Kumbe Vin'gamuzi vya Startimes ni kimeo? teknolojia yake kuisha tarehe 31 Desemba! China vilikataliwa, Uganda vikakataliwa, vimeletwa Tanzania nchi inayoongozwa na wababishaji!
Mkuu niliwahi kuonya kuhusu hili, jana nilimjibu Mkuu Meningitis lakini kwa bahati mbaya nilipoteza thread, nataka kuirudia tena hapa kam ifuatavyo:
Naona usanii unaendelea kulitafuna taifa!kwa waelewa wa mambo tumeshanusa harufu chafu ya ufisadi ndani ya TCRA.nisiseme mengi bali nijikite kwenye swali langu au letu!
Ili niweze kuona local channels zote ninunue king'amuzi kipi?
This is a very serious question from the common mwananchi.
Mkuu Meningitis, kama unavyo sema kuna kitu kinaendela behid the scene si bure! Kwanza kwa nini TCRA waliamua kusitisha matangazo kwa njia ya analouge wakati wakijuwa fika kwamba ITV/STARTV hawana vingamuzi sokoni – mimi nilifikili wahusika wote wanashirikishwa kikamilifu mpaka dakika ya mwisho, kwa nini StarTimes ndio ilionekana kujuwa kinacho endelea zaidi kuliko kampuni mengine? TCRA walifanya maksudi kujaribu kuipiga tafu StarTimes - sio bahati mbaya hata kidogo.
La Pili nilisha sema kwamba TCRA walikurupuka mno ku-roll out mfumo wa digitali, walikuwa hawakufanya home work ya kutosha - inawezekana kivipi kukubalia ma-multiplexors wasambaze mawimbi wakati wakijuwa wazi wazi kwamba kuna baadhi ya maeneo yanayohitaji gap fillers! Swala hilo wangelivaria njuga kwa kuhakikisha constraint hiyo inakuwa addressed kikamilifu - na hiyo si kazi rahisi kwa kuwa Minara ya kurushia matangazo haiko sehemu moja - nyingine ziko Kisarawe na nyingine Makongo kwa hiyo gap haziko confined sehemu zinazo fanana!!!!
La Tatu TCRA ina wajibu wa kuwalazimisha bila woga ma-Multiplex Providers wote ku-multiplex local channels zote na ziwe free, kwa wale ambao watahitaji channels za ziada/starehe basi hao walipie, tatizo hapa inaonekana TCRA ina dalili za woga woga kwa wafanya biashara hizi za TV, mimi huwa nashangaa nisikiaopo TCRA wanawakaribisha wafanya biashara hawa eti wawape ushauri wa jinsi ya kuendesha Shirika hili la UMMA badala ya kuwa watch dog wanafanya vitu vingine tofauti kabisa, wala tusishangae yanayo endelea sasa hivi.
La nne, hapo mwanzo jukumu la ku-multiplex matangazo yote ya Television zote nchini lilikuwa liwe la TBC pekee, kama nakumbuka vizuri TBC wali float mpaka tenda kufanikisha jukumu hilo; cha ajabu sijuhi kulitokea nini baadae tukaja fahamishwa kwamba TCRA imekubali kutoa liseni kwa makampuni mengine ma wili yatakayo fanya kazi zile zile za TBC!! Sasa nini kilitokea in between – God knows. Hivi TCRA waliwezaje ku-defy directive za Serikali au walitoa visingizio gani vya ku-justify kukubalia makampuni mengine kijihingiza katika biashara ya ku-multiplex channels za makampuni mengine? Mimi binafsi nilikuwa napendelea kuwepo Provider mmoja ili kupunguza adha hizi ambazo tume anza kuzishuhudia, tusigekuwa na ulazima wa kununua multiple vingamuzi na mambo mengine ya kijikanganya unnecessary.
Mwisho, kitakajo kuja kutokea baadae ni nini?? Ushindani wa kibihashara na malumbano yasiyo na tija - katika hilo kampuni ya StarTimes itapata wakati mgumu labda wabadilike, infact sina uhakika kama vingamzi hivyo viko
Fully compliant with DVB-T2 standard, si ajabu ndio vilikataliwa huko Uganda wakaja kuvi-dump hapa TANZANIA wakijuwa wazi wazi hatuwezi kuwafanya chochote au wanaoana Watanzania ni mbumbumbu!!!.