Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,502
- 51,097
Ndugu Spika
Ninakuelewa vizuri, pengine huna uchungu sana na wananchi, kwa sababu mazingira yako ya kuingia bungeni tangu mwanzo, na baada ya uchaguzi 'feki' wa mwaka 2020 ni kwa mbeleko ya dola. Kwa hivyo labda unadhani una cha kuilipa fadhila serikali.
Lakini nataka nikukumbushe tu kuwa nafasi uliyonayo ni nyeti sana, inagusa maslahi ya moja kwa moja ya wananchi. Kwa hiyo nakuomba jambo moja tu kuwa, kama wewe huwezi kutetea wananchi, basi angalau waache wabunge watetee na wasimamie maslahi ya wananchi.
Ndugu Spika, Nimekufuatilia jinsi unavyoendesha bunge haswa katika huu mgogoro wa wananchi wa kimasai huko Ngorongoro na Loliondo, umeonekana huna chembe ya kujali hata kodogo madhila yanayowakuta wananchi wa kimasai.
Wewe unaitetea serikali. Ulianza kwa kuagiza yupe aliyerekodi clip iliyoonyesha wananchi wakikimbia mirindimo ya risasi na mabomu yaliyokuwa yakirushwa na maaskari eti akamatwe, ukasema eti tuko katika vita ya kiuchumi.
Ndugu Tulia, vita ya kiuchumi ndo inamaanisha dola kunyanyasa, kutesa na kuhujumu wananchi wake yenyewe?
Cha kushangaza, badala ya kumuacha Mbunge wa wananchi mheshimiwa Sendeka awakilishe wananchi kwa uhuru na uwazi kadri ya ufahamu wake wewe ukajigeuza Wakili wa serikali kuuliza maswali utadhani bungeni tuko mahakamani. Spika ulitaka kuachive nini? Ulitaka kumfurahisha nani? Ulikuwa unamtetea nani, kwa nini na kwa faida ya nani?
Bahati Nzuri Ole Sendeka alikusomea barua ya Waziri mkuu mstaafu ndugu Mizengo Pinda, ikikutanabahisha kuwa uwelewa wa Serikali kuhusu eneo la Loliondo kuwa ni maeneo ya vijiji vya wananchi kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2009 ya uhifadhi, na kwamba uelewa wa serikali ni kuwa sheria hiyo ilifuta sheria ya uhifadhi ya mwaka 1974. Sasa wewe Tulia ulitaka kuprove bungeni kuwa serikali na akina Mizengo Pinda walikosea kudhani kuwa sheria hiyo ya mwaka 2009 ilifuta ile ya mwaka 1974?
Ndugu Tulia, unafahamika vizuri toka zamani kuwa pale maslahi ya serikali na CCM yanapohongana na wananchi wewe huwa unasimama na serikali, na ndiyo maana unakumbukwa kwa kesi maarufu ya wananchi wasimame umbali gani kutoka kituo cha kupiga kura baada ya kupiga kura.
Yote hii ni kuzuia wananchi wasilinde kura zao zisichakachuliwe. Sasa naona na kwenye hii issue ya ndugu zetu wamasai wewe hujaoi hata kidogo feelings zao, bali upo kuhakikisha dola inalindiwa taswira yake, licha ya uonevu mkubwa wanaotendewa wamasai underground.
Ndugu Spika, Je unajua kuwa OBC na mwanamfalme walikuja nchini kimagumashi?
Ndugu Spika je unajua kuwa OBC inashutumiwa kunuka rushwa na kununua watu kibao tangu ilipoingia nchini?
Ndugu Spika hebu amua sasa. Na wewe uko tayari kuingia katika payroll, au kufanya bidding ya kampuni ya mwarabu ya OBC au unataka kusimama na wananchi?
Ndugu Spika, ushauri wangu kwako. Simama na wananchi, achana na hao waliowekwa mfukoni na OBC. Maana kama kuna machafuko yatakayokuja Tanzania, nayaona yataletwa na hiyo kampuni ikishirikiana na madalali wao, wengine wakiwa ni watu waliowahi kushika nyadhifa kubwa katika nchi hii.
Ndugu Spika,
Wananchi tunataka uhuru wetu, ila naona makampuni ya nje kama hiyo OBC ikishirikiana na madalali wauza nchi wanataka kuupoka huo uhuru. Hatutakubali!