Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Habari zenu wanaJamiiForums

Je una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie. Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi.

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

Ahsanteni sana na karibuni nyote.
Mnabore kwann kwenye dish channel nyingi hamna tofauti na kwenye antenna? Pesa nyingi alafu mnazingua wekeni E tv,na Citizens angalau vingenevyo mnabagua na kutuwekea utofauti mbona pesa hamuweki kiwango sawa kwa wote?
 
Sioni sababu wala umuhimu wa huu uzi. Nadhani Startimes wameona maswali yamewazidi. Ubabaishaji at work
 
Startimes acheni ubabaishaji haiingii akilini mtu unanunua kifurushi hata wiki haijaisha mnasema mmebadili mfumo na antenna hazitumiki tena. Kama mlijua mna matatizo na mifumo yenu mngetoa taarifa wakati wa manunuzi ili mtu aamue kuacha kununua ama aendelee.

Elfu 12 ni nyingi sana TCRA waangalieni hawa watu, nipo Himo Kilimanjaro Startime Mungu anawaona
 
Kwanini Wateja wa Startime hususani maeneo ya Njiapanda-himo,Rombo,marangu na maeneo jirani mmewaondoa katika mfumo wa antena, gari zenu za matangazo zimekua zikipita kuwataka watumiaji warudi vingamuzi hivyo kwakua havitaweza fanya kazitena kwa gharama ya 75000/=

Kweli ii ni sawa? au utapeli. na wateja wengi wamegomea wameona bora kubakia na kumbukumbu na kuikataa startimes
 
nataka kujua ukilipia kifurushi cha mambo cha 6000 unatumia siku ngapi na 12000 unatumia siku ngapi maana naona unatumia siku sita tu kimeisha naomba ufafanuzi
 
Kwenye E na Leo Series 1 hamna title wala timer ya vipindi mmebaki kuandika. THE END tuuu
rekebisheni
 
Mimi kitu walichoniuzi Hawa watu matapeli ni hivi nimelipia kinga'amuzi changu kama dk 20 King'amuzi kikaandika aota data download nikawapigia wakasema kilete napeleka wananiambia akifai tena ni chakubadilisha niongeze 32000 nipatiwe kingine lakini wenywe kwa muda huwo awana mpka vije na aijulikani vinakuja lini je ile pesa niliyolipia iko wapi Mimi naona wanaprogram yani wanavizima kusudi ili waseme vibovu na wanajua uwezi kutengeneza popote ili ukanunue kingine kweli hii ni biashara ujinga mtupu Startime
 
wachina mnashindwa na wabongo...yaani mnashindwa kuweka channel za Afrika Mashariki tena kwenye dish........Azam oyeee...Startimes mmefuliaa........jipange upya..
 
Naomba kuuliza katika kifurushi cha Mambo ukilipia sh. 15,000 channel ngapi zinatakiwa zionekane?? Mbona TV imman wala Mliman TV hazipatikani wala Emmanuel Tv?

Mimi mteja wenu mwenye Acc # 02035098916
 
Back
Top Bottom