Masanja nawe unakosea kabisa. Kumbuka Serikali inaundwa na Rais (kwa kushauriana na Waziri Mkuu ambaye naye huteuliwa na Rais). Mtu pekee aliyepata mandate ya wananchi wote ni Rais peke yake na siyo wabunge (mmoja mmoja) wala huyo Waziri Mkuu mwenye ambaye kachaguliwa na watu chini ya 40,000. Waziri Mkuu wanapata nguvu kwa kuwa wabunge wengi ni wa chama chake (Katiba - Waziri Mkuu atatoka chama chenye wabunge wengi au Mbunge mwenye kuungwa mkono na wabunge wengi).
Hili lina ukweli kwa kiasi fulani. Lakini wote wawili (Rais na Wabunge) wanachaguliwa wakiwa na mandate tofauti kabisa na hivyo si sawa kuona kwamba mwingine mwenye mandate moja yuko juu ya mwingine kwa vile ana mandate tofauti. Rais anachaguliwa kuwa kiongozi na mtendaji mkuu wa Taifa letu na anateuliwa kusimamia na kutekeleza ilani ya chama chake kama Rais wa Jamhuri. Na pamoja na hayo anatekeleza majukumu yake anayopewa Kikatiba (siyo kichama). Hiyo ndio mandate yake.
Wabunge wanachaguliwa kuwa wawakilishi wa wananchi siyo katika kusikiliza malalamiko na matatizo yao tu au kushughulikia mambo ya kwenye majimbo yao tu bali kufanya kile ambacho pia wanapewa kikatiba kama mandate yao, yaani "kuishauri na kuisimamia serikali". Kwa maneno mengine wabunge ndio sauti ya wananchi wengi zaidi na siyo Rais!
Wananchi wanapoona mambo hayaendi wanavyotaka au matatizo kwenye uendeshaji wa serikali yao wanapomlilia Rais wanafikiria Rais ni kama Mfalme fulani hivi; Wananchi wanapaswa kuwalilia wabunge wao kwani ni wao ndio wanaweza kuihoji serikali na waziri yoyote juu ya jambo lolote lilimo ndani ya serikali, ni wao wanapitisha fedha za matumizi mbalimbali (bajeti) na ni wao ndio wanatunga sheria za kusimamia au kufuatwa na vyombo vingine. Mandate yao basi ni kubwa mno lakini ni tofauti na ile ya Rais. Na tofauti hii haifanyi mhimili mmoja kuwa juu ya mwingine; bali vyote vikifanya kazi zao sawasawa ndio nchi hujengwa na kazi hutekelezwa.
Bunge likitioa maazimio sio amri kwa Serikali. Serikali inaweza kusema sitekelezi na Bunge linachoweza kufanya na kura ya kutokua na imani. BASI.
Bunge likitoa amri kwa serikali au maagizo kwa serikali; serikali inatakiwa kukataa au kukubali. Ikikataa Bunge linapiga kura ya kutokuwa na imani na serikali hiyo kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani Waziri Mkuu na kumlazimisha kujiuzulu (na kuvunja baraza la mawaziri). Kama serikali haitaki kutekeleza yanayoamriwa na Bunge basi serikali inapoteza uhalali wake kwani hatuwezi kuwa na serikali isiyowatii wananchi wake (kumbuke Bunge ndio wawakilishi wa wananchi na madaraka ya kutawala yanatoka kwa wananchi)!
Tukikubali kuwa serikali inaweza kusema "sitekelezi" tunakubali jambo hatari sana. Leo Bunge linapitisha bajeti ya kutenga bilioni 100 kwa ajili ya mradi wa nishati. Serikali inasema "hatutaki" tutatumia bilioni hizo 100 kujenga madampo ya kuoeshea mifugo. Bunge linakubali kuwa serikali imekataa maagizo ya Bunge, basi Bunge nalo linapoteza uhalali wake kwani linakuwa limeshindwa "kuisimamia" serikali.
Hivyo, sikubali kabisa hii dhana kuwa serikali inaweza kulikatalia Bunge madaraka yake na ikabakia kuwa serikali halali kwani siku serikali ikikataa kusimamiwa na Bunge basi tumeruhusu utawala wa Kiimla.
Sisi tunavyoenda na commentaries ni kana kwamba Bunge linaweza kuilazimisha serikali itende itakacho. Hapana.
