DOKEZO Serikali itupie jicho Chuo cha St. Joseph kwa madudu haya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kwenda: Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania – TCU 23 Julai 2024

Mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha St. Joseph kilichopo Mbezi Luguruni, Dar es Salaam, ambacho kinatoa kozi mbalimbali za sayansi, ikiwemo udaktari. Dhumuni la barua hii ni kuomba Taasisi yako tukufu kutembelea na kufanya ukaguzi wa matatizo ambayo yamekuwa yakifanyika na kulelewa na uongozi wa chuo kwa muda mrefu sasa. Hali hii imefika mahali ambapo hatujui wa kumwelekea zaidi ya taasisi yako na Wizara ya Elimu Pamoja na Mama Samia mwenyewe.

Ukweli ni kwamba matatizo haya, hadi yanapofika kwako, tafadhali tambua kuwa tumeshajaribu kufuata ngazi mbalimbali za uongozi ndani ya chuo chetu, kuanzia katika idara zetu hadi kwa Makamu Mkuu wa Chuo, lakini hadi sasa hatujaona mabadiliko yoyote na hali yetu kama wanafunzi ni mbaya bado. Naomba nitoe ufafanuzi wa baadhi ya matatizo tunayokabiliana nayo hapa:

  • Matokeo ya Mitihani: Matokeo ya mitihani yanachelewa kutolewa kwa wakati na hayawekwi kwenye mifumo. Tunapofuatilia tunapewa kauli mbaya na tunashindwa kupata msaada wa kutatua tatizo hili ndani ya chuo. Hali hii inasababisha wanafunzi ambao hawafanyi vizuri kubeba mzigo mkubwa wakati wa mitihani, hivyo matokeo kuwa mabaya zaidi na wengine mpaka wanabeba masomo mihula mingine.
  • Uvujishaji wa Mitihani na Hongo za Ngono na Pesa: Asilimia kubwa ya walimu wanavujisha mitihani kwa wanafunzi kwa njia za rushwa, ikihusisha ngono na pesa. Wanafunzi wanaokataa kutoa rushwa wanashindwa kwa makusudi na walimu wa masomo, na hakuna hatua zinazochukuliwa na uongozi licha ya ushahidi ulio wazi. Mfano wa hali hii ni kitengo cha Biochemistry, ambacho kimekuwa na tabia hii kwa muda mrefu, pamoja na vitengo vingine. Kinachoshtua zaidi ni kwamba vitendo hivi vinaendelea kwa uwazi na walimu wanaohusika hawachukuliwi hatua zozote.
  • Ufundishaji wa Walimu: Walimu hawaingii darasani kwa kutosha na kwa wakati, hasa katika mafunzo ya vitendo ambapo usimamizi unakuwa sio mzuri. Hii inafanya kuwa ngumu kwa mwanafunzi kuwa mbobezi katika fani ya udaktari. Mbaya zaidi, walimu hawapo pamoja na wanafunzi wakati wa kwenda kwenye vitendo hospitalini na tunakuwa chini ya usimamizi wa mahospitali ambao pia hawana muda na sisi, na mwishowe wanatupa alama ilimradi wakamilishe wajibu wao bila kujali uwezo wetu.
  • Ushauri wa Walimu: Walimu wanatumia lugha chachu na ushauri wao unakuwa wa hovyo. Hawapiti vizuri kile tulichoandika, hivyo kukosesha alama na wengi wao wanaishia kupata supplementary. Na hizi supplementary zinahitaji kulipiwa, jambo ambalo sio haki tokea mwanzo.
  • Kuhama kwa Wanafunzi: Kwa baadhi ya wanafunzi ambao hawawezi kuvumilia uonevu wa St. Joseph na wanataka kuhama, chuo kinakuwa kigumu sana kuwaachia wahame, jambo linaloleta madhara kwa mwanafunzi na kujikuta akisoma bila furaha. Baadhi ya njia wanayotumia ni kutotoa matokeo kwa wakati kwa wanafunzi, ili kuwaweka kwenye hali ngumu ya kuhamia vyuo vingine.
  • Idadi ya Wanafunzi na Vifaa: Chuo kinajaza wanafunzi zaidi ya kiwango kilichowekwa na Tume ya Vyuo Vikuu, ambapo hufanya waalimu kutofundisha vizuri na sisi wanafunzi kutopata elimu bora kama chuo kinavyotangaza. Wingi wa wanafunzi unatusababisha kushindwa kutumia nafasi vizuri kwa sababu ya msongamano na upungufu wa rasilimali za elimu kama vitabu katika maktaba.
  • Vifaa vya Masomo ya Vitendo: Wakati wa masomo ya vitendo, tunakuta vifaa ni vichache na vingine ni vibovu au vimeisha muda wake. Maabara yao ni ndogo na hazikidhi viwango vilivyowekwa na TCU na taasisi nyingine za afya. Hii inatokana na tamaa ya uongozi kuangalia maslahi yao binafsi badala ya kuzingatia ubora wa wahitimu wa chuo.
Kama nilivyosema awali, matatizo haya yanaweza kuonekana kuwa madogo lakini yanapokuwa katika kujenga taifa lenye madaktari bora, haya ni makubwa sana na wanaoumia ni sisi wanafunzi ambao tukitoka hapa tunategemewa kutoa tiba bora kwa wanadamu. Tumeona pia kuwa chuo kinachukua mwanafunzi kwa wingi kwa sababu kozi za afya zinagombaniwa sana, hivyo hali hii inafanya kelele zetu kuwa sio kipaumbele kwao.

