Serikali kutoza ushuru asilimia 10 kwenye mashine za kukaushia rangi za kucha

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,943
Reaction score
2,982
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/27 leo Juni 11, 2026, Bungeni, Dodoma. amesema Serikali itaanza kutoza ushuru wa bidhaa wa 10% kwenye mashine za kukaushia rangi za kucha (nail polish dryers) zinazoingizwa nchini, akifafanua hatua hiyo imechukuliwa kimkakati ili kudhibiti afya za watumiaji.

"Lengo la hatua hii, kwanza kabisa ni kuzuia athari za kiafya zinazoweza kutokea kutokana na matumizi ya vifaa hivi, ikiwemo matatizo ya ugonjwa wa saratani," amesema Balozi Khamis Mussa Omar.

Sambamba na hilo, serikali imeongeza ushuru wa bidhaa kutoka 10% hadi 15% kwenye bidhaa nyingine zote za urembo zinazoingizwa kutoka nje ya nchi (cosmetics).

Aidha, Serikali imependekeza kutoza ushuru wa bidhaa wa 20% kwenye maua, matawi, na matunda ya bandia yanayotengenezwa kwa vifaa vya plastiki na kuingizwa nchini. Hatua hii inalenga kupunguza mrundikano wa taka zisizooza, huku ikisaidia kupanua wigo wa kodi na kuongeza mapato ya serikali.

"Kutoza ushuru wa bidhaa wa kiwango cha asilimia 20 kwenye maua ya bandia, matawi ya bandia, matunda ya bandia, pamoja na bidhaa zinazofanana na hizo zinazoingizwa nchini zinazotambulika kwenye HS Heading 67.02. Lengo la hatua hii ni kupunguza athari za kimazingira zinazotokana na matumizi ya bidhaa husika, kuongeza wigo wa kodi, na mapato ya serikali."-Amesema Balozi Khamis Mussa Omar

Pia, kuongeza kiwango cha ushuru wa bidhaa kutoka asilimia 10 hadi asilimia 15 kwenye bidhaa za urembo zinazoingizwa ndani ya nchi zinazotambulika kwa HS Heading 33.03, 33.04, 33.05, na 33.07.
 
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/27 leo Juni 11, 2026, Bungeni, Dodoma. amesema Serikali itaanza kutoza ushuru wa bidhaa wa 10% kwenye mashine za kukaushia rangi za kucha (nail polish dryers) zinazoingizwa nchini, akifafanua hatua hiyo imechukuliwa kimkakati ili kudhibiti afya za watumiaji.

"Lengo la hatua hii, kwanza kabisa ni kuzuia athari za kiafya zinazoweza kutokea kutokana na matumizi ya vifaa hivi, ikiwemo matatizo ya ugonjwa wa saratani," amesema Balozi Khamis Mussa Omar.

Sambamba na hilo, serikali imeongeza ushuru wa bidhaa kutoka 10% hadi 15% kwenye bidhaa nyingine zote za urembo zinazoingizwa kutoka nje ya nchi (cosmetics).
Huyu nae ni mzenji?!
Sasa kama zinamadhara si wazipige marufuku
 
Mbona wameweka asilimia ndoto.
Kukomesha hayo maujinga ya kuweka kucha bandia ilifaa iwe hata 40%
 
Back
Top Bottom