mkurya org.
JF-Expert Member
- Sep 25, 2014
- 1,571
- 1,697
Mkuu siku za nyuma hiki chuo kilikuwa chini ya dini ya kikristo na ndo kilikuwa kinakisimamia afu walikuwa na marecturer wazuri na walikuwa wanalipwa vizuri afu kilikuwa kinasifika sana lakini siku hizi hiyo dini imejiondoa na marecture wenyewe hawapo wamebaki wahindi wenye elimu master ya linguistic ndo wamekua wanaoongoza chuo cha engeneering kwa maana hawana sifa yoyote ya kufanya hivyo na kwenye chumba cha mtihani anaweza kukwambia andika chochote kama hujui afu atasahihisha na assignment anaweza kukwambia ukopy maswali na solution zake kutoka kwenye daftari uliyoyafanya afu tunakusanya anaenda kusahihisha ndo hivyo limetokaNdio hao hao, lakini si walitumia workshop hizo hizo mnazolalamikia, walifundishwa na wahindi hao hao mnaowalalamikia!?
Nikweli mkuu waliingia na gia ya udini lakini ukishindwa kulipa hata sh 400,huwezi kufanya UE kisa hujamaliza ada.Inasakitisha sana kwakweli.Kwahiyo wahindi waliingia na gia ya dini😱😱😱
So bad!!. Anyway mie ata nikiona CV zao naweka pembeni. Kunasiku niliulizwa na bosi hivi hawa nao ni degree holder nkasema tu mh. Serikali iingilie kati. Tunaogopa kuwapa kazi hawa. Mie kama nna mdogo wangu bora nimpeleke pale VETA atatoka yuko powa ata hiyo certificate.Nikweli mkuu waliingia na gia ya udini lakini ukishindwa kulipa hata sh 400,huwezi kufanya UE kisa hujamaliza ada.Inasakitisha sana kwakweli.
Haya ni matokeo ya kutofanya vizuri kidato cha sita,ungefanya vizuri ungekuwa UDSM au DIT,ufaulu wako hafifu huko chini unakuja kujaza sever za jf bure tuInaendelea
2.Kukosekana kwa wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali kama vile Maprofesa(Professors), Madaktari(Doctors), Wakufunzi waandamizi(senior lecturers) kwenye vitivo vya UALIMU,CSE,EEE,CIVIL,ECE,MECHANICAL kulingana na sheria za vyuo vikuu, mapungufu haya yanapelekea kukiukwa kwa sheria za nchi na kupelekea kukosekana kwa ubora wa elimu inayotolewa katika chuo hiki na kutokidhi mahitaji ya kitaifa na kimataifa, wanafunzi wanasikitishwa na mwenendo wa chombo chenye dhamana ya kusimamia Elimu ya juu katika nchi yetu kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki kwa kipindi kirefu jambo lililopelekea wanafunzi kukosa imani na serikali yao na kukatishwa tamaa ya kuendelea na masomo katika chuo hiki.
3. Uwepo wa wakufunzi wasiokuwa na sifa stahiki na uzoefu katika kufundisha masomo ya Elimu ya juu.Wakufunzi wasiokuwa na sifa stahiki huletwa kwa wingi kutokea nchini India, na wengine huajiriwa kwa sababu ya kuwa na undugu/familia na baadhi ya viongozi wajuu wa chuo hiki. Jambo hili ni kinyume na sheria za ajira Tanzania kwa uongozi kushindwa kutoa fursa sawa za ajira kwa wazawa na wageni pia kwa kuajiri zaidi ya asilimia 80 ya watumishi wa chuo hiki ni wageni na sio wazawa jambo ambalo ni kinyume na sheria na taratibu za ajira kwasababu ajira zinazofanywa na wageni zinaweza kufanywa na wazawa, ushahidi wa kutokidhi sifa za ukufunzi upo kwa baadhi ya wakufunzi kukosa sifa za kitaaluma ambazo wanapaswa kuwa nazo ili kutimiza majukumu katika ngazi mbali mbali za vitivo mfano mkuu wa idara ya shahada ya Uhandisi wa Umeme akiwa na sifa ya mkufunzi msaidizi (assistant lecturer).
4. Kuwa na maabara zenye vifaa duni (chakavu), zisizokidhi ubora na mahitaji ya fani mbali mbali zifundishwazo chuoni, kwa mfano kozi ya uhandisi wa mekanika kukosa maabara muhimu katika masomo yao na kozi nyingine za ualimu na uhandisi kuwa na maabara zisizo na vifaa, wataalam na zisizokidhi ubora wa kitaifa na kimataifa.Upungufu huu unapelekea taifa kuzalisha wataalamu na walimu wasio na ujuzi wa kutosha katika fani husika jambo ambalo ni hatari kwa ajira zao na ustawi mzima wa taifa.
