Spring of Sadness - Eric Shigongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spring of Sadness - Eric Shigongo

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Sanda Matuta, Dec 31, 2009.

 1. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Naombeni msaada wenu kwenye hili na ikiwezekana toeni ushauri wenu kwa huyu Bwn. Shigongo, kwangu kama nimepituka na Watunzi wengine wa hadithi na sinema za Kitanzania na kuzipa majina ya kiingereza.

  Mimi binafsi sio mtaalam wa lugha hiyo ya kiingereza ila kwa kiasi fulani naweza kugundua kosa.

  Juzi hapa nilisoma katika gazeti la Risasi kama sikosei huyo Bw Shigongo ameandika hadithi humo na kuipa Jina la SPRING OF SADNESS na kuitafsiri kwa kiswahili kwa KISIMA CHA HUZUNI.

  Kwa maana halisi ya hicho kingereza hapo yaani SPRING ni tofauti kabisa na maana mgeuzo ya KISIMA kwa kingeleza.

  Kisima ni maji yaliyo tulia tofauti kabisa na spring,spring ni maji yaliyo katika kububujika au kutiririka.

  Nadhani Bwn.Shigongo angetafuta watu wanao jua lugha hizo vizuri akawapa kazi ya edit hadithi zake na kuzirekebisha pale inapo bidi,na si tu kuziweka kwenye kurasa.

  Magazeti yake yanasomwa na watu wengi, wengine wapo katika kujifunza, sasa unapomwambia spring ni kisima na kubeba hiyo maana, then atabisha hata kwenye ukweli akiaambiwa spring si kisima.

  Na kama mimi ndio nisiye elewa hapa basi tafadhali nielimisheni
   
 2. locust60

  locust60 Senior Member

  #2
  Dec 31, 2009
  Joined: Oct 1, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu sanda matuta unasema kingereza au kingeleza?.sijaelewa
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  To be precise spring ni chemchemi more than kisima.

  Unaweza kuchimba ardhi na kutengeneza kisima kwa kuipata water table iliyo chini.Hiki ni kisima.Well.

  Spring ni maji yanayokuja juu yenyewe na kububujika.Chemchemi.

  Shigongo mbona michemsho yake ni major tu, yaani hili ukilingnisha na michemko mingine utaona wala si issue kabisa.
   
 4. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ha ha........!

  Asante mkuu kwa malekebisho.
  Nilikotokea kwenye R tuna weka L,na the opp.is also true
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo ulitaka tafsiri ya SPRING OF SADNESS IWEJE?...ulitaka iwe ni

  maji yaliyo katika kububujika au kutiririka YA HUZUNI..! au vipi?:eek::D
   
 6. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi sikuta iwe vyovyote ila kwa maana HARISI.
  Angeweza kuandika tu 'KISIMA CHA HUZUNI' na ikaleta maana inayo jitosheleza,hakukua na haja ya KINGEREZA kwani walengwa wa hizo hadithi walio wengi hawajui hiyo lugha au wapo katika kujifunza hiyo lugha.
  Kwa kuwapa maana ya maneno zisizo sahihi ni kuwapotosha katika kijifunza.
  Sasa labda wewe uwe na mawazo mengine?!
   
 7. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  "MTIRIRIKO WA HUZUNI" ......ingefaa zaidi.

  Lakini sisi si Shigongo yeye mwenyewe ndio mwenye haki ya kuamua.
  Tunachoweza kufanya ni kushauri kile kilicho sahihi tu!
   
 8. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,696
  Likes Received: 8,232
  Trophy Points: 280
  Nadhani na wewe una uhusiano na Shigongo wa kutafsiri ndovyo sivyo..spring of sadness=chemchemi ya huzuni!
  Nawakilisha..
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Nimekuerewa poti:)! Marekebisho tunasema malekebisho!
   
 10. k

  klf Member

  #10
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Je, tuna hakika kwamba kichwa cha maneno hakimaanishi/hakihusu kipindi cha mwaka cha kuchipua? Kwa Kingereza husemwa mara nyingi kwa mfano "Winter of Sorrow/Discontent" bila kuwepo kwa nia ya kugusia mambo ya hali ya hewa hata kidogo. Matumizi haya ni ya kitamathali.
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Hii ni zamani ila leo nimekuwa nikipekua kila linalotokea mbele yangu na kuliwekea komenti ikiwezekana.

