Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Wasira ameyasema hayo leo Juni 22,2025 alipokuwa akizungumza katika kikao cha ndani na viongozi na wanachama wa Chama hicho Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza , ambapo amesisitiza utawala bora kwa kutii katiba na sheria za nchi badala ya kuvunja sheria kwa kisingizio cha uhuru wa demokrasia.
Wakati akieleza hayo Wasira alionesha kukishangaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)ambacho kimekuwa na kauli mbiu yake ya 'No Reform No Election' yenye lengo la kuvuruga uchaguzi mkuu mwaka huu na kuhoji kama hawataki kupiga kura kwanini walijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Wasira alifafanua kwamba kwa akili ya kawaida unaweza kujiuliza Katiba ipo inasema kila baada ya miaka mitano unafanyika Uchaguzi Mkuu halafu anatokea mtu anasema hakuna uchaguzi.
“Anasema hivyo kwa kutumia Katiba ipi? Katiba inaeleza wazi huwezi kughairisha uchaguzi alafu wewe unasema lazima usiwepo,kutaka kuzuia uchaguzi ni kinyume na Katiba na ni kutaka kuanzisha fujo…
“Je huo ndio utawala bora? Katiba inasema kila baada ya miaka mitano tunafanya uchaguzi wewe unasema hautafanyika…utawala bora ni kutii katiba na sheria na sio kutaka kukamilisha mambo binafsi kwa kukiuka sheria za nchi.”
Pia alisema kaulimbiu ya ‘No Reform No Election' inaenda kufa muda si mrefu kwasababu tayari imezidiwa nguvu na Oktoba Tunatiki, na ushahidi wa hilo Watanzania wako tayari kwenda kupiga kura kwani wamejiandikisha.