5. Maktaba isiyokidhi viwango vya ubora wa kutoa huduma kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu. Hili linatokana na kukosekana kwa vitabu muhimu na vya kutosha na kukosekana kwa miundombinu rafiki kulingana na idadi ya wanafunzi wa fani zote, hili linadhoofisha ufanisi wa shughuli za kitaaluma kwani masomo ya Elimu ya juu yanamuhitaji mwanafunzi kujisomea na kufanya tafiti mbalimbali katika fani husika na hivyo kuwafanya
Kidato cha sita na two ya point 12,lakini hivyo vyuo unavyovisifia ni bora hata na hii st joe.Chungulia humu kuna uzi unaozungumzia hizo takataka unazozisifia.Kwa ufupi tu elewa tz hakuna chuo kizuri kwa engineering.Ndio mana tunapambana kiboreshwe na sio hatukuwa na uwezo kuja kusoma kwenye hizo takataka za kumeza desa tu.Haya ni matokeo ya kutofanya vizuri kidato cha sita,ungefanya vizuri ungekuwa UDSM au DIT,ufaulu wako hafifu huko chini unakuja kujaza sever za jf bure tu
TCU wamewatupa,Waziri wa elimu naye amewatupa,basi nyinyi wanafunzi ndio MAJIPU sema hamjielewi tuLeo ndo nineamini prof ndalichako na yeye ni jipu haiwezekani apewe walaka ulioandaliwa na serikali ya wanafunzi na kuusoma in two days ndani kukiwa na matatizo yote yanawakabili wanafunzi afu anafika chuoni anaanza kuwasikiliza wahindi badala ya serikali ya wanafunzi na ilipofika zamu ya serikali ya wanafunzi kuzungumzia matatizo yanayowakabili anamnyang'anya raisi wa chuo kipaza sauti kwamba asiongee vitu ambavyo havijaongelewa na huku vyote vipo kwenye ule walaka ulioandaliwa na yeye kupewa na sijaona umuhimu wake wa kuja chuoni maana hakuna hata kitu kimoja alichotatua afadhali angebaki hukohuko hata asije..!!
Hivi na wewe una degree?,mbona hata kuandika hujui?.Bora nisipate kazi kwenye taasisi yenu kama nawewe ni muajiri.Ndio maana hatuajiri wanaotoka chuo hiko
Hadi wewe unaajiri......!!!Kadanganye watoto hukoNdio maana hatuajiri wanaotoka chuo hiko
Sawa mkuu umesikika.Mi naona apa madai ni mawil tu..
1.Ada ipungue
2. Hela za mkopo zifike kwa wakati
Vinginevyo hamtaki kusoma...kwan ukiwa prof ndo unajua...kwa hyo angekuja billgate kufundisha mngemkataa?...mbona hao wahind wanatoa product nzuri tu tena zenye discipline kuliko vyuo vyote....Someni acheni utani
Mkuu matatizo ya msingi ya nyumba yako unaweza kuyafahamu zaidi kuliko matatizo ya nyumba yajirani yako kwa hiyo unapoambiwa matatizo ya hiki chuo sio kuangalia tu picha ya nje na ukatolea ufafanuzi kiasi hicho na tuliopo huku tunakushangaa sana maana hujui hata tumeanzia wapi na tumeishia wapi mpaka mida hii....!!!!Mi naona apa madai ni mawil tu..
1.Ada ipungue
2. Hela za mkopo zifike kwa wakati
Vinginevyo hamtaki kusoma...kwan ukiwa prof ndo unajua...kwa hyo angekuja billgate kufundisha mngemkataa?...mbona hao wahind wanatoa product nzuri tu tena zenye discipline kuliko vyuo vyote....Someni acheni utani
Mtaishia kurudi darasani na kusoma basiMkuu matatizo ya msingi ya nyumba yako unaweza kuyafahamu zaidi kuliko matatizo ya nyumba yajirani yako kwa hiyo unapoambiwa matatizo ya hiki chuo sio kuangalia tu picha ya nje na ukatolea ufafanuzi kiasi hicho na tuliopo huku tunakushangaa sana maana hujui hata tumeanzia wapi na tumeishia wapi mpaka mida hii....!!!!
Engineers are meant to be innovative and create jobs. Huo mkwara wa kuajiliwa kawatishie waliosemea udereva wa meli au garimoshi.Ndio maana hatuajiri wanaotoka chuo hiko