Vitu viwili kuhusu hii profile ya Stella Manyanya
Kwanza:EMPLOYMENT HISTORY: TANESCO Head of Department 1992 To Date - Stella Manyanya amekuwa mbunge huu ni mwaka wa 6 sasa. Inawezekana bado jina lake liko kwenye payroll system ya TANESCO maana bado anasema anafanya kazi huko? Kanuni za bunge zinaruhusu kuwa mbunge huku bado unaendelea na utumishi kwenye shirika la umma? Kama hafanyi kazi TANESCO kwa nini aandike bado yuko huko 6 years after she joined the Parliament? Kama Stella Manyanya anashindwa hata kutoa taarifa sahihi kuhusu mwajiri wake anawezeje kuwa sahihi kwenye jambo lolote analoongea Bungeni?
La pili: Facial hair - Mwanamke kuwa na facial hair ni 'uchafu' - UNHYGIENIC! Na kama kuna mtu hapa Jamvini mke wake anafuga ndevu au hanyoi nywele miguuni anatakiwa ajue hivyo - UCHAFU. Nimewahi kuona wasichana na wamama wangi wanatembea bila wasiwasi huku miguu imejaa minywele na wengine ndevu kama wanaume! I hope Stella Manyanya wakati anazunguka dunia kuchunguza Richmond alinyoa hizo ndevu maana atakuwa ametoa taswira mbaya kuhusu wanawake wa Tanzania na personal hygiene.
Stella Manyanya bado anahesabika ni mtumishi wa TANESCO ingawa ni mbunge,yuko kwenye likizo ya bila malipo......
Si yeye tu,ni wabunge wengi ambao wako kwenye likizo ya namna hii,wakishapata ubunge wanaruhusiwa ama kuacha kazi ama kuomba likizo ya bila malipo mpaka watakapoacha ubunge wao....
Baada ya kuacha ubunge wanayo hiari ya kuendelea na ajira zao ama kuendelea na ustaarabu mwingine wa kuwa wastaafu....
Angalia waraka huu namba 1 wa mwaka 2000,pia kuna marekebisho ambayo yamefanywa katika waraka namba 2 na namba 3 kama sikosei...
Waraka Namba 1 wa Mwaka 2000
KUHUSU WAGOMBEA UDIWANI, WAGOMBEA UBUNGE WA VITI MAALUM, UBUNGE WA KUTEULIWA NA RAIS KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA WAGOMBEA UBUNGE KATIKA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
1.0 Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na.1 wa Mwaka 2000 uliwekwa Masharti yanayowaongoza Watumishi wa Umma kushiriki katika shughuli za Kisiasa nchini.
2.0 Baada ya Masharti hayo kutumika kwa muda wa takriban mwaka mmoja na nusu, Serikali imeamua kufanya marekebisho katika Waraka huo kwa lengo la kuboresha Masharti hayo kwa Watumishi wa Umma watakaoamua kugombea au watakaoteuliwa katika nafasi zilizotajwa hapo juu kama ifuatavyo:
2.1 Watumishi wa Umma wanaoamua kugombea Udiwani
Watumishi wa Umma watakaoamua kugombea Udiwani wanaruhusiwa kufanya hivyo na endapo watabahatika kushinda wataendelea na ajira zao kwani Udiwani sio ajira.
Hata hivyo Watumishi wa Umma ambao ni waajiriwa katika Halmashauri (Council) hawaruhusiwi kugombea Udiwani katika Halmashauri wanazofanya kazi.
2.2 Watumishi wa Umma Wanaoamua Kugombea Ubunge Kupitia Viti Maalum
Watumishi wa Umma watakaoamua kugombea Ubunge kupitia Viti Maalulm wanaruhusiwa kufanya hivyo na endapo watashindwa wana hiari ya ama kuacha kazi na kulipwa mafao yao au kuchukua likizo bila malipo kwa kipindi chote cha uhai wa Bunge tangu Tume ya Uchaguzi itakapowatangaza kuwa Wabunge.
2.3 Watumishi wa Umma Wanaoteuliwa na Rais wa Kuwa Wabunge kwa Mujibu wa Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 (Toleo la Mwaka 2000)
Watumishi wa Umma watakaoteuliwa na Rais kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (Toleo la Mwaka 2000) wana hiari ya ama kuacha kazi na kulipwa mafao yao au kuchukua likizo bila malipo kwa kipindi chote cha uhai wa Bunge kuanzia siku watakayoteuliwa.
2.4 Watumishi wa Umma Watakaogombea Ubunge Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki
Watumishi wa Umma watakaochaguliwa kuwa Wabunge katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaweza kuendelea na kazi katika Utumishi wa Umma au kuchukua likizo bila malipo. Aidha, wakati wa kuhudhuria Vikao vya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watalazimika kutoa taarifa kwa Waajiri wao na watapewa ruhusa maalumu ya kuhudhuria Vikao hiyvo.
3.0 MWISHO
Masharti mengine yanabaki kama yalivyo. Aidha, marekebisho haya yatatumika kuanzia tarehe ya Waraka huu; Isipokuwa kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Afrika Mashariki marekebisho haya yatatumika kuanzia tarehe 15 Juni, 2001.