Stella Manyanya amkaba koo Dr Slaa

kweli nimeamin CCM inachakachua AKILI za watu, sms ni personal isue, bungeni imefikaje? Ni stella huyu nnaemjua mimi au? Kweli ccm inakufa vibya..
 
Kama nimekuelewa vizuri unataka Dr. Slaa amsemee mchumba wake?? assuming ni kweli Josephine alituma hizo sms, je ni lazima Dr. Slaa atakuwa aliziona ama unataka kusema ndiye alimtuma??

Hebu kuwa serious kidogo mkuu.
Nope, i am just wishing slaa to be a man enough to ask his wife and clarify the matter... if he leaves this to josephine yanaweza kuishia kwenye mipasho ya wanawake

that is the stand i would take being a leader and the head of family...
 
Nope, i am just wishing slaa to be a man enough to ask his wife and clarify the matter... if he leaves this to josephine yanaweza kuishia kwenye mipasho ya wanawake

that is the stand i would take being a leader and the head of family...

Hebu suppose kuwa Josephine amemuandikia kweli Stella hizo SMS, Dr.Slaa akamuuliza na akajibiwa kuwa kweli amemuandikia unategemea kuwa Slaa atakuja hapa akiri hilo?
 
Slaa anatisha..mpaka Eng. Stella Manyanya yupo kwenye anga zake???. Mh..ina maana Josephine katuma msg ya matusi bure bure tuu! Au ndo Eng. anamzengea DR..? Mwisho wake stella ameamua kutoka kivingine bungeni baada ya kutoswaa??. Politics bwana..acha tu..inabidi uwe chuma kweli kweli.
 
Hivi siyo yule mama aliyeko katika ile 'list of shame 'ya Dr,labda kaamua falsafa ya jino kwa jino
 
Stella Manyanya atema cheche Bungeni akimtuhumu Dr Slaa kwa kuwafundisha wananchi wasifanye kazi wakati yeye amewahamasisha wananchi wa kijiji chake (hakukitaja) wajitolee kufanya kazi za maendeleo anasema ameudhiwa sana na kauli ya Dr Slaa kuwaambia wananchi wakisikia halufu ya chakula kizuri basi kinakuwa kimepikwa kwa mbunge,pia amemuonya anayeitwa Mchumba wa Dr Slaa kwa kumuandikia SMS za kumtukana,anasema eti alifuatilia hizo SMS akakuta zimetoka kwa Josephine Emmanuel
Najiuliza hivi wabunge wa CCM hawana mambo ya kuchangia zaidi yakuingiza personalities

Hakuna mwongozo ulioombwa kuhusu kutaja majina?? au ndo yale yale ya mwenyekiti kwenda kwa ubinafsi
 
Sio bure Stella Manyanya na Josephine kuna kitu!! Ilikuaje mpaka wakawa wanatukanana kwenye sms? Sisi wote ni watu wazima tafakari

Ni kweli Stella alikuwa anammendea Dr wa ukweli, Josephine alpogundua akaamua kumtolea uvivu, stella nae hasira za kutukanwa na josephine anaenda kuzitolea bungeni, badala ya kujadili budget anajadili isue zake binafsi...
 
Sio bure Stella Manyanya na Josephine kuna kitu!! Ilikuaje mpaka wakawa wanatukanana kwenye sms? Sisi wote ni watu wazima tafakari

Ha ha ha inawezekana kuna zaidi ya siasa nimecheka kweli
 
Hebu suppose kuwa Josephine amemuandikia kweli Stella hizo SMS, Dr.Slaa akamuuliza na akajibiwa kuwa kweli amemuandikia unategemea kuwa Slaa atakuja hapa akiri hilo?
simpo sana mwalimu

talk to wife or ignore injinia nyanya
 
bunge la mwaka huu, hivi wanajadili bajeti au sms kutoka kwa josephine, nachoka mwenzenu sijui yatakwisha lini haya.
Hoja mezani ni hotuba ya Waziri Mkuu. Sasa Josephine aningia vipi hapo? Wabunge wengine bwana? Huyu Mama amefilisika baada ya hoja yao ya kudandia ya ufisadi kukosa mshiko.
 
Stella got it wrong on Slaa kuhamasisha wananchi wasifanye kazi, sijawahi sikia huu upuuzi, lakini suala la sms naomba tusianze kurusha mawe, slaa is a member of JF, so he can as well clarify kuhusu sms kutoka kwa josephine...

Kweli upumbavu hauna ujazo kuwaambia watu waandamane na kuacha shughuli zao ni sawa na kuwahamasisha wasifanye kazi.
 
Ni kweli Stella alikuwa anammendea Dr wa ukweli, Josephine alpogundua akaamua kumtolea uvivu, stella nae hasira za kutukanwa na josephine anaenda kuzitolea bungeni, badala ya kujadili budget anajadili isue zake binafsi...

This is what i heard hata mimi....
 
Swali kwa Ir Manyanya. Una mme?
Swali tena kwa Ir Manyanya unamtamani Dr Slaa?
Nimeamini, ccm inachakachua akili za wasomi. Hata hivyo sishangai Tanesco kuwa kama ilivyo kama kweli wewe dada ulikuwa engineer pale! Ninaanza kuwa na shaka na elimu yako!
 
