PreGE2025 Wasira: CCM inasimamia amani, iko tayari kukosolewa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,354
Reaction score
18,627
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira, amesema chama hicho kinasimamia amani na kiko tayari kukosolewa ikiwa upizani watasema wanavunja kanuni ya utawala bora.

1750096651251.png
Licha ya kauli hiyo pia amehadharisha kwamba yoyote atakayewakosoa ajipange kwakuwa watamhoji kwamba wamevunja kanuni ipi na kwa mujibu wa sheria gani, huku akisisitiza wakosoaji kutojaribu kutumia njia haramu na kuvunja haki ya wengine.

Wasira ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanachama wa CCM wilayani Mbongwe, mkoani Geita, ambako amesema nchi inaendeshwa kwa sheria na katiba na ni muhimu kutii utawala wa kisheria na watu kuacha kusikiliza wale wanaotoa matamshi ya kichochezi.

"Hatuwezi kuona mtu yoyote akivunja amani ya nchi alafu tukakaa kimya kwasababu gharama yake ni kubwa, na hatutakuwa tayari kuona hilo linatokea kwa maslahi binafsi," amesema.

"Umoja lazima ubaki kama nguzo kuu ya maendeleo ya Tanzania, sote ni kazi yetu kuhakikisha kwamba nchi yetu inadumisha utulivu," amesema Wasira

Chanzo: Nipashe Digital
 
Political party kazi yao ndo hiyo kulinda Amani ya nchi.

Hapa tutasubiri Sana.
 
Kama mko tayari acheni kuteka na kuua watu na muache kubambikia watu kesi
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira, amesema chama hicho kinasimamia amani na kiko tayari kukosolewa ikiwa upizani watasema wanavunja kanuni ya utawala bora.

Licha ya kauli hiyo pia amehadharisha kwamba yoyote atakayewakosoa ajipange kwakuwa watamhoji kwamba wamevunja kanuni ipi na kwa mujibu wa sheria gani, huku akisisitiza wakosoaji kutojaribu kutumia njia haramu na kuvunja haki ya wengine.

Wasira ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanachama wa CCM wilayani Mbongwe, mkoani Geita, ambako amesema nchi inaendeshwa kwa sheria na katiba na ni muhimu kutii utawala wa kisheria na watu kuacha kusikiliza wale wanaotoa matamshi ya kichochezi.

"Hatuwezi kuona mtu yoyote akivunja amani ya nchi alafu tukakaa kimya kwasababu gharama yake ni kubwa, na hatutakuwa tayari kuona hilo linatokea kwa maslahi binafsi," amesema.

"Umoja lazima ubaki kama nguzo kuu ya maendeleo ya Tanzania, sote ni kazi yetu kuhakikisha kwamba nchi yetu inadumisha utulivu," amesema Wasira

Chanzo: Nipashe Digital
Mwambie huyo mzee kwavile yeye ameshiba aache kuhubiri mambo ya kihuni.
 
Nani alimuua mzee KIBAO??
 
Back
Top Bottom