Stella Manyanya amkaba koo Dr Slaa

Stella Manyanya atema cheche Bungeni akimtuhumu Dr Slaa kwa kuwafundisha wananchi wasifanye kazi wakati yeye amewahamasisha wananchi wa kijiji chake (hakukitaja) wajitolee kufanya kazi za maendeleo, anasema ameudhiwa sana na kauli ya Dr Slaa kuwaambia wananchi wakisikia harufu ya chakula kizuri basi kinakuwa kimepikwa kwa mbunge.

Pia amemuonya anayeitwa Mchumba wa Dr Slaa kwa kumuandikia SMS za kumtukana, anasema eti alifuatilia hizo SMS akakuta zimetoka kwa Josephine Emmanuel.


Najiuliza hivi wabunge wa CCM hawana mambo ya kuchangia zaidi yakuingiza personalities?

Sera ya Magwanda (CDM) ni kuwapa wananchi vitu vya bure, sasa siwezi kushangazwa na Slaa kusema hivyo kwani huyu jamaaa hapendi watu wafanye kazi anapenda awape watu vitu vya bure bure
 
Stella Manyanya atema cheche Bungeni akimtuhumu Dr Slaa kwa kuwafundisha wananchi wasifanye kazi wakati yeye amewahamasisha wananchi wa kijiji chake (hakukitaja) wajitolee kufanya kazi za maendeleo, anasema ameudhiwa sana na kauli ya Dr Slaa kuwaambia wananchi wakisikia harufu ya chakula kizuri basi kinakuwa kimepikwa kwa mbunge. Pia amemuonya anayeitwa Mchumba wa Dr Slaa kwa kumuandikia SMS za kumtukana, anasema eti alifuatilia hizo SMS akakuta zimetoka kwa Josephine Emmanuel.Najiuliza hivi wabunge wa CCM hawana mambo ya kuchangia zaidi yakuingiza personalities?
Hata mimi nimemshangaa, badala ya kupeleka ishu polisi analeta bungeni! ni kupoteza muda wa bunge kwa mambo personal na hata hivyo hana uhakika kama josephine emmanuel ndiye huyo 'mke' wa dr. slaa, amejudge kwa kufananisha jina.
 
Huyu Injinia Manyanya nilikuwa namheshimu sana lakini kwa kauli hii ya bungeni nimemfuta katiika orodha ya watu ninaowaheshimu. Inaelekea naye ana matatizo ya kiakili kama ilivyo kwa magamba wengi ndani ya Bunge.
 
Nimewahi kusoma humu juu ya wanaharakati waliofungua shauri mahakamani kupinga hii mifuko ya maendeleo ya jimbo, mifuko ambayo wengine tuliipinga sana pamoja na kuwa viongozi wa CDM waliiunga mkono.

Napendekeza wanaharakati hawa wafungue shauri jingine kupinga sheria ya haki na kinga kwa wabunge, sheria inayowapa kinga ya kutoshitakiwa wabunge kwa yale wayafanyayo wanapokuwa bungeni. Pengine kinga hii ikiondolewa itawafanya wabunge kuwa makini na yale wanayoongea bungeni kwa hofu ya kuburuzwa mahakamani. Otherwise, tutaendelea kushuhudia tabia za kilevi kama alivyoonyesha Manyanya leo.
 
hapana swahiba.... the approach she used was right kwani hakutaka yawe haya, ila kale ka manyanya kameyaleta kenyewe Ustaarab aliotumia josephine ndio mzuri hakutaka kulumbanaau unaonaje?? ulitaka aianzishe jf?
Nadhani Josephine angeyaeleza haya(aliyomtumia sms) jukwaani ingekuwa bora zaidi badala ya kumtumia sms,unless kulikuwa na lingine zaidi.......................Fikiria MTM ni politishani na Bala naye ni politishani wa mlengo halafu Bala anamtumia sms MTM yenye maneno '....................,jirekebishe bana,unaidhalilisha fani yako'...........MTM(japo binadamu tunatofautiana) aanaweza kuipokea sms hii kicinge aisee,akadhani Bala anamfuatafuata ama ana ajenda ya siri
 
Stella got it wrong on Slaa kuhamasisha wananchi wasifanye kazi, sijawahi sikia huu upuuzi, lakini suala la sms naomba tusianze kurusha mawe, slaa is a member of JF, so he can as well clarify kuhusu sms kutoka kwa josephine...
Hata Josephine ni memba humu, anaweza kujisemea.
 
