St Joseph ni jipu

maudambwi

Member
Oct 14, 2014
15
4
Chuo cha st joseph cha engineering & technology kilichopo mbezi luguruni ni mmoja chuo ambacho hakiko kwenye ubora wa kutoa mafunzo ya uhandisi. Why?
1. Chuo hakina qualified lectureres wa kutosha hasa hasa senior lectureres. Hakuna prof hata mmoja huku madocta hwazidi wa4 na wamebobea kwenye masomo ya kompyuta eng au comunications etc. Kwahyo kozi kama mech eng na civil haina senior lecturer hata mmoja.
2. Workshops na labs chache, ndogo na hazina vifaa vya kutosheleza.
3. Maktaba iliyopo ina vitabu vichache mno na vingi ambavyo ni muhimu havipo.
4. Uongozi wa chuo ni mbovu ukizingatia chuo cha uhandisi kinaongozwa na mhindi mwenye masters ya linguistics. Prospectus ya chuo haijajitosheleza, staffs wa kila kozi hawajaoanishwa.
5. Ucheleweshwaji wa pesa za meals and acmdtn huku za field zinatolewa baada ya field.
6. Ada ya chuo ni kubwa na hailandani na huduma tunazopata chuoni hapa. Pia chuo hakilipi kodi why a huge tuition fee?

Matatizo ni mengi lkn na inahitaji uchunguzi wa kina na cio wa kijinga jinga tcu wanaoufanya.

TUNAITAJI VYUO BORA. CIO BORA CHUO, ILIMRADI KIWEPO.

Mama ndalichako tunaomba msaada wako. Asante.
 
Mkuu nadhani kuna haja ya kufanya ukaguzi wa kina kwa vyuo vyote. Naamini kuna vyuo vingi havistahili kuwepo.Leo hii tunalia ajira hakuna wakati kiuhalisia wahitimu wengi hawajaiva kabisa(half-baked)
 
Chuo cha st joseph cha engineering & technology kilichopo mbezi luguruni ni mmoja chuo ambacho hakiko kwenye ubora wa kutoa mafunzo ya uhandisi. Why?
1. Chuo hakina qualified lectureres wa kutosha hasa hasa senior lectureres. Hakuna prof hata mmoja huku madocta hwazidi wa4 na wamebobea kwenye masomo ya kompyuta eng au comunications etc. Kwahyo kozi kama mech eng na civil haina senior lecturer hata mmoja.
2. Workshops na labs chache, ndogo na hazina vifaa vya kutosheleza.
3. Maktaba iliyopo ina vitabu vichache mno na vingi ambavyo ni muhimu havipo.
4. Uongozi wa chuo ni mbovu ukizingatia chuo cha uhandisi kinaongozwa na mhindi mwenye masters ya linguistics. Prospectus ya chuo haijajitosheleza, staffs wa kila kozi hawajaoanishwa.
5. Ucheleweshwaji wa pesa za meals and acmdtn huku za field zinatolewa baada ya field.
6. Ada ya chuo ni kubwa na hailandani na huduma tunazopata chuoni hapa. Pia chuo hakilipi kodi why a huge tuition fee?

Matatizo ni mengi lkn na inahitaji uchunguzi wa kina na cio wa kijinga jinga tcu wanaoufanya.

TUNAITAJI VYUO BORA. CIO BORA CHUO, ILIMRADI KIWEPO.

Mama ndalichako tunaomba msaada wako. Asante.
hivi kabla havijaanza kazi si waanaandikisha na kukaguliwa na kupata idhini ya kuviendesha sasa kila uchao tunasikia malalamiko ya hivi vyuo mkaguzi ndio jipu namba moja au ni vyake au alipewa rushwa akavigubalia ilhal anajua kabisa havina kiwango
 
hivi kabla havijaanza kazi si waanaandikisha na kukaguliwa na kupata idhini ya kuviendesha sasa kila uchao tunasikia malalamiko ya hivi vyuo mkaguzi ndio jipu namba moja au ni vyake au alipewa rushwa akavigubalia ilhal anajua kabisa havina kiwango
Mkuu kwanza tz hakuna chuo kinachojitoshekeza kila kitu kwa course yeyote.But matatizo yaliyopo st joseph niyamuda mrefu na nadiriki kusema Prof Mgaya ni jipu tena anahusika kukilinda hichi chuo.Chuo kimeharibika baada ya wale wanaoitwa washiriki ambao ni kanikasa katoliki kujitoa.
 
