Ssebo hakujenga nyumba Dar?

Ssebo hakujenga nyumba Dar?

Hapa duniani tunapita. Umewahi kuona mtu anajenga njiani
 
Umekuja hapa kutuambia hana nyumba ili tumcheke lakini huwezi kujua anapitia mitihani gani. Mara nyingi hapa Tanzania ukiwa na kipato kizuri kidogo watu wanakunyonya mpaka unachanganuikiwa hata sijui kama utakumbuka kujenga. Watu wanataka pesa zako tu mpaka uishiwe kama hujajenga majungu kama ya mleta mada hapa. Bongo bora uwe kapuku tu utakuwa na amani
 
Watanzania sijui mtaacha lini haya maisha ya kikuda! Ndiyo maana miaka ile nilipoenda kufanya kazi kijijini na kununua Toyota Carina TI yangu, baadhi ya watu wenye mtazamo kama wa kwako wakanishangaa eti nimenunua gari, huku ninaishi nyumba ya kupanga!

Kha! Kwani kujenga nyumba ni lazima?
Kujenga nyumba sio lazima ila tutakushangaa kwanini huwezi kujenga wakati una hela
 
Naona bongoland kua na nyumba au kujenga nyumba ni big deal, kuna watu wanaamua tu hawataki kujenga ili mradi atapanga sehemu nzuri bila tatizo. Maana wengine wanaona shida ujenge li nyumba la milioni 200 Kibada sijui Goba, baada ya miaka kama 5 unavuta unawaacha familia na madeni ya bank si sawa. Bora hio pesa upange ila watoto waende shule za uhakika likitokea la lakutokea umewaachia watoto msingi wa elimu bora bila madeni.
Wewe kidogo ndio umeeleza kimantiki wengine ni maskini wennzetu wasisema eti hawataki tu kujenga bila sababu
 
Nikayakumbuka ya makamu wa raisi yule ,watu wanaulizana je familia iende wapi ? Waliokubali kuwasitiri wanaulizana upenuni watakaa siku ngapi ?

Nikiwa na rafiki yangu katika ile familia ,mama akasema rafiki yako mualike aje kuishi hapa nyumbani ,wakati nafanya huo mpango na mimi mzee akanitimua nyumbani nikaenda kuishi machungwa keko ,dah rafiki yangu akapitia shida na mimi huku nikawa wa uswazi bila kupenda eti natetea ndoto ninayoitaka ,yakanikuta nikaenda kuliwa na mbu bila kupenda .

Kujenga si muhimu kama kipato kipo na kinajitosheleza ila kama kina shida basi dunduliza walau upate kwa kujikinga na fedhea kwa wanao ukiondoka .

Ila kujenga sio lazima wala sio suala la msingi ikiwa sio sehemu ya focus zako ,ssebo sioni kama alikuwa mtu wa mambo hayo ya kiswahili ijapokuwa nyumba alikuwa nayo ila ndiyo vile wanasema mmbeya hasubili pakuche ,mleta mada kaja mbio mbio bila kuuliza .

Nazungumza haya nikiwa na ushahidi wa mjengo wake labda ikiwa aliuza , kabla ya kifo
 
Watanzania sijui mtaacha lini haya maisha ya kikuda! Ndiyo maana miaka ile nilipoenda kufanya kazi kijijini na kununua Toyota Carina TI yangu, baadhi ya watu wenye mtazamo kama wa kwako wakanishangaa eti nimenunua gari, huku ninaishi nyumba ya kupanga!

Kha! Kwani kujenga nyumba ni lazima?
Aisee Wewe uliamua kuishi maisha ya priority zako kwanza, wao walikuwa kwenye syllabus ya lazima uanze na msingi hadi paa 😂
 
Siyo mTZ so hawezi kumiliki ardhi....Kwenye kujenga hakujanishangaza sana ila kuishi kibachela kwa umri wake na alikuwa pia na changamoto za afya ndiyo kimenishangaza.
mbona yeye hakushangaa kuishi kibachela? Unampangia maisha? Unajua kisa cha kuamua kuishi kibachela? Usione watu wanatembea kiongozi.....
 
Nikayakumbuka ya makamu wa raisi yule ,watu wanaulizana je familia iende wapi ? Waliokubali kuwasitiri wanaulizana upenuni watakaa siku ngapi ?

Nikiwa na rafiki yangu katika ile familia ,mama akasema rafiki yako mualike aje kuishi hapa nyumbani ,wakati nafanya huo mpango na mimi mzee akanitimua nyumbani nikaenda kuishi machungwa keko ,dah rafiki yangu akapitia shida na mimi huku nikawa wa uswazi bila kupenda eti natetea ndoto ninayoitaka ,yakanikuta nikaenda kuliwa na mbu bila kupenda .

Kujenga si muhimu kama kipato kipo na kinajitosheleza ila kama kina shida basi dunduliza walau upate kwa kujikinga na fedhea kwa wanao ukiondoka .

Ila kujenga sio lazima wala sio suala la msingi ikiwa sio sehemu ya focus zako ,ssebo sioni kama alikuwa mtu wa mambo hayo ya kiswahili ijapokuwa nyumba alikuwa nayo ila ndiyo vile wanasema mmbeya hasubili pakuche ,mleta mada kaja mbio mbio bila kuuliza .

Nazungumza haya nikiwa na ushahidi wa mjengo wake labda ikiwa aliuza , kabla ya kifo
Makamu wa Rais alikosa nyumba? Au
 
Watanzania mnaamini sana katika nyumba kama kobe harafu zimewatia kwenye wimbi la umasikini kwa kutaka sifa ya kuwa na nyumba huku uwezo mdogo badala ya kuendeleza biashara unatoa hela Dukani unapelela kwenye nyumba baadae unaenda tena NMB wakupe mkopo wa riba kubwa inapelelea nyumba hiyo kuuzwa tena..
😂😂😂😂
 
Tanzania kuna wenye nyumba maskini sana
 
Hata Uganda msiba umefanyika mtaani tu. Aisee K sio dili
 
Back
Top Bottom