mine eyes Kudo swahiba92 ludist Toyota escudo Clkey macson3 boga la kiangazi LEGE Smart911 Richard irakunda skfull popie Krizy Beat hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Mlenge Kacheda mjasiliamali Laki Si Pesa cocochanel kinusikwetu big jambo mludego Shupavu Kacheda mjasiliamali Mweweso Songa Heri esiankiki mnadhimu mkuu wa jf red apple the-sniper MR KUO
 
Taxi - (99)

“Nimekuelewa!” Tunu alisema na kuanza kupiga hatua.

Safari ya kueleka ndani ikaanza, Tunu alikuwa ametangulia mbele akiwa amenyanyua mikono yake juu na wakati huo bastola ya Lisa ikiwa nyuma yake ikiendelea kumgusa kisogoni. Hasira zilikuwa zimemshika kwa kuingia mikononi mwa Lisa, hata hivyo aliendelea kujifanya ameishiwa ujanja ili aweze kulichunguza vyema lile jumba.

Wakati wanatembea alifikiria kufanya shambulizi la kushtukiza lakini akajionya kuwa kufanya uamuzi wowote wa kukurupuka kwa kipindi kile usingekuwa na tija yoyote na badala yake alitakiwa kusubiri kwanza hadi hapo ambapo muda mwafaka ungewadia.

Walizunguka kutoka kule nyuma ya nyumba na kutokezea upande wa mbele wa ile nyumba na wakati wote huo Tunu alikuwa akiyachunguza mandhari ya nyumba ile huku pia akiupima uimara wa Lisa. Walipofika kwenye mlango wa mbele Lisa akamwamuru Tunu ausukume ule mlango na kuingia, kwani ulikuwa umerudishiwa tu, haukuwa umefungwa kabisa.

Wakaingia na kutokea sebuleni. Ilikuwa ni sebule kubwa yenye samani zote za kisasa. Tunu aliendelea kupiga hatua huku macho yake yakizunguka kulichunguza eneo lile kama kulikuwa na watu au mtu mwingine yoyote.

“Simama,” Lisa aliamuru na Tunu akasimama huku akiyazungusha macho yake, hakuweza kumwona mtu mwingine pale sebuleni ingawa hali hiyo haikumshawishi aamini kuwa Lisa alikuwa peke yake mle ndani.

“Kwani wengine wako wapi?” Tunu aliuliza huku anatafuta namna ya kujiokoa toka mikononi mwa Lisa, alitazama kando kwenye dirisha na kuachia tabasamu.

“Sikukwambia kuwa sipendi maswali ya kijinga, we kahaba?” Lisa alifoka.

“Sawa, kahaba mwenzangu!” Tunu alisema huku akiangalia kwenye dirisha na kubetua kichwa chake kwa tabasamu la chati kana kwamba alikuwa anampa mtu fulani ishara. Lisa akageuza shingo yake haraka kutazama upande ule wa dirisha, hilo likawa kosa kubwa. Tunu alimvaa Lisa na kumkumba. Wakapigwa mwereka sakafuni huku bastola zikimtoka Lisa na kuangukia kando.

Lisa akainuka haraka kuifuata bastola yake lakini kabla hajaifikia Tunu akajitupa tena na kuunyoosha mguu wake kuipiga teke, ikasogea mbali, halafu akaunyanyua ule mguu kutaka kumtandika teke la kifuani lakini Lisa akawa mwepesi na kulikwepa, kisha akajirusha kwa mgongo kumfuata Tunu.

Alipokuwa hewani Tunu alitupa ngumi lakini Lisa akaiona na kuikwepa, ya pili akaidaka na kuuviringisha mkono wake huku akijizungusha na kutupa kiwiko lakini Tunu akakikwepa na kumdaka shingo yake, akamkaba kwa nguvu zake zote.