WARAKA MAALUM KUHUSU CHUO CHA MT.YOSEFU KAMPASI KUU (LUGURUNI, KIBAMBA - DAR ES SALAAM).

UTANGULIZI Chuo cha MTAKATIFU YOSEFU.

Tawi la Luguruni jijini Dar es salaam ni kinatoa Stashahada na shahada za Uhandisi na ualimu wa masomo ya Sayansi.Chuo hiki kinasimamiwa na watawa wa Maria Immaculate wakishirikiana na wawekezaji kutoka nchini India.Waraka huu umeandikwa kwa kuzingatia malalamiko ya muda mrefu ya wanafunzi dhidi ya ukiukwaji wa sheria ya vyuo vikuu hasa sheria namba 7 ya mwaka 2005 ambayo inatoa muongozo juu ya uendeshaji mzima wa shughuli za vyuo vikuu sera na taratibu za kisheria zilizowekwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya wizara ya Elimu na Sayansi. Kukiukwa kwa sheria hizi kumepelekea chuo cha MTAKATIFU YOSEFU kukosa sifa stahiki za kuendelea kutoa huduma ya kitaaluma, kwa kuzingatia matakwa ya kisheria waraka huu umeandaliwa ili kuufahamisha umma wa watanzania juu ya ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa vyuo vikuu nchini Tanzania katika kampasi kuu ya Mt. YOSEFU (Luguruni kibamba-Dar es salaam). Kwa msingi huo waraka huu unabainisha mapungufu ya kiungozi katika chuo cha Mt.YOSEFU, Mapungufu ya uendeshwaji wa shughuli za kitaaluma, hatua ambazo zimechukuliwa na wanafunzi katika kutatua changamoto mbalimbali na madai ya wanafunzi katika namna sahihi ya kutatua changamoto mbalimbali.

CHANGAMOTO MBALIMBALI AMBAZO WANAFUNZI WA CHUO CHA MTAKATIFU YOSEFU WANAKUTANA NAZO KATIKA SHUGHULI ZA KITAALUMA.

1. Kuwepo kwa uongozi mbovu wa Chuo, ukiongozwa na makamu mkuu wa chuo (vice principal) mwenye shahada ya pili ya Lugha (Masters in Linguistics) ambayo ni kinyume na sheria na taratibu za vyuo vikuu ambazo zinabainisha sifa za makamu wa chuo anapaswa kuwa Elimu katika ngazi ya ni UProfesa au Uprofesa msaidizi(Associate professor or Professor) ambaye anapaswa kubobea katika masomo ya fani zinazotolewa chuoni.Vice principal huyu anajulikana kwa jina la Mr. Loyola Prateep hana sifa na uzoefu wa majukumu ya uongozi wa chuo, Hili limemfanya kuwa na uongozi kutumia kauli za vitisho vya kusitisha masomo ya wanafunzi au kutishia ajira ya wafanyakazi pale wanapohoji maamuzi yake juu ya masuala mbalimbali yanayohusu taratibu za uendeshaji wa shughuli mbalimbali na hasa za kitaaluma chuoni.
 
Mkuu kwanza tz hakuna chuo kinachojitoshekeza kila kitu kwa course yeyote.But matatizo yaliyopo st joseph niyamuda mrefu na nadiriki kusema Prof Mgaya ni jipu tena anahusika kukilinda hichi chuo.Chuo kimeharibika baada ya wale wanaoitwa washiriki ambao ni kanikasa katoliki kujitoa.
Hicho chuo si cha walutheri?
 
