Stanslaus Nyongo: Hakuna wa kuinunua serikali ya Rais Samia

Stanslaus Nyongo: Hakuna wa kuinunua serikali ya Rais Samia

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo amewatoa hofu Wananchi wa Kijiji cha Fukayosi, Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo, akisisitiza kuwa hakuna Mtu aliye juu ya sheria wala anayeweza kuinunua Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Nyongo ameyasema hayo Novemba 3, 2026, alipofika Mijijini hapo kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili Wakulima na Wafungaji, hususan migogoro inayohusiana na shughuli zao. Katika ziara hiyo, amewataka Wananchi kuheshimu Sheria za Nchi na kuacha kujichukulia Sheria mkononi. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuundwa kwa mabaraza yatakayoshughulikia migogoro, kuwawajibisha wanaokiuka Sheria na kuhakikisha hatua stahiki za kisheria zinachukuliwa dhidi ya wakosaji.

Vilevile, amewataka Wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika hatua zote za uchunguzi na upelelezi ili Watuhumiwa wanaobainika kuhusika na makosa wafikishwe mahakamani na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

 
Back
Top Bottom