Kwa nini usingemsema kwa kupitia jukwaa?...Nadhani ujumbe ungemfikia kwa urahisi zaidi......Btw......Kuna watu wameshaanza kutafsiri mengine hapa kwamba huenda kuna 'conflict of interest' kati yako na mhe. mbunge ndiyo maana wewe ukamtumia ujumbe.....

Jukwaa gani tena wakati unajua josephine si mwanasiasa wa majukwaani? afterall njia aliyoitumia kumfikishia ujumbe ni muafaka kabisa, mwenye matatizo ni manyanya alkiyeamua kulipuka, tena bungeni ambapo anajua kwamba josephine hayupo na hawezi kumjibu.

Punguza speculation mkuu, "conflict of interest" ipi tena wakati josephine alikuwa amefika kijijini kwao na kukuta hali ngumu ya maisha ya wanakijiji ndo akaona bora amkumbushe manyanya kuwawakilisha vizuri wanakijiji wenzake badala ya kuwa vuvuzela!!??
 
huyu manyanya ni mbunge wa kuteuliwa au kuchaguliwa....naomba tufanye kama jana kwa yule mbunge wa kilindi....hakuna mwenye picha za jimbo la huyu mama?
 
josephine amejibu vizuri sana...usijibu kitu mama ....yule manyanya hana lolote.....
 
Manyanya si mstaarabu na Josephine nae si mstaarabu vile vile.

Utamuandikiaje msg mtu na kutumia maneno Kama 'acha ushabiki na unafiki' ?
 
Manyanya si mstaarabu na Josephine nae si mstaarabu vile vile.

Utamuandikiaje msg mtu na kutumia maneno Kama 'acha ushabiki na unafiki' ?

ni jambo la kwaida kabisa katika kusema ukweli kuwa huo ni unafiki maana hawakilishi ipasavyo wananchi wake.......hata mimi nilishawahi andika kwa jk tena nafuu ya hii josephine ..labda atanijibu kupitia hotuba ya mwisho wa mwezi ..
 
Wabunge wanataka waendelee kupewa sitting allowances kwa kuchangia na kushangilia hoja mfu kama hii ya sms.

Kama hii ni kweli au sikweli inatusaidia nini sisi wananchi wa Tanzania. Hii ni personal issue na kama vipi nenda polisi.
 
duh hiyo ya sms ni kali ya wik, mama spika alisemaje alipoona ishu ambazo ni personal tena kwa mtu ambaye sio mbunge kuzumziwa bungeni! plz nipeni updates plz
 
Wabunge wote wa CCM karibu ni mavuvuzela hivyo sio ajabu hapa kuona wanasema mambo yasiyo ya msingi katika Taifa
 
ni jambo la kwaida kabisa katika kusema ukweli kuwa huo ni unafiki maana hawakilishi ipasavyo wananchi wake.......hata mimi nilishawahi andika kwa jk tena nafuu ya hii josephine ..labda atanijibu kupitia hotuba ya mwisho wa mwezi ..

Haijalishi wala haihalalishi Kama wewe si mstaarabu kuwa na mwengine awe si mstaarabu pia.

Kama alikuwa na nia njema angechagua maneno mazuri ya kumwambia, besides Manyanya ni mbunge Wa viti maalum na ni msaidizi tu wa jimbo
 
Back
Top Bottom