Inaendelea

2.Kukosekana kwa wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali kama vile Maprofesa(Professors), Madaktari(Doctors), Wakufunzi waandamizi(senior lecturers) kwenye vitivo vya UALIMU,CSE,EEE,CIVIL,ECE,MECHANICAL kulingana na sheria za vyuo vikuu, mapungufu haya yanapelekea kukiukwa kwa sheria za nchi na kupelekea kukosekana kwa ubora wa elimu inayotolewa katika chuo hiki na kutokidhi mahitaji ya kitaifa na kimataifa, wanafunzi wanasikitishwa na mwenendo wa chombo chenye dhamana ya kusimamia Elimu ya juu katika nchi yetu kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki kwa kipindi kirefu jambo lililopelekea wanafunzi kukosa imani na serikali yao na kukatishwa tamaa ya kuendelea na masomo katika chuo hiki.

3. Uwepo wa wakufunzi wasiokuwa na sifa stahiki na uzoefu katika kufundisha masomo ya Elimu ya juu.Wakufunzi wasiokuwa na sifa stahiki huletwa kwa wingi kutokea nchini India, na wengine huajiriwa kwa sababu ya kuwa na undugu/familia na baadhi ya viongozi wajuu wa chuo hiki. Jambo hili ni kinyume na sheria za ajira Tanzania kwa uongozi kushindwa kutoa fursa sawa za ajira kwa wazawa na wageni pia kwa kuajiri zaidi ya asilimia 80 ya watumishi wa chuo hiki ni wageni na sio wazawa jambo ambalo ni kinyume na sheria na taratibu za ajira kwasababu ajira zinazofanywa na wageni zinaweza kufanywa na wazawa, ushahidi wa kutokidhi sifa za ukufunzi upo kwa baadhi ya wakufunzi kukosa sifa za kitaaluma ambazo wanapaswa kuwa nazo ili kutimiza majukumu katika ngazi mbali mbali za vitivo mfano mkuu wa idara ya shahada ya Uhandisi wa Umeme akiwa na sifa ya mkufunzi msaidizi (assistant lecturer).

4. Kuwa na maabara zenye vifaa duni (chakavu), zisizokidhi ubora na mahitaji ya fani mbali mbali zifundishwazo chuoni, kwa mfano kozi ya uhandisi wa mekanika kukosa maabara muhimu katika masomo yao na kozi nyingine za ualimu na uhandisi kuwa na maabara zisizo na vifaa, wataalam na zisizokidhi ubora wa kitaifa na kimataifa.Upungufu huu unapelekea taifa kuzalisha wataalamu na walimu wasio na ujuzi wa kutosha katika fani husika jambo ambalo ni hatari kwa ajira zao na ustawi mzima wa taifa.

5. Maktaba isiyokidhi viwango vya ubora wa kutoa huduma kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu. Hili linatokana na kukosekana kwa vitabu muhimu na vya kutosha na kukosekana kwa miundombinu rafiki kulingana na idadi ya wanafunzi wa fani zote, hili linadhoofisha ufanisi wa shughuli za kitaaluma kwani masomo ya Elimu ya juu yanamuhitaji mwanafunzi kujisomea na kufanya tafiti mbalimbali katika fani husika na hivyo kuwafanya
 
Inaendelea.

wanafunzi kutokuwa na hali ya kujituma katika masomo yao na kupelekea kuwa na wataalamu wasiokuwa na sifa.

6. Kutokuwa na mazingira rafiki ya kujisomea kwa wanafunzi, mazingira ya nje ya chuo ambayo wanafunzi huweza kutumia katika kujisomea kwa mfano kuna eneo linalotumika kwa ajiri ya huduma za chakula(cafeteria) isiyokuwa na ubora na kuwa hatarishi kwa afya za wanafunzi kwani paa lake limeezekwa kwa material ya plastic ambayo ni hatari pale ambapo jua linawaka wakati wa mchana.Eneo hili pia hutumiwa na wanafunzi kujisomea jambo ambalo ni hatari kwa afya za wanafunzi na linadhoofisha shughuli za kitaaluma chuoni.