Lisa akaanza kutapatapa akitupa viwiko vyake ili kujikwamua toka kwenye ile kabali, kimoja kilimpata Tunu na kutua kwenye mbavu zake kikamwachia maumivu makali, akayavumilia na kuendelea kumkaba. Lisa akatupa tena kingine, hakikumpata, cha tatu kikampata tena na kumtia maumivu makali zaidi. Tunu akashindwa kuvumilia na kumwachia!

Bila kutarajia Lisa alirusha konde lililotua barabara kwenye shavu la kulia la Tunu. Tunu akatema damu. Lisa akainuka kuifuata bastola yake lakini Tunu hakumruhusu achukue bastola. Akawahi kumvuta. Kuona hivyo Lisa alitupa teke lakini Tunu akaudaka mguu na kumvuta kwa nguvu huku akimrukia mgongoni na kumkaba tena. Safari hii aliikandamiza mikono ya Lisa kwa magoti yake na Lisa hakuweza kufurukuta, akaanza kuishiwa nguvu.

“Sasa zamu yako kujibu maswali yangu, mlimfuata nani pale Elli’s?” Tunu alimuuliza Lisa huku kamkaba.

“Sijui,” Lisa alijibu kwa jeuri. Tunu akamtwanga ngumi kali iliyompa maumivu makali. Lisa akagugumia kwa maumivu. Akazidi kumkaba hadi alipoona anaanza kukoroma, akamwachia na kuziwahi bastola zote mbili, ile ya kwake aliyonyang’anywa aina ya Glock 19M na ile ya Lisa aina ya 45 Colt.

Akazishika vyema zote mbili, moja mkono wa kulia na nyingine mkono wa kushoto na kuzielekeza kwa Lisa ambaye alikuwa anatapatapa pale sakafuni kwa maumivu.

“Mlimfuata nani pale Elli’s?” Tunu alirudia tena swali lake. Lisa akacheka kwa dharau.

“Hayo maswali yako ya kijinga sidhani kama nipo kwenye mood ya kuyaji...” Lisa hakumaliza kujibu, akakatishwa na mvumo wa risasi mbili toka kwenye bastola ya Tunu yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Tunu alikuwa amefyatua risasi mbili za upesi upesi zikapita pembeni ya kichwa cha Lisa na kumtengenezea maumivu makali sikioni. Lisa akaonekana kuogopa sana.

“Kama hutonijibu unajua kitakachokutokea, you know me, Lisa. You know me very well,” Tunu alifoka. Sasa sura yake ilikuwa imebadilika, aliuvua ubinadamu na kuuvaa unyama, macho yake yalikuwa yanawaka kama kaa la moto.

“Hata kama nikikujibu swali lako haitasaidia kitu...” Lisa alisema huku akicheka kwa dharau.

“Mambo ya kunisaidia au kutonisaidia nayajua mwenyewe. Nijibu kabla sijakifumua kichwa chako kwa risasi! Wala usijidanganye kuwa unachelewesha muda ili wenzako wafike kutasaidia, sina muda wa kumbembelezana kwa sasa,” Tunu alisema na kupeleka tena kidole chake kwenye kilimi ili kufyatua risasi, alimaanisha alichokuwa akikizungumza.

“Usidhani kuniua mimi ndiyo umeshinda, bado una kazi ngumu sana, Tunu.”

“Kazi ngumu ndizo ninazozipenda! Sasa nijibu, mlimfuata nani?” Tunu alifoka. Kisha akaachia risasi moja iliyoparaza kichwani ikazipunyua nywele za Lisa. Lisa akatoa ukelele wa hofu, “Nasema! Nasema!”

“Sema haraka!” Tunu akamkaripia.

“Tulimfuata Sammy!” Lisa akaropoka.

“Mnamtakia nini?”

“Mzee katutuma tumteke na lile gari lake...” Lisa alianza kuropoka kwa hofu lakini akaonekana kusita huku hofu kubwa ikitanda usoni kwake. Tunu akahisi uwepo wa kitu kilichomwogofya Lisa. Hakujiuliza mara mbili, alijirusha na kujitupa chini nyuma ya sofa moja dogo na muda ule ule kichwa cha Lisa kilifumuliwa na risasi zilizotoka kwenye bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti.

Mambo yanazidi kupamba 🔥🔥🔥Taxi inazidi kuleta kizaazaa! Ili kuyajua yote endelea kufuatilia stori hii ya kusisimua...
 
Bahati nzuri au mbaya Mimi sizozani na watu wasionijua au nisiowajua. Ila hujatumia busara kunitukana, usiamini katika matusi ndugu mdau.

Any way naomba tuishie hapa.
kama huzozani usilete shobo zako
 
Taxi (100)

Tunu aliviringika na kutambaa kama nyoka akihama kutoka sofa lile dogo na kwenda kwenye sofa kubwa. Akajilaza kimya akijaribu kusikilizia lakini akahisi chuma kikielekezwa kichwani kwake, moja kwa moja akatambua kuwa ulikuwa ni mtutu wa bastola na aliyeshika bastola hiyo alikuwa hatua moja tu toka alipolala. Mwili wake ukaingiwa na baridi.

Tunu hakutikisika wala kuinua mikono yake iliyoshika bastola. Alijua wazi kuwa alikuwa amepatikana. Hakuwa na ujanja na wala hakutakiwa kufanya lolote lile kwa pupa isipokuwa kuutii kila atakachoambiwa na mtu yule.

“Weka bastola zako chini na uinuke taratibu,” sauti ya ukakamavu ya yule mtu ilimwamrisha Tunu. Taratibu akaziweka chini bastola na kusimama akiwa amenyoosha mikono yake juu.

Alihisi kama ameona mzimu, alijikuta akitazamana na mtutu wa bastola aina ya FNX 45 Tactical yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Bastola ile ilikuwa imeshikwa na mwanamume mfupi mwenye umbo lililojengeka kwa misuli kutokana na ratiba nzuri ya mazoezi. Mwanamume yule alikuwa amevaa fulana nyekundu iliyombana na kulionesha vyema umbo lake lililojengeka kwa misuli, suruali ya bluu ya jeans na miguuni alivaa raba nyeusi.

Tunu alimtazama kwa wasiwasi. Macho ya yule mwanamume yalikuwa na dalili zote za ukatili, uwendawazimu na unyama uliokubuhu.

“Uledi!” Tunu alimaka kwa mshangao. Alikuwa akimfahamu vyema Uledi Mkama tangu alipokutana naye katika ofisi ya Mr. Oduya wakati huo yeye Tunu akifanya kazi hapo. Alifahamu kuwa Uledi alikuwa mmoja wa vijana wawili waliokuwa wakitumwa kufanya kazi maalumu na za siri za Mr. Oduya, yeye na Dulla Mcomoro. Alikumbuka kuwa ni hawa wawili wakishirikiana na Spoiler waliohusika kwenye mauaji ya Jaji Lutego.

“Uledi!” Tunu aliita katika namna ya kutaka kumzubaisha lakini Uledi hakutaka maongezi yoyote na Tunu, yeye alidhamiria kuua na kupeleka kichwa kama alivyoagizwa na Mr. Oduya.

Alianza kuvuta ndimi ya bastola, Tunu akafumba macho kwani alijua kile ambacho kingetokea na hakutaka kuona. Mara ukasikika mlio mkubwa wa risasi kutoka kwenye bastola isiyo na kiwambo cha kuzuia sauti, damu zikamrukia Tunu ambaye alianguka sakafuni huku akihisi moyo wake ulikuwa umepoteza mapigo yake, kisha akatulia kama mfu akiwa hajui iwapo alikuwa amekufa au alikuwa ndotoni.

Sister! Sister!” Tunu akasikia sauti ya mwanamume ambayo haikuwa ngeni masikioni mwake, alihisi kuitambua vyema. Akajiuliza ameisikia wapi?

Sister... ni mimi dereva wako. Inuka tuondoke haraka kuna wenzao wataingia hapa dakika yoyote kuanzia sasa,” ile sauti ilisema tena kwa wasiwasi. Sasa aliikumba vyema. Ni kweli ilikuwa ni sauti ya yule dereva wa teksi aliyoikodi. Hata hivyo hakujitokeza kwa kuogopa kuwa huenda ulikuwa ni mtego.

Tunu aliinua uso wake kwa wasiwasi na kumwona yule dereva akiwa ameshika bastola akiangalia kule kwenye mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni kwa wasiwasi na kuanza kutoka haraka. Tunu hakutaka kuwa mbishi, akainuka na kuokota haraka bastola yake na mkoba wake, akautupia jicho mwili wa Uledi na kuona jinsi kichwa chake kilivyokuwa kimefumuliwa kwa risasi, hakutaka kuzubaa akatoka kuanza kumfuata nyuma yule dereva.

Walielekea nyuma ya ile nyumba na wakati huo huo ukasikika muungurumo wa gari lililokuwa linaikaribia ile nyumba na kukomea mbele ya geti kubwa la nyumba ile. Hawakusubiri, wakarukia matawi ya mti yaliyokuwa yameinamia mle ndani na kupanda haraka kisha wakajirusha na kuangukia nje ya ukuta wa ile nyumba. Yule dereva akaanza kutimua mbio kuelekea bondeni. Tunu akamfuata. Baada ya mwendo mfupi wakaanza kuambaa na ule Mto Msimbazi kabla hawajaanza tena kupandisha kama wanarudi juu lakini wakiwa mbali na eneo la ile nyumba waliyotoka.

Tunu, are you okay?” yule dereva alimuuliza Tunu wakati wakikimbia. Tunu akashtuka sana kusikia yule dereva akimwita kwa jina lake, muda huo walikuwa wanapita katika vichochoro vya nyumba za eneo lile.

I’m okay!” Tunu akamjibu yule dereva kwa ufupi huku akiwa katika tahadhari kubwa. Bastola amezishika mkononi tayari kwa lolote.

“Endelea kunifuata, gari nilikwenda kulificha sehemu huko mbele ili wasinishtukie.” yule dereva alisema huku akiendelea kukimbia.

Pamoja na kuendelea kumfuata yule dereva lakini Tunu bado alikuwa katika mawazo kumuhusu yule dereva. Alikuwa anajiuliza yule nin nani hasa? Kwa nini amemwokoa toka kwa wale watu wakati inasemekana yeye pia ni mmoja wao? Je, katumwa na nani aje amwokoe? Au yeye pia ni undercover? Tunu alijiambia kuwa alikwisha hisi tangu mwanzo kuwa yule dereva hakuwa wa kawaida kama walivyo madereva wengine, alionekana mwelewa sana wa mambo na mwepesi wa kushika maelekezo.

Waliendelea kukimbia kwa kasi, yule dereva akiwa mbele na Tunu akiwa nyuma ingawa kwa upande fulani alianza kumwogopa sana. Jasho jingi lilikuwa linamtoka kwa kukimbia. Baada ya dakika kadhaa za kukimbia wakatokea kwenye kichochoro kimoja na kuikuta ile taxi ikiwa imeegeshwa hapo. Yule dereva akageuka kumtazama Tunu kwa macho makali.

“Pole sana, huo ndiyo uzalendo kwa nchi yako,” yule dereva alisema lakini Tunu hakumjibu. Alimtazama usoni kwa makini.

Mchezo unazidi kunoga, wamejitokeza wengi na sasa kuna huyu dereva wa taxi! Kuna nini ndani ya Taxi? Endelea kufuatilia hadi mwisho...

Thisi is for you Shunie
 
Awww uzidi barikiwa Bishop
 
Bishop ww nouma hakika sikutegemea kama hii kitu inakoenda itakuwa kitu kitamu balaa,uuuuhu hata Sam nahisi na yy ni wa geti Jeusi, tunaomba tuongezee kidogo basi
 
Da

Hii story hatari na nusu!!! Had I nimesisimkaaa!!! Thanks Bishop
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom