Star TV na ITV kujitoa rasmi Startimes muda si mrefu!

bampami

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2011
Posts
5,700
Reaction score
4,126
Habari nilizozipata, mda mfupi ulio pita ni kuwa mwanasheria wa continental ametuma barua ya kuitaarifu startimes kujitoa kwa startv rasmi startimes, na mda simrefu Itv nao wanatuma rasmi barua kama hiyohiyo, huk startimes mashop yote ya dar ya startimes yameambiwa yawataarifu wateja kuhusu kutoka kwa hizo channel mbili.

NTAENDELEA KUWA UPDATE.....

Source mimi mwenyewe toka maeneo ya hapa bamaga startimes, nimepata habari hizi nikiwa ndani ya duka lao mda huu..wakijadiliana watafanyaje???



 
Makubwa!!, sasa haka ka startimes kangu nikatupie jalala lipi jamani?
 
Wajitoe haraka sana, startimes kazi imewashinda. Natamani kukitupa hiki kisi-MBUZI chao.
 
Si walituambia kuwa ving'amuzi vyote vitakua vinaonyesha 5 local channels bure including itv, star tv, tbc 1,chanel 5 na channel 10?
 
Kwanini wameamua kujitoa kwenye Startimes?

Hivi ni nani huwa anamlipa mwenzie ili channel yake iwepo hewani, ni startime au TV channel?
 
Bora maana nilikuwa nampango wa kununua

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hizo habari ni uongo na uzushi wa vijiweni!

Sheria ya mawasiliano kupitia TCRA inazitamka ITV, TBC, STAR TV, CHANNEL 10 na EATV kama ni FTA yaani Free To Air channels na sio Pay TV.

Sheria inawataka wamiliki wote wa visimbuzi vyenye local license kuziweka kwenye list hizo channels bure bila walaji kulipia!

Wakuu endeleeni kuumiza macho kupitia visimbuzi vyenu!
 
ni ngumu sana,TCRA inawalazimisha watoa huduma kuonesha ITV, TBC, STAR TV, CHANNEL 10 na EATV bila malipo
 
Kwenye hiki king'amuzi cha kikulima cha Star Times kuna tangazo linapita kuwa Star TV wanataka kujitoa kwa Star Times,Sijui wanafikiria nini wakati coverage yao ni ndogo sana hasa kwa kupitia king'amuzi chao cha CONTINENTAL.
Nafikiri hawajajifunza kwa CLOUDS TV ambao walijifanya wanakimbia Star Times wakati hata watazamaji hawana,
Nafikiri wakae chini waangalie suala hili vizuri kabla ya kukurupuka.
 
Kila jambo hufanywa kufuatana na maslahi hivyo basi kama Star Tv wameona kwamba kwao ni hasara wana haki ya kujitoa
 
Siku hizi haina haja ya kuwa na Tv tena kwa maana masharti ni mengi
 
Reactions: mja
Nimeliona hilo tangazo...ntatafuta king'amuzi kingine...startimes wanazingua na channl zisizo na viwango
 
nami ndo naona,itakuja kufuatia itv nao kujiondoa
 

Tangazo linapita saiv kwenye tv, Star tv wanajitoa
 


Mkuu wewe ndio unaleta habari za vijiweni. Tayari tangazo la kujitoa kwa STAR TV linapita kwenye screen, wakisema

Ndugu mteja kutokana na matakwa ya STAR TV inatulazimu kuitoa katika orodha ya chaneli zetu. kwa maelezo zaidi piga STAR TV 0202503262. Samahani kwa usumbufu utakao jitokeza.

Jambo hili limekuja kipindi kizuri wakati watunga sheria wetu wakiwa kazini. Tuone basi kama hii ishu iaibuliwa bungeni.
 
Sasa tunaondoa maana halisi ya Digital coz inatakiwa mtu akiwa kwenye king'amuzi chochote apate Chanel zote muhimu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…