7. Ukiukwaji wa Haki za wanafunzi na ubaguzi, Hili ni suala ambalo lipo wazi kwa baadhi ya wakufunzi wenye asili ya kihindi kufanya unyanyasaji na ubaguzi, kwa mfano katika nchi ya India miezi kadhaa iliyopita mwanafunzi wa kitanzania alidhalilishwa kwa kuchaniwa nguo zake na kulazimishwa kutembea katika hali ya utupu hadharani. Hata huku kumekuwa na vitendo hivi vya unyanyasaji kwa kutoa kauli za kufedhehesha kwa wanafunzi wa kitanzania, kwa mfano wanafunzi wa kitivo cha ualimu walitolewa maneno ya kufedhehesha na mkuu wa kitivo chao kwa kudai kuwa wanafunzi wa kitivo hicho ni maskini kwa sababu wao hudai fedha za mikopo za kujikimu mara kwa mara. Vile vile wanafunzi wote wamekuwa wakilazimishwa kuwa na akaunti katika benki ya EXIM pekee kwaajili ya pesa za mikopo ambapo inasadikika uongozi huitumia benki hii kuchelewesha fedha za wanafunzi kwa makusudi kwa kuziweka katika Fixed akaunti kwa faida ya chuo, jambo hili limepelekea kuwa na migomo isiyo ya lazima kwa wanafunzi kushinikiza kulipwa pesa zao pale wanafunzi wanapo fatilia fedha zao na kubaini bodi ya mikopo imewasilisha pesa za wanafunzi chuoni kwa kipindi kirefu. Vile vile kumekuwa na ucheleweshaji wa makusudi wa malipo ya bima ya afya jambo linalo sababisha kuchelewa kwa kadi za Bima ya afya ya Taifa kwa wanafunzi wa chuo, uzembe huu umepelekea baadhi ya wanafunzi kukosa kadi za bima ya afya kwa miaka mitatu ili hali wamekuwa wakichangia pesa kwaajili ya michango ya bima ya afya.

8. Kuwa na mitaala isiyokidhi (mibovu) mahitaji ya kitaifa na kimataifa, mitaala inayofundishwa haiendani na matakwa ya sera ya elimu na mitaala hii haikidhi mahitaji ya soko la ajira la kitaifa na kimataifa. Kumekuwa na udanganyifu juu ya mitaala inayofundishwa kuwa inaendana na sera ya taifa katika elimu jambo ambalo si kweli kwani mtaala uliopitishwa na tume ya vyuo vikuu ni tofauti na mtaala unaofundishwa, Kwa mfano mtaala wa kitivo cha ualimu hauna uhusiano wowote na mitaala ya vyuo vingine
 
Inaendelea.

katika nchi yetu na wanafunzi wamekuwa wakifundishwa vitu wasivyojua watavitumia vipi pale watakapo hitimu masomo yao na kwenda kuwajibika katika fani waliyobobea.

9. Ucheleweshaji wa vyeti na mahafali kwa wahitimu kwa kuwa na sababu isiyo na msingi, kwa kumsubiria kiongozi mkuu wa wamiliki wa chuo kwa kutoa sababu ya kutoweza kuja nchini Tanzania katika majira ya kiangazi, kwa sababu hiyo wanafunzi wanao hitimu wamekuwa wakichelewa kupata ajira na kushindwa kuendelea na masomo ya udhamiri(masters), kwani huchelewa wakati wa kuanza masomo hayo.Wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa masomo wamekuwa wakihitmu mwezi septemba wa kila mwaka na Vyeti vya muda/matokeo (Provisional certificates/Transcripts) hutolewa mwezi wa Februari ya mwaka unaofuatia baada ya kuhitimu, Uongozi wa cho umeshindwa kuwa na ratiba au muda wa kutoa vyeti vya kitaaluma unaotambulika kwa wanafunzi walio hitimu masomo yao na jambo hili hupeleka usumbufu na gharama zisizo za lazima katika kufatilia vyeti chuoni.