Hivyo basi, tunaomba wizara yako itupie jicho katika suala hili. Nimeona ni muhimu kutumia wakati huu wa udahili ili wanafunzi watarajiwa wajue changamoto za chuo hiki. Nikiamini kwa muongozo wako, kweli yatapewa kipaumbele na kutafutiwa suluhisho.

Naomba nisisitize msaada wako.

Pamoja katika ujenzi wa taifa.

Nakala:
WIZARA YA ELIMU
TAKUKURU
MCT
 
Poleni sana nimeona wanafunz hawa kwenye taasisi fulani wakiwa mazoezin ni kweli wako unga unakuta uelewa wa mambo anazidiwa na mwanafunzi wa uuguzi mwaka wa pili

Ada kubwa tu treatment nzur aaaaaah

Sema mngesoma kwa bidii mkasoma vyuo vya serikali mngeinjoy kama vp achana na udaktar kasome uuguzi UDOM
Ila kitakachowasaidia ni kusambaza habari kila sehemu kupitia kila platform iwe Facebook, Instagram, ticktock na Twitter watabadilika tu ili wasikose wateja ila serikali itakuwa vigum maana wakaguzi watakula rushwa wanyamaze tu
 
Kwenda: Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania – TCU 23 Julai 2024

Mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha St. Joseph kilichopo Mbezi Luguruni, Dar es Salaam, ambacho kinatoa kozi mbalimbali za sayansi, ikiwemo udaktari. Dhumuni la barua hii ni kuomba Taasisi yako tukufu kutembelea na kufanya ukaguzi wa matatizo ambayo yamekuwa yakifanyika na kulelewa na uongozi wa chuo kwa muda mrefu sasa. Hali hii imefika mahali ambapo hatujui wa kumwelekea zaidi ya taasisi yako na Wizara ya Elimu Pamoja na Mama Samia mwenyewe.

Ukweli ni kwamba matatizo haya, hadi yanapofika kwako, tafadhali tambua kuwa tumeshajaribu kufuata ngazi mbalimbali za uongozi ndani ya chuo chetu, kuanzia katika idara zetu hadi kwa Makamu Mkuu wa Chuo, lakini hadi sasa hatujaona mabadiliko yoyote na hali yetu kama wanafunzi ni mbaya bado. Naomba nitoe ufafanuzi wa baadhi ya matatizo tunayokabiliana nayo hapa:

  • Matokeo ya Mitihani: Matokeo ya mitihani yanachelewa kutolewa kwa wakati na hayawekwi kwenye mifumo. Tunapofuatilia tunapewa kauli mbaya na tunashindwa kupata msaada wa kutatua tatizo hili ndani ya chuo. Hali hii inasababisha wanafunzi ambao hawafanyi vizuri kubeba mzigo mkubwa wakati wa mitihani, hivyo matokeo kuwa mabaya zaidi na wengine mpaka wanabeba masomo mihula mingine.
  • Uvujishaji wa Mitihani na Hongo za Ngono na Pesa: Asilimia kubwa ya walimu wanavujisha mitihani kwa wanafunzi kwa njia za rushwa, ikihusisha ngono na pesa. Wanafunzi wanaokataa kutoa rushwa wanashindwa kwa makusudi na walimu wa masomo, na hakuna hatua zinazochukuliwa na uongozi licha ya ushahidi ulio wazi. Mfano wa hali hii ni kitengo cha Biochemistry, ambacho kimekuwa na tabia hii kwa muda mrefu, pamoja na vitengo vingine. Kinachoshtua zaidi ni kwamba vitendo hivi vinaendelea kwa uwazi na walimu wanaohusika hawachukuliwi hatua zozote.
  • Ufundishaji wa Walimu: Walimu hawaingii darasani kwa kutosha na kwa wakati, hasa katika mafunzo ya vitendo ambapo usimamizi unakuwa sio mzuri. Hii inafanya kuwa ngumu kwa mwanafunzi kuwa mbobezi katika fani ya udaktari. Mbaya zaidi, walimu hawapo pamoja na wanafunzi wakati wa kwenda kwenye vitendo hospitalini na tunakuwa chini ya usimamizi wa mahospitali ambao pia hawana muda na sisi, na mwishowe wanatupa alama ilimradi wakamilishe wajibu wao bila kujali uwezo wetu.
  • Ushauri wa Walimu: Walimu wanatumia lugha chachu na ushauri wao unakuwa wa hovyo. Hawapiti vizuri kile tulichoandika, hivyo kukosesha alama na wengi wao wanaishia kupata supplementary. Na hizi supplementary zinahitaji kulipiwa, jambo ambalo sio haki tokea mwanzo.
  • Kuhama kwa Wanafunzi: Kwa baadhi ya wanafunzi ambao hawawezi kuvumilia uonevu wa St. Joseph na wanataka kuhama, chuo kinakuwa kigumu sana kuwaachia wahame, jambo linaloleta madhara kwa mwanafunzi na kujikuta akisoma bila furaha. Baadhi ya njia wanayotumia ni kutotoa matokeo kwa wakati kwa wanafunzi, ili kuwaweka kwenye hali ngumu ya kuhamia vyuo vingine.
  • Idadi ya Wanafunzi na Vifaa: Chuo kinajaza wanafunzi zaidi ya kiwango kilichowekwa na Tume ya Vyuo Vikuu, ambapo hufanya waalimu kutofundisha vizuri na sisi wanafunzi kutopata elimu bora kama chuo kinavyotangaza. Wingi wa wanafunzi unatusababisha kushindwa kutumia nafasi vizuri kwa sababu ya msongamano na upungufu wa rasilimali za elimu kama vitabu katika maktaba.
  • Vifaa vya Masomo ya Vitendo: Wakati wa masomo ya vitendo, tunakuta vifaa ni vichache na vingine ni vibovu au vimeisha muda wake. Maabara yao ni ndogo na hazikidhi viwango vilivyowekwa na TCU na taasisi nyingine za afya. Hii inatokana na tamaa ya uongozi kuangalia maslahi yao binafsi badala ya kuzingatia ubora wa wahitimu wa chuo.
Kama nilivyosema awali, matatizo haya yanaweza kuonekana kuwa madogo lakini yanapokuwa katika kujenga taifa lenye madaktari bora, haya ni makubwa sana na wanaoumia ni sisi wanafunzi ambao tukitoka hapa tunategemewa kutoa tiba bora kwa wanadamu. Tumeona pia kuwa chuo kinachukua mwanafunzi kwa wingi kwa sababu kozi za afya zinagombaniwa sana, hivyo hali hii inafanya kelele zetu kuwa sio kipaumbele kwao.

Hivyo basi, tunaomba wizara yako itupie jicho katika suala hili. Nimeona ni muhimu kutumia wakati huu wa udahili ili wanafunzi watarajiwa wajue changamoto za chuo hiki. Nikiamini kwa muongozo wako, kweli yatapewa kipaumbele na kutafutiwa suluhisho.

Naomba nisisitize msaada wako.

Pamoja katika ujenzi wa taifa.

Nakala:
WIZARA YA ELIMU
TAKUKURU
MCT
Saint Joseph ya luguruni Mbezi wanatoa kozi za uhandisi na ualimu tu
Hamna kozi ya afya pale , Branch ya Boko ndio kuna vitivo vya afya
 
Shida ya vyuo vya private ni kunyanyasika tu alafu wanawatoza ada kubwa. nashauri mkifanikiwa ni kheri uhamie government achana na mavyuo ya private hakufai huko.
 
Mhh! Nina dogo amechaguliwa computer science mwaka huu hapo St Joseph vipi napo kwenye hiyo department kuna matatizo kama hayo ya huko kwenye Afya? Msaada tafadhari
 
Ukiitwa kutoa ushahidi unaweza kuthibitisha (una vielelezo vya rushwa ya ngono, hongo) au haya uliyoyasndika unadhani ndiyo hufanyika hapo chuoni?
 
Back
Top Bottom