Spinning zinavyotugharimu

Spinning zinavyotugharimu

Tupo kwenye laiti traki. Tutembee vifua mbele. Tuwe wazalendo
 
Operation zifanyike kimya kimya kwa kumuogopa nani?
Kama mnataka misaada yao nendeni kwao mkafanye ushoga mpewe misaada maana naona inawauma sana.
NO USHOGA TANZANIA
Bora tule nyasi.

Msitake kujifichia kwenye ushoga, tatizo ni jiwe kwa kiburi cha madaraka. Kuchezea box la kura, kunyanyasa wapinzani, uhuru wa habari nk. Hilo la ushoga mnalichomekea ili mpate support ya watanzania wengi kuficha sababu hasa za kuchukuliwa hatua.
 
mambo yakiwa magumu Makonda ajiandae kwa kutolewa kafara, ndivyo watakavyo hao wapenda ushoga, jamaa akipigwa chini itabadili upepo...siungi mkono ushoga lkn ndivyo watakavyo hawa mabepari

Hili unalolipendekeza ni gumu sana. Apigwe chini apelekwe wapi? Kuna watu wasiostahili kuwa mbali na mwenye maamuzi. Huyu ni mmoja wapo, kama sio ndie mwenyewe mwenye funguo za makabati yote.

Unasahau pia msemo huu "Ukinilazimisha ndio unaharibu kabisa". Akifanya kama unavyopendekeza atadharauliwa!

Atolewe hapo labda asogezwe ndani zaidi kwenye giza ili atende bila kuonekana kwenye kamera kama ilivyo sasa.
 
Msitake kujifichia kwenye ushoga, tatizo ni jiwe kwa kiburi cha madaraka. Kuchezea box la kura, kunyanyasa wapinzani, uhuru wa habari nk. Hilo la ushoga mnalichomekea ili mpate support ya watanzania wengi kuficha sababu hasa za kuchukuliwa hatua.

Na hili la ushoga ndilo wanaloliweka mbele. Hawataki kabisa hayo mengine yawe sababu za kunyimwa misaada.

Lakini nami pia nawalaumu hawa wazungu kwa kiasi fulani. Tabia yao ni kupiga kelele nyingi linapojitokeza hili la mashoga. Wakati ukandamizaji unapofanyika kwa raia wa kawaida na wanasiasa, sauti zao huyu hafifu sana, na hazisikiki. Hii tabia yao hata mimi huniudhi.
 
this time wamebugi.... sidhani kama bashite aliwashirkisha wataalam
matokeo yake ime backfire mbayaa

wamewamaliza wasanii na watu mashuhuri
wakadhani ushoga utawatoa wakasahau LGBT ni ishu world wide
"tatizo wana spin alot mbinu zmewaishia = na alot of spining ni indicator ya unapropiates somewhere inside!!
Ushoga hautakiwi na watanzania walio wengi sana kwa sababu za kiutamaduni wetu.
Tatizo suala hili linashughulikiwa na mtu asiye na akili kabisa za kumtosha yeye mwenyewe, achilia mbali kuongoza mkoa.
Matokeo tunayaona live.
Mtu anaacha kushughlikia visima, barabara, kero za wananchi anarukia vilivyo juubya uwezo wake kufikiri na kutenda.
 
Na Thadei Ole Mushi.

#Spin Doctor ni taaluma ya kijasusi ya kubadili hali ya mambo. Taaluma hii hutumiwa sana sana na wanasisa katika kuondoa mijadala na kashfa kubwa zinazowakumba au zinazoikumba Serikali.

Najua unajua kuhusu Wasbato maalia waliokuwa wakishinda pale Airport wakisubiri kwenda ulaya bila Passport walivyofanikiwa kuuzima mjadala wa Richmond, Escrow ikazimwa na Rais Mstaafu Kuumwa Tezi Dume nk.

NATAKA KUSEMA NINI?

Denmark ni mojawapo ya nchi zinazounda nchi za Scandinavia ambazo ni Sweden, Finland, Norway, Iceland. Nchi hizi zina ushirikiano mkubwa sana na ndizo zinazochangia asilimia 40 ya Budget yetu. Na hizi Asilimia 40 ndio chanzo cha Uhakika tofuti na asilimia 60 za ndani ambazo Mara nyingine hazifiki na Mpango kakiri bungeni kuwa makusanyo ni madogo.

Baada ya WB wiki hii kutunyima fedha sasa Denmark wametunyima msaada na kumzuia balozi wao kututembelea.

Hili Gazeti la Politiken ndio Gazeti Pendwa na linaloongoza kwa kusomwa nchini Denmark na nchi za Scandinavia. Kuna Kampeni kubwa sana huko njee kuhusu Tanzania.

#Ni kweli kuwa hatukubaliani kwa Pamoja maswala ya Ushoga, Tatizo ni namna tulivyokuwa tunalishughulikia. Haya Mambo huwa yanamalizwa kimya kimya. Someni namna gani Ghana ilipunguza Rushwa iliyokuwa imeitafuna Ghana.

Mambo Mengine huna haja ya Operation za Wazi Bali ni Kimya kimya. Tuangalie Spinning tunazotumia sasa kumaliza agenda za msingi mtaani nani anazitengeneza na je zina Athari gani kwa taifa.

Spinning ni Muhimu ila lazma ziandaliwe na wataalamu baada ya kujiridhisha kuwa hazitaleta athari hapa wanahitajika watu Smart sana...

Kama hali Ikiendelea hivi hatutaweza kupandisha mishahara ya wafanyakazi na mambo mengi ambayo tuliahidi kwenye Ilani na kwenye Budget yanaweza yasikamilike.

Ole Mushi
0712702602View attachment 934811


Ni hivi, baada ya kauli za Makonda, Serikali ilitoa msimamo na kupingana na Makonda. Lakini hawa DENMARK wameendelea kushikilia bango hata baada ya Statement ya serikali. Kwa akili ya kawaida, unaamini uamuzi wa Denmark ni kweli kutokana na mambo ya ushoga au kuna kitu wapigwa chini? TAFAKARI.
 
Back
Top Bottom