Kweli upumbavu hauna ujazo kuwaambia watu waandamane na kuacha shughuli zao ni sawa na kuwahamasisha wasifanye kazi.
yawezekana pia ujazo hauna upumbavu na uelewa usio na uelewa ukakuyumbisha kwenye kudadisi na kuchanganua....

hakuna watu waliowahi kuandama nchi hii kama wanaCCM, tatizoi ni kwamba nyani haoni kundule

at times wapumbavu kama "mimi na wewe" huwa tunashindwa kuelewa simpo theories za productivity na motivation and how we can use demonstration as a driver for productivity, including maanamano

but anyway, nisijeleta sokomoko kwa sokomoko mwenye uelewa wa ki-sokomoko na kuishia kuwa kisonono

Thanks
 
Bunge letu sasa ni la mipasho na kulipizana.
Jukwaa la kuwakilisha wananchi sasa limekuwa jukwaa la kuonyeshana nani zaidi kwa mipasho na kuchafuana.
Kweli tunahitaji new blood mjengoni kuondoa haya majungu jungu na mipasho isiyo na Tija.
 
inaonesha kuna mambo ya ziada,may be manyanya kamnyemelea mume wa mtu.hzo sms alizotumiwa huenda zina jambo,aache kumfuatilia mume wa mtu.
 
injinia wapi huyu sifa gani za kuitwa injinia? TUna ushahidi na inajulikana hata ktk masters yake pale UDSM alikamatwa na kibuti akidesa.. kama si huruma ya wakufunzi wa chuo wangemtimua.Kama aliweza kutumia kibuti kudesa basi atakuwa anaibia serikali pia. Injinia hana muda wa kuongea upuuzi kama huu anatakiwa aongee mambo ya msingi hasa ya kimendeleo, kwa upeo wa kawaida sidhani mtu kama dr slaa angeweza kuwaambia wananchi wasifanye kazi.ana lake jambo. Bunge la mwaka huu taarabu tupu.
 
simpo sana mwalimu

kama ni mimi ntasimama, ntaomba ruhusa ya kuongea na nitasema kwamba ni kweli kumekua na majibishano kati ya hao wawili and it was more personal au yanahusiana na "mambo yao" ambayo hayana tija kwangu na kwa taifa... na nimemkanya mchumba wangu aache hayo mawasiliano kwani watanzania wanahitaji maendeleo na sio malumbano ya kike

vilevile ntamshauri stella aache kujibishana (kama na yeye hujibu) na atafute muda wayajadili na kuyamaliza kikubwa kwani wote ni watu wazima na wenye heshima zao....

Mwisho nitaomba msamaha kwa wabunge kwamba mambo ya personal sms hayana tija kwa taifa na kama kila mtu angeanza kusema sms anazotumiwa na mwingine basi bunge lingegeuka "kanga moko laki si pesa"
Hivi hawa nao si binadamu kama wewe na mimi? Kwangu tatizo sio sms ila kuipeleka bungeni wakati wa kuchangia hotuba ya Waziri Mkuu. Inaathiri vipi maendeleo ya watu?
 
GreatThinkers,
Lets Go Deep, bado namchukulia huyu ni kilaza.

Je Josephine Emanuel ni mmoja tu countrywide? Kwanza majina haya yote ni ya wote, hata ukitaka leo ubatizwe kwa hayo majina inawezekana. Napata wasi wasi juu ya upeo wa huyu MBU..NGE,

Chapa rapa!
 
Wavua magamba watasema haka kamama kanatafuta umaarufu kwa mgongo wa Dr.Slaa

Stella Manyanya ni miongoni mwa wabunge vigeugeu na wasiosimamia chochote. Kwenye bunge lililopita huyu mwanamama alikuwa kwenye kamati ya Dr Mwakyembe iliyochunguza saga la Richmond. Na alisikika bungeni akilalama jinsi 'wataalam wetu' wanavyoangusha nchi. Kamati yake ilitoa mapendekezo 18 ambayo yalipitishwa na bunge. Sasa Stella Manyanya anaweza kutuambia amefikia wapi katika kusimamia mapendekezo ya kamati yake hiyo? Ni mapendekezo mangapi yametekelezwa? Amechukuwa hatua gani dhidi hao aliowaita 'wataalum watu'?

Kusema kuwa Dr Slaa anawahamasisha wananchi wasifanye kazi nadhani huyu mama anatakiwa awaombe watanzania msahama. Hivi watanzania hawana uwezo wa kufikiri mpaka waambiwe na Dr Slaa ni nini cha kufanya na nini wasifanye? Kama sio madharau ya hali ya juu kwa watanzania ni nini? Miaka 50 ya uhuru wananchi tunahoji ni kwa nini hatuna chakula cha kutosha, kwa nini hospitali zetu hazina dawa, kwa nini hatuna umeme, na kwa waliounganishiwa umeme kwa nini kila kukicha ni mgao? Kwa nini 80% ya wanafunzi wamefeli? kwa nini wabunge wanalipwa kwa kila kikao wanachohuria lakini wafanyakazi wengine hawalipwi? Kwa nini wazee wa iliyokuwa Afrika Mashariki hawajalipwa mafao yao? Wananchi tunauliza hela za EPA zimerudi? na ni nani walihusika kwenye ununuzi wa rada? Kwa kifupi Stella Manyanya sisi wananchi tunauliza maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Hii haihitaji couching toka kwa Dr Slaa.

Stella Manyanya kapata ubunge wa viti maalum, na sasa analipa fadhila kwa kufanya kazi maalum ya kunyamazisha watu na ku-intimate citizens kupitia chombo cha kutunga sheria yaani bunge. Anaweza kusema kama yeye mbunge amefanya nini? Huyu mama na record gani ki-utendaji kiasi anaweza kumkashifu Dr Slaa? She is a morally bankrupt nominated MP who stands for nothing and it is about time she gets real - Watanzania tumechoka kulishwa matapishi. 50 years mnaimba amani na ulivu wakati watu wanakula mlo mmoja tena kwa kubahatisha!
 
Back
Top Bottom