Spika Tulia: Tusijadili masuala ya vyoo Bungeni

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
"Wabunge hapa wameuliza kuhusu vyoo na wewe (Naibu Waziri Dugange) kwenye majibu yako ukatoa majibu, nafikiri kwa nchi yetu tulipofikia ni mahali ambapo hatutakiwi kuwa tunazungumza vyoo kwenye zahanati, choo kimoja pale vyoo viwili pale, serikali inafanya kazi sana na hakuna sababu ya kujadili vyoo humu ndani," - Spika wa Bunge, Dkt. TuliaAckson
 
Anataka ajiweke kwenye position ya kifahari na kwamba ccm wamefanya makubwa na kwamba mambo ya vyoo yanawatia aibu kuzungumzwa humo?

Kweli tunaspika aisee

Choo siyo mhimu? Wakati huo huo unahimiza usafi ili kuepuka kipindupindu?

Ccm, vyoo tu vimewashinda? Kuwasema juu ya jambo la umeme tunawaonea kumbe
 
"Wabunge hapa wameuliza kuhusu vyoo na wewe (Naibu Waziri Dugange) kwenye majibu yako ukatoa majibu, nafikiri kwa nchi yetu tulipofikia ni mahali ambapo hatutakiwi kuwa tunazungumza vyoo kwenye zahanati, choo kimoja pale vyoo viwili pale, serikali inafanya kazi sana na hakuna sababu ya kujadili vyoo humu ndani," - Spika wa Bunge, Dkt. TuliaAckson
Safari moja ya waziri nje ya nchi inajenga vyoo za zahanati mkoa mzima.. na posho za wabunge kwa siku moja zinajenga vyoo vya zahanati nchi nzima
 
Kikokotoo cha wastafu na fao la kujitoa tu vimewashinda kwa nini msijadili vyoo kitu ambacho ni changamoto katika shule, zahanati, hospitali na stendi za mabasi na daladala nchini?
 
Hio ndio level yetu.

Huko ambako hawajadili vyoo wanavyo kila mahala first class na visafi, mashuleni, mahospitalini, na mitaani.

Tumeona vyoo vya manyasi Chato na kwingineko, kwanini tusijadili sasa na kutafuta akili ya kutatua matatizo? Asione aibu hata mbuyu ulianza kama mchicha.

Viwanda tumeua, SGR inasuasua, Sukari utata, umeme utata, sasa anataka tujadili Nuclear power wakati huu wa kidatu tu unatutoa jasho, au anataka tujadili MaICBM, ships building yard, Viwanda vya magari na drones ambazo hatuna.

Madam speaker, hiyo ndio level yetu hatuna namna tujadili tu namna ya watu wetu kupata vyoo Bora, au kwasababu yeye anaishi kwenye mansion Dom, Dar na Mbeya.
 
Nyumba ni choo sasa kama hakuna sijui inaitwa pagala. Acha 2025 ije labda tunaweza kupata nafuuu ya mawazo nje ya kujani
 
Humo ndani ni kumsifia mama tuu

Lete hoja awekwe kwenye fedha

Lete hoja nguo yake iwe nguo ya taifa

Hizi ndio hoja za kujadili bungeni
 
"Wabunge hapa wameuliza kuhusu vyoo na wewe (Naibu Waziri Dugange) kwenye majibu yako ukatoa majibu, nafikiri kwa nchi yetu tulipofikia ni mahali ambapo hatutakiwi kuwa tunazungumza vyoo kwenye zahanati, choo kimoja pale vyoo viwili pale, serikali inafanya kazi sana na hakuna sababu ya kujadili vyoo humu ndani," - Spika wa Bunge, Dkt. TuliaAckson
Je kuna vyoo vya kutosha kwenye kila zahanati humu nchini? Ni visafi? Vinatosha? Kama hapana kwann tusijadili?
 
Ndio shida ya spika ya Bluetooth, inatoa sauti hapa ila aliyeconnect yupo mita kadhaa huko 😂🤣
 
"Wabunge hapa wameuliza kuhusu vyoo na wewe (Naibu Waziri Dugange) kwenye majibu yako ukatoa majibu, nafikiri kwa nchi yetu tulipofikia ni mahali ambapo hatutakiwi kuwa tunazungumza vyoo kwenye zahanati, choo kimoja pale vyoo viwili pale, serikali inafanya kazi sana na hakuna sababu ya kujadili vyoo humu ndani," - Spika wa Bunge, Dkt. TuliaAckson
Sasa wagonjwa hawana pa kunyea wakimuuliza mbunge hana majibu sasa mbunge akaulize wapi?
 
Back
Top Bottom