Stella Manyanya jana anadai anauchungu kuzungumza CHADEMA hawakuzingatia jinsia? Leo anajua kutetea wanawake? Mbona hatukumsikia akisimama kumtetea mwanamke Mwenyekiti wa wanawake CCM Taifa Sofia Simba, aliyefukuzwa uanachama, tena kwa kosa sawa kabisa na wenzie, manake kama ni kutoka nje kupinga maamuzi ya Kamati Kuu wakati wa kumtafuta mgombea wa urais2015, mama huyu hakuwa pekeyake, mbaya zaidi wote aliotoka nao Kimbisa kasamehewa, Nchimbi kapewa onyo kali, ila huyu mama na wabunge wengine wanawake hakuna hata mmoja hata kujitokeza hadharani kumpa pole.
Tukumbuke mama Simba alikua anaongoza wanawake viti maalum zaidi ya 100 bungeni, lakini hakuna aliyejitokeza, leo Manyanya anatuigizia kanakwamba demokrasia ya vyama vingine inamgusa ambao kimsingi hoja yake dhaifu, ni unafiki wa hali ya juu kuwai kuonekana. Yani watu kama yeye hawafai kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi. Taifa halihitaji watu hawa. Angeonekana wamaana sana japo hata kama Sofia Simba alifanya makosa ambayo hatuyajui, basi tungeona ata akijitokeza kutoa pole.