Baba Swalehe
JF-Expert Member
- Jun 6, 2017
- 19,527
- 37,943
Mungu yupo na dini ya kweli ni matendo memaSwali zuri. Suala la watu kujitenga au kuhitilafiana ni kutokana na ujinga,mataminio ya nafsi na ujuaji.
Kila jambo lina chanzo,na ukisoma vizuri utakuta ya kuwa asili ya Mola wetu kuchagua miongoni mwa waja wake kuwa mitume au manabii ni baada ya waja kuanza kufanya shirki/ushirikina.
Binadamu tumeumbwa na utashi,uhuru wa kutenda na kuchagua na tukapewa nyenzo za kuupokea ukweli. Huu uhuru tuliopewa ndio tunautumia vibaya. Leo hii hakuna mtu anae lazimishwa kufanya uovu zaidi ya hiari yake mwenyewe,na kuna wakati mwanadamu anaweza kufanya jambk huku akijua kabisa jambo hili lina madhara lakini akafanya,hapa nani wa kumlaumu ? Kuuliza swali kwanini kuna madhara ni uvivu wa kufikiri na kujiuliza kwanini unafanya jambo ovu au lenye madhara ni matumizi mazuri sana ya akili.
Mitume wote walikuwa na imani moja,walikuja kutangaza wito kwa waja wote wamuabudu Mola mmoja na wampige vita mshirikina na wajitenge na taghuut. Hii ndio kauli ya mitume wote,hapa utaona ya imani ni moja,ila mitume walitofautiana sheria kutokana na mahitaji. Ndio maana sheria ya Mussa si ya Issa ,ya Issa si ya Daudi si ya Suleymaan na si ya Muhamman amani ya Allah iwe juu yao.
Nakomea hapa kufupisha maelezo,kama utakuwa na swaki kwa haya nikiyo kueleza utauliza.
kk
Ila bado hatujaweza kuthibitisha uwepo wake , hilo usibishe dada !