10. Ratiba ya kuhitimu masomo isiyoendana na ratiba za vyuo vingine na isiyotoa fursa kwa wahitimu wa chuo hiki kuingia kwa wakati sahihi katika soko la ajira. Kulingana na taratibu zilizowekwa na Tume ya vyuo vikuu (TCU) vyuo vingi nchini humaliza mwaka wa masomo mwezi julai. Chuo cha Mt. YOSEFU kimekuwa na ratiba inayo kamilisha mwaka wa masomo mwezi octoba, Sababu kubwa inayopelekea kuchelewa huko ni kusubiria wanafunzi wengine wa mwaka wa mwisho ambao mwaka wa mwisho wa masomo baadhi ya wanafunzi humalizia masomo yao nchini India na sio nchini kwetu kwa hiyo ili kuhitimu, wanafunzi wa mwaka wa mwisho huwa hawana budi kusubiria wenzao walio India ili kuhitimu pamoja. Jambo hili limekuwa likiwaumiza wanafunzi si tu kwa kuchelewa kuingia katika ushindani wa soko la ajira lakini pia limekuwa likiwafanya waishi maisha magumu katika miezi michache kabla ya kuhitimu kwani fedha za kujikimu ambazo wanakopeshwa na bodi ya mikopo hutolewa kwa kuzingatia ratiba ya kukamilika kwa mwaka wa mwisho wa masomo ambapo pesa hukadiriwa mpaka mwezi julai jambo linalowafanya wanafunzi wa mwaka wa mwisho kuwa na bajeti ya ziada kwa miezi mitatu inayoongezeka ili kukamilisha mwaka wa masomo.

11. Viwango vikubwa vya ada ya masomo kwa mwaka na michango mingine katika chuo. Kiwango cha ada ni kikubwa na kumekuwa hakuna mchanganuo wa malipo ya ada ambayo wanafunzi wanapaswa kuilipa kwaajili ya mwaka wa masomo, vilevile kumekosekana uwazi juu ya kiwango halisi ambacho wanafunzi wanapaswa kulipa kwani katika kitabu cha muongozo cha Tume ya vyuo vikuu Ada elekezi kwa mujibu wa Tume ni tofauti na kiwango halisi ambacho mwanafunzi anapaswa kulipa ili aweze kuruhusiwa kuendelea na masomo. Kwa mfano Ada elekezi ya mwaka mwaka jana iliyoainishwa katika kitabu cha Tume ya vyuo vikuu (TCU) kwa kozi za shahada ya ualimu wa sayansi ilikuwa ni
 
Inaendelea.

Tsh.1,500,000/= wakati kiwango halisi cha ada ambayo ilitozwa na chuo ni Tsh.1,820,000/= bila ya michango yeyote na ada iliyojumuisha michango mingine ilikuwa ni Tsh.2,100,400/=. Hali hii iko vivyo hivyo kwa kozi za uhandisi ambapo ada na michango Mingine inafikia TSh. 3,000,000/=. Hili limekuwa ni suala ambalo haliwaumizi wanafunzi tu bali wazazi wote wenye watoto wanaosoma katika chuo hiki ambao wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa ambao hau hakisi hali halisi ya viwango vya ada katika vyuo vingine nchini kwetu.Vile vile kumekuwa na viwango vikubwa vya ada ya mitihani ambayo ina faini endapo mwanafunzi atachelewa kulipa. Viwango hivi vipo kati ya Tsh. 120,000/= hadi 150,000/= Kwa mwaka wa masomo viwango hivi ni vikubwa na havina uhalisia na viwango vya ada za mitihani katika vyuo vingine.

HATUA ZILIZOTEKELEZWA NA WANAFUNZI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOBAINISHWA.

1. Mnamo mwaka 2013 wanafunzi wa kitivo cha Ulimu waliwasilisha kwa wizara ya elimu changamoto zinazowakumba na mwaka huo huo Tume ya vyuo vikuu (TCU) ilituma timu ya wataalumu waliokuja kufanya uchunguzi zidi ya madai ya wanafunzi na walitoa ahadi ya kutoa suluhisho kwa changamoto ambazo wanafunzi walikuwa wakizipata. Hata hivyo mwaka huo ulipita bila ya changamoto kutatuliwa.

