Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,253
- 34,203
Gesi imefikia wapi mkuu?Serikali imekabidhi rasmi mkandarasi eneo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa bwawa la kuzalisha umeme ‘’Stiegler’s Gorge’’. Hii inatoa njia kwa mkandarasi kuanza kazi rasmi ambayo itaongeza zaidi ya Megawatts za 2,100 za umeme kwenye gridi ya kitaifa.
Serikali imetenga Shilingi bilioni 700 kutoka vyanzo vya mapato ya ndani katika mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Eneo la ujenzi wa maradi huo lilikabidhiwa rasmi kwa mkandarasi, Arab Contractors Company ambayo itafanya kazi kwa kushirikiana na kampuni ya EI Swedy na kukamilisha mradi huo mwaka 2022. Bwawa hilo litakuwa kubwa zaidi Afrika, na la kwanza katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambalo litakuwa na uwezo wa kutunza maji yenye ujazo wa lita bilioni 3.3, pia litasaidia katika kukuza kilimo cha umwagiliaji.
Mradi huo utakapokamilika utaondoa tatizo la uhaba wa nishati ya umeme nchini
Sent using Jamii Forums mobile app