CCM wana wakati mgumu sana kujibu hotuba ya Rostam. Wassira anafikiri Watz wa 1990 ndo wa 2011. Anakosea sana. Huko nyuma walitumia uelewa mdogo wa wananchi kama mtaji wa kushinda na hata kutumia mabavu bila kujali demokrasia. Inasikitisha sana maana Wassira anasema ameenda Igunga kujibu hoja za chama siyo za Rostam. Huku ni kuchanganyikiwa. Ila pia siyo tatizo lake maana nao uzee tatizo na sijui kama Rais aliliona hilo au anagawa tu uwaziri. Vijana wako wengi na wenye mawazo mapya na ya kujenga. Shida ya CCM ukishakuwa na nafasi mpaka ufie hapo sasa sijui kama hiyo nayo ni sera ya chama au la.
Mungu huwa hamfichi mnafiki atawaumbua mmoja mmoja. Tunawaomba sana wananchi wa Igunga waamue kwa utashi wao na si vinginevyo kwani maendeleo si kwa ajili ya chama,mbunge au kada yeyote bali kwa ajili yao wenyewe.
Kuna wengine wanasema Mwl ataweza nini kuongoza hana elimu. Sijui kama watu wa CCM walimsikia "Rais wao" alipokuwa anateua mawaziri mwaka 2005. Kikwete alisema hivi "Uwaziri hausomewi ". Lakini Katiba yetu Ibara ya inasema hivi
67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa. Kwa hiyo kwa wagombea wote waliopendekezwa na vyama vyao wanazo sifa hizi (a) na (b). Kinachohitaji hapa ni UTASHI, UTHUBUTU na UADILIFU katika utendaji.
Wana-Igunga Mungu awatie nguvu, awape ufahamu, busara na hekima katika kufanya maamuzi sahihi
Naomba kuwasilisha