  Kwa hapa, phrase ya "Spring of Sadness" bila kuanza na "the" ina maana kuwa kipindi cha kuchipua, kinachofuata mara tu baada ya kipupwe, hakikuwa cha furaha. The Spring ina maana ya spiringi kama tunavyozijua za kwenye gari, na Sadness siyo maombolezo, bali ni kukosa furaha. Matumizi ya neno spring kwa maana ya kisima au chem chem ni makosa kwani chem chem inaitwa springs. Kama mheshimiwa Shigongo alitaka kusema "kisima cha maombolezo" angesema "The well of mourns (au mourning)" (-ambayo haisikiki vizuri katika kiingereza) au kama alitaka kusema chemchem ya maombolezo basie angesema "The springs of mourns (au mourning)." Vinginevyo angejiepusha kabisa na kutafsiri neno kwa neno (jambo linalowasumbua sana watu wanaofikiri kwa kiswahili na kuandika/kuzungumza kwa kiingereza) na badala yake akatumia phrase nyingine tofauti kabisa inayochukua maana ya kile alihotaka wasomaji wafahamu.
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  na huyo shigongo ndio mbunge mtarajiwa wa ccm
   
 13. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkulu umeeleweka/nimekuelewa
   
 14. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Huyu bwana kama mtu ulipitapita shule ukasoma vitabu vya kawaida sana kama vile zaka la damu, kijiji chetu, hawala ya fedha, this time tomorrow, mine boy, willy Gamba's (mhusika), Joram Kiango's (mtunzi), Cain and Abel, Sydney sheldon (mtunzi), james hardley chase (e.g. there is always a price tag), ...., etc etc etc, huwezi kuthubutu kusoma vitabu vya shigongo, kwanza title ya novel yenyewe tu inakuboa unaona huyu mtu kama hii profession amesomea, basi hakuiva na hataiva ila ataendelea kulazimisha tu! Sivipendi vitabu vyake kwanza sababu tu ya title na wala huwa sitamani hata nimnunulie mdogo wangu asome!
   
 15. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Huyu bwana kama mtu ulipitapita shule ukasoma vitabu vya kawaida sana kama vile zaka la damu, kijiji chetu, hawala ya fedha, this time tomorrow, mine boy, willy Gamba's (mhusika), Joram Kiango's (mtunzi), Cain and Abel, Sydney sheldon (mtunzi), james hardley chase (e.g. there is always a price tag), ...., etc etc etc, huwezi kuthubutu kusoma vitabu vya shigongo, kwanza title ya novel yenyewe tu inakuboa unaona huyu mtu kama hii profession amesomea, basi hakuiva na hataiva ila ataendelea kulazimisha tu! Sivipendi vitabu vyake kwanza sababu tu ya title na wala huwa sitamani hata nimnunulie mdogo wangu asome!
   
 16. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hata sababu ya huyo ndugu kutafsiri kila mara mimi siielewi. Sijui ndio kutujulisha kiingereza kimemkolea? Makosa ni mengi tu huwa anayafanya mwenye tafsiri zake. Bora abaki na kiswahili tu - kwa ushauri.
   
 17. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #17
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Labda hadithi au riwaya zinakuwa ni za kiingereza na yeye anacho fanya ni kuzitafasiri kwa kiswahili na kudai kuwa yeye ndiye mtunzi.
   
 18. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #18
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Joram Kiango hakuwa mtunzi, alikuwa ni mhusika wa kwenye riwaya... Mtunzi alikuwa ni Ben R. Mtobwa
   
 19. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #19
  Sep 25, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ah, nyinyi mwaona sasa.Lakini sisi ambao tumeanza kusoma hadithi za Shaigongo tanga miaka ile tulishagundua kuwa si lolote wala si chochote.Nadhani tatizo lake kubwa ni ukiritimba wa utunzi.Magazeti yake yote anataka atunge yeye na wala hawapi nafasi watunzi wengine wazuri ambao wamejaa tele nchini.Anatakiwa kubadilika sasa
   
 20. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  chemichemi au chemchem :confused2: ! swali zuri nakupa heko mtoa MADA
   
Loading...