Absolutely! Na limepewa njia za kufanya hivyo.
a. Serikali ikikataa wanaweza kupigiwa kura ya kutokuwa na imani, WAziri Mkuu na baraza wanavunjika lakini Bunge na Rais bado wapo
b. Wanaweza kumuita Waziri yeyote na kumhoji jambo lolote lililo chini yake
c. Kujadilii utekelezaji wa kila Wizara wakati wa kikao cha bajeti; kumbuka Bunge ndio wawakilishi wa wananchi hivyo sisi wananchi kupitia wawakilishi wetu tunauliza, vipi kuhusu barabara fulani, vipi kuhusu mpango fulani n.k Serikali haiwezi kukataa kutoa maelezo. Tukikubali hilo tumekwisha!
d. Kujadili na kuidhinisha (yaani sisi wananchi ndio tunakubali) mpango "wowote" wa serikali na siyo tu hilo bali pia kuutengea fedha na kuundia sheria. Rais hana madaraka hayo; hayo ni madaraka yetu wananchi. Tukikubali kuwa serikali inaweza kujitekelezea mpango wake au kuendelea na mpango uliokataliwa na Bunge halafu ikabakia kuwa serikali tukwishnei!
e. Kuridhia mikataba yote ya serikali na hapo ina maana "mapatano yoyote ya mkataba ambayo mmojawapo wa walioshiriki ni Serikali ya
Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Idara
yoyote ya Serikali hiyo au mtumishi yeyote wa Serikali aliyeshiriki
kwa niaba ya Serikali."
Hii ina maana Bunge lilikuwa na haki ya kupitia Mikataba ya Richmond, kama vile lilivyo na haki ya kupitia wa Dowans, Rites, n.k na kuiridhia ikibidi. Na Bunge likisema "serikali vunjeni mkataba huu" serikali haiwezi kusema "hatuvunji" na ikabakia madarakani! Ikifanya hivyo, the parliament has become obsolete and inherently irrelevant.
Mwenye mandate ya kwenda nchi nzima kusema niliwaahidi hili na nimefanya au sikufanya ni Rais peke yake.
Si kweli. Lipo Bunge moja tu nalo linaitwa "Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" hakuna Bunge la Urambo, Bunge la Kigoma Kaskazini au Bunge la Igunga. Hivyo, Bunge nalo lina mandate ya kitaifa kama vile Rais alivyo na mandate yake. Kufikiria kuwa Rais ndiye mwenye mandate ya kitaifa na nyinyi wengine you have parochial mandate ni hatari kwa demokrasia. Wabunge wetu japo wanatoka katika vyama, majimbo na wanaingia tofauti wanaitwa ni "Wabunge wa Jamhuri ya Muungano"!
Spika atarudi Urambo, Zitto Kigoma Kaskazini, Hamad Rashid Wawi etc.
Ndio lakini hawarudi kwenye vibunge vyao huko; na wakirudi bila ya kupigania haki yao ya kusimamia serikali na kuilazimisha serikali kwa njia za kikatiba, wanastahili kubakia huko huko Urambo, Kigoma Kaskazini na Wawi, wasirudi tena Dodoma; hawastahiili.
Hii ni serikali dhaifu tu, Mkapa angesema hapana na ingekuwa HAPANA.
Kama Mkapa naye angeruhusiwa kusema "hapana" kwa vile ni "Mkapa" basi tumekwisha! Madaraka na haki ya Bunge hayategemei nani Rais. Rais angeweza kuwa Malaika Jibrili lakini akiapa kulinda na kuhifadhi Katiba yetu atapimwa kwa kipimo kile kile!
Role ya Bunge katika Richmond ilipaswa kuisha pale Serikali ilipoanguka.
Hapana. Bunge lilitoa melekezo ya Kamati yake (soma haki, madaraka na kinga ya Bunge).. na serikali ilitakiwa kutii. Kilichotakiwa baada ya Lowassa kujiuzulu ni kutekelezwa maazimio yote na wala tusingefika hapa. Pinda ndiye aliyekoroga alipofikiri anaisaidia nchi kwa kuanzisha uchunguzi wake mwenyewe na kufanya vitu ambavyo Bunge halikuagiza. Kwa maneno mengine aliamua kulidharau Bunge (sisi wananchi!). Serikali haiwezi kutudