Stori ya Aida Olomi: Dada aliyepigwa risasi maandamano ya CHADEMA

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,243
103,925
FB_IMG_1519707579637.jpg


Aida Olomi akibebwa kama mzoga na askari wa jeshi la Polisi, February 16, baada ya kupigwa risasi mguuni (jeraha la risasi limezungushiwa alama). Polisi walimuokota akiwa hawezi kutembea na kumuongezea kipigo cha marungu kabla ya kumbeba na kumtupa kwenye gari. Aida na wenzie walipelekwa mahabusu kituo cha polisi Oysterbay, ambapo inadaiwa hajapatiwa matibabu yoyote na kidonda chake kimeanza kuoza. Taarifa zinaeleza kuwa Aida amegoma kula tangu jana ili kushinikiza haki yake ya matibabu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni ACP Muliro Jumanne amekiri kuwa ni kweli jeshi hilo linawashikilia watu watatu wenye majeraha ya risasi, akiwemo Aida lakini wameshapatiwa matibabu. Hata hivyo Muliro hakutaja hospitali zilizowapa matibabu watu hao, zaidi ya kusema ni hospitali za serikali.

KeshoAida na wenzake watatimiza siku 10 mahabusu tangu wakamatwe, bila kupandishwa kizimbani. Polisi wamekataa kuwapeleka mahakamani kwa maelezo kwamba upelelezi haujakamilika, jambo ambalo ni kinyume na sheria. Polisi pia wamezuia haki ya mahabusu hao kutembelewa na ndugu na jamaa zao.!

Updates
Mkt wa BAWACHA Segerea bi. Agnesta Lambert anashikiliwa na Jeshi la Polisi Oysterbay na amenyimwa dhamana. Kosa analotuhumiwa ni kupiga picha.

Kiongozi huyo alikwenda kwa lengo la kumtembelea bi. Aida majeruhi wa risasi ambaye yuko mikononi mwa polisi siku ya 11 sasa.

------
Hongera Jeshi la Polisi kwa kusimamia maadili.
[HASHTAG]#Justice4Aida[/HASHTAG]
 
Hata kwenye msahafu imeandikwa" Kila mmoja atabeba mzigo wake"

Watu wa maeneo ya Pwani walituambia, Wajinga ndio waliwao"

Waingereza walivyo na kauli chafu wakamalizia kwa kusema, "you reap what you sow".

Mtu yeyote anayetenda jambo bila planning nzuri lazima matokeo yake huwa mabaya. Kina Mbowe walioanzisha maandamano waliandaa njia za kujinasua kama hali ingekuwa mbaya lakini wale walifuata mkumbo bila kupanga ndio wamejikuta kwenye kadhia hii ya kipigo cha polisi.

Watu wenye fikra pana hutafuta chanzo badala ya matokeo. Huyo dada kama angejiuliza chanzo cha maandamano katika maisha yake nadhani asingepata matokeo haya ya kuandamana.
 
Kwamba huyu dada ni mjinga?heri yenu nyinyi mlio ktk mikono salama ya mungu wenu,
Wewe uko nyuma ya komputa/simu halafu unaendelea kumjaza ujinga huo msichana?

Labda kama wewe ndiye huyo msichana lakini vinginevyo haina tofauti na kumtoa kafara halafu baadaye unaanza kumpamba kuwa ni shujaa!

Kumbuka aliyeongoza maandamano yuko kwake na familia yake akiendelea kula maisha kama kawaida wakati huyo msichana ana sijui siku kumi hakuna hata msaada kutoka CHADEMA achilia mbali aliyeanzisha maandamano.

Ama kweli wajinga ndio waliwao!
 
[HASHTAG]#justice4AIda[/HASHTAG]
[HASHTAG]#justice4Aida[/HASHTAG]
[HASHTAG]#justice4Aida[/HASHTAG]
[HASHTAG]#justice4Aida[/HASHTAG]
[HASHTAG]#justice4Aida[/HASHTAG]
 
Hata kwenye msahafu imeandikwa" Kila mmoja atabeba mzigo wake"

Watu wa maeneo ya Pwani walituambia, Wajinga ndio waliwao"

Waingereza walivyo na kauli chafu wakamalizia kwa kusema, "you reap what you sow".
Kwahiyo Akwilina alivuna alichopanda, shukuru uko Tanzania.
 
Back
Top Bottom