2. Mnamo mwaka 2014 kwa mara nyengine Tume ya vyuo vikuu (TCU) ilituma timu ya wataalamu kufanya uchunguzi kwa kuzingatia kanuni na taratibu, Tume ya vyuo vikuu ilipata nafasi ya kufanya kikao na serikali ya wanafunzi na changamoto ziliwasilishwa na serikali ya wanafunzi kwa niaba ya wanafunzi na Tume ili ahidi kuchukua hatua katika kuhakikisha changamoto zinatatuliwa na shughuli za masomo kuendelea kama kawaida kwa kuzingatia taratibu, sheria na kanuni za vyuo vikuu.

3. Katika kuendelea kutafuta suluhisho za changamoto hizi ambazo ilionekana kutotafutiwa suluhisho mapema, mnamo mwaka 2015 wanafunzi wa chuo hiki walifanya mgomo wa kutoingia madarasani jambo lililopelekea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuagiza wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi kuunda tume ya uchunguzi na kuhakikisha ripoti ya chuo hiki inawasilishwa bungeni, katika kutafuta suluhu ya changamoto zilizoainishwa katika waraka huu aliyekuwa Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi wa serikali ya awamu ya nne Mh.Shukuru Kawambwa mwaka huo alifika chuoni akiambatana na Katibu mtendaji Tume ya vyuo (TCU) vikuu ndugu Prof,Yunus .D. Mgaya, ambapo walikutana na uongozi wa chuo, cha kusikitisha hawakuweza kuonana na wanafunzi ambao ndio wa hangwa wa changamoto za chuo hiki na hata kile kilichoafikiwa katika kikao cha Mh.Waziri na uongozi wa chuo
 
Inaendelea.

wanafunzi hawakupata fursa ya kufahamu na ripoti nzima ya kile ambacho Bunge liliagiza haifahamiki hata hivi sasa.

4. Mwaka huu wanafunzi wote wa chuo hiki wamekuwa katika hali ya kuhakikisha changamoto hizi sugu zinapata suluhisho sahihi na la kudumu, wanafunzi wa vyuo vikuu vishiriki kampasi ya songea,kampasi ya arusha wamekuwa katika migomo ya kuhakikisha changamoto zinazokikumba chuo hiki zinapata suluhisho, baada ya Tume ya vyuo vikuu (TCU) kujiridhisha juu mapungufu yaliyokuwapo katika vyuo vikuu vishiriki vya Mt.YOSEFU (Kampasi ya Songea na Arusha) Tume ya vyuo vikuu (TCU) ilifikia uamuzi wa kuvifutia hati ya kuendesha masomo kwa kutokidhi matakwa ya sheria za vyuo vikuu.Baada ya kufungwa kwa kampasi ya Songea ambayo ilikuwa ikitoa masomo ya shahada na stashahada za kilimo na ualimu na sababu zilizopelekea kufungiwa kwa chuo hiki kufanana na changamoto zinazopatikana katika kampasi kuu ya chuo hiki na kampasi ya Arusha.

5. Serikali ya wanafunzi ilichukua hatua kwa kuomba ufafanuzi kutoka kwa uongozi wa chuo juu ya uhalali wa kuendelea na masomo ili hali changamoto hizi zikiendelea, kwa kufuata ngazi kimamlaka serikali ya wanafunzi ilihitisha kikao cha dharura na kumuomba Makamu mkuu wa chuo (Vice pricipal) kuhudhuria kikao hicho kwa lengo la kutoa ufafanuzi kwa serikali ya wanafunzi juu madai ya wanafunzi. Makamu Mkuu wa chuo (vice principal) alimuagiza chief dean of student kukutana na serikali ya wanafunzi kwa niaba yake ili kutoa majibu ya kile ambacho wanafunzi waliiagiza serikali yao katika kupata ufafanuzi wa madai ya wanafunzi. Kwa bahati mbaya hakukuwa na majibu kutoka kwa Dean of students ambaye aliitaka serikali ya wanafunzi kumtafuta Mkuu wa chuo (Vice chancellor) ambaye kimamlaka alipaswa kuwa na majibu ya madai wanafunzi.

6. Serikali ya wanafunzi iliandika barua ikimuomba mkuu wa chuo kukutana na serikali ya wanafunzi ili kuipatia serikali ya wanafunzi majibu ya madai ya wanafunzi wa chuo hiki, kwa bahati mbaya barua ya serikali ya wanafunzi haikujibiwa, na vice chancellor hakutokea kama aivyoombwa na serikali ya wanafunzi. Baada ya jitihada za kuonana na uongozi wa chuo kushindikana Serikali ya wananfunzi iliamua kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizi kwa kuihusisha Tume ya vyuo vikuu(TCU) ambapo majibu ya Tume hayakuwa ya kuridhisha na yakifanana na majibu ambayo imekuwa ikiyatoa hata miaka iliyopita na leo changamoto zimekuwa sugu na zenye kuhatarisha shughuli zote za kitaaluma. Serikalli ya wanafunzi iliridhia kwenda katika ngazi ya wizara na Tarehe 26 machi 2016 serikali ya wanafunzi ikiongozwa na Rais ilifika wizara ya Elimu,sayansi na Teknolojia ikiwa na lengo la kuonana na Mh.Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako ambapo serikali ya wanafunzi
 
Inaendelea.

haikupata ushirikiano kutoka kwa watendaji wa wizara na zaidi serikali iliagizwa kurudi Tume ya vyuo vikuu (TCU), ambapo taratibu zilizotolewa na Tume ya vyuo vikuu katika kutafuta suluhu ya changamoto za chuo hiki hazikuwa ridhisha wanafunzi kulingana na ukubwa wa changamoto na hitaji la haraka katika kupata suluhisho la kudumu.

MADAI YA WANAFUNZI JUU YA HATUA SAHIHI ZA KUZINGATIA KATIKA KUTAFUTA SULUHISHO KWA CHANGAMOTO ZINAZOWAPATA KATIKA SHUGHULI ZA KITAALUMA.

1. MADAI YA WANAFUNZI KITIVO CHA UALIMU Kutokana na sababu zilizopelekea kufungwa kwa vyuo vikuu vishiriki vya Mt.YOSEFU (kampasi ya Arusha na kampasi ya Songea), kama ilivyobainishwa na katibu mtendaji Tume ya vyuo vikuu(TCU) Prof.Yunus.D.Mgaya kuwa vyuo vikuu vishiriki vilikiuka taratibu na sheria za vyuo vikuu ikiwa ni pamoja na kufundisha na mitaala isiyokidhi ubora wa mahitaji ya kitaifa na kimataifa na kwa mujibu wa sera ya Elimu ya Taifa.Wanafunzi wa kitivo cha ualimu katika kampasi kuu ya chuo cha Mt.YOSEFU (Luguruni) hawaoni uhalali wa kuendelea na masomo katika kampasi kuu, kwa kuzingatia sababu zilizopelekea vyuo vikuu vishiriki (kampasi za Arusha na Songea) kufutwa kwa kuwa na mtaala usio na sifa ambapo ni mtaala huo huo unaotumika katika kitivo cha ualimu kampasi kuu(Luguruni), wanafunzi wa kitivo cha ualimu wanaiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwahamisha wanafunzi wote wa kitivo cha elimu kutoka chuo hiki na kuwapeleka katika vyuo vingine.

Ombi hili linapewa nguvu ya kimantiki kwa kuwa kampasi kuu ya Mt.YOSEFU ina sifa za kutoa masomo ya uhandisi pekee na haina miundombinu, sera, mtaala na wataalamu wanaoweza kukidhi mahitaji ya utoaji wa fani ya shahada ya ualimu wa sayansi.

Na kulingana na mapungufu ya mtaala wa kitivo cha ualimu wa masomo ya sayansi uhakika wa ajira ya wahitimu wa kitivo cha ualimu upo mashakani. Kutokana na sababu hizo wanafunzi wa kitivo cha elimu hawatakuwa tayari kuendelea na masomo hadi hapo serikali itakaposikiliza maombi yao ya kuhamishiwa katika vyuo vingine.

Na kwa mantiki hiyo wanafunzi wa kitivo cha ualimu wapo tayari kushirikiana na serikali ili kuhakikisha ombi la wanafunzi wa kitivo cha elimu linatekelezwa kwa ufanisi na kuepusha hali yeyote ya kuzorotesha shughuli za kitaaluma kwa wanafunzi wa kitivo cha ualimu ambao ndio watakao kuwa msingi na uti wa mgongo wa Taifa katika kuliletea taifa wataalamu na kuleta chachu kwa maendeleo ya Taifa Letu.
 
Inaendelea.

MADAI YAWANAFUNZI KITIVO CHA UHANDISI.

Kwa kuzingatia hatua zilizochukuliwa na wanafunzi kwa kushirikiana na serikali ya wanafunzi toka mnamo mwaka 2013, na kwa kuzingatia taratibu na kanuni katika kutatua changamoto mbalimbali, wanafunzi waliona umuhimu wa kuihusisha Tume ya vyuo vikuu(TCU) ambayo inazifahamu changamoto za chuo hiki kwa kipindi kirefu, Hata hivyo kutokana na kukosekana kwa suluhisho kwa changamoto hizi ambazo toka mwaka 2013 Tume imekuwa ikiahidi kuzitatua, wanafunzi wamekosa imani na Tume hiyo, na kwa kuwa imebainika Tume ya vyuo vikuu(TCU) inachukua hatua stahiki pale inapopata msukumo toka kwa wanafunzi wanaoguswa na changamoto za kitaaluma, Wanafunzi wa Kitivo cha uhandisi wanahitaji kufanyika kwa marekebisho kwa yaliyopelekea kutokea kwa changamoto zilizobainishwa kwa haraka iwezekanavyo, na katika kipindi cha kufanyika marekebisho wanafunzi hawatakuwa tayari kuendelea na masomo kwasababu hakuna mantiki ya kuendelea na masomo ili hali kukiwa na wakufunzi wasio na sifa, upungufu wa vifaa vya kufundishia na kukosekana kwa maabara muhimu za masomo ya uhandisi.

Katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wa shahada za uhandisi wanapata Elimu bora itakayowafanya waweze kutambulika na bodi mbalimbali za kitaalamu kama Bodi ya usajili wa wahandisi (Engineers registration Board), na kupata fursa ya kutumia ujuzi wao katika fani walizobobea na kuendana na soko la ajira nchini kwetu.

Wanafunzi wa kitivo cha uhandisi wanaiomba serikali kukifunga chuo kwa muda ili kuruhusu mapungufu yaliyobainishwa ambayo ni muhimu katika kufanikisha shughuli za kitaaluma yanatatuliwa na wanafunzi watakuwa tayari kuendelea na shughuli za kitaaluma endapo tu changamoto zilizoainishwa katika waraka huu zinapata suluhisho sahihi na kwa wakati, kutokana na ukweli ambao Tume ya vyuo vikuu (TCU) imekuwa ikiwaeleza wanafunzi kuwa mara kwa mara Tume imekuwa ikuagiza uongozi wa chuo kufanyia kazi mapungufu mbalimbali, na pengine kwa makusudi au la uongozi wa chuo umeshindwa kufanyia marekebisho changamoto hizi huku masomo yakiendelea, basi wanafunzi wanaona kuna kila sababu ya kusitisha shughuli za kitaaluma ili kuuonyesha uongozi wa chuo kuwa changamoto zinazo kikumba chuo ni kubwa na zinazohitaji marekebisho ya haraka na makubwa ili kuhakikisha Elimu na wataalamu wanaohitimu katika chuo hiki wanakuwa ni wataalamu wenye sifa na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa na wenye kuleta tija kwa Taifa letu.
 
Itaendelea yaliyoongelewa jana na leo asubuhi katika kikao na hawa matapeli wa kihindi na pia kikao cha saa tisa.
 
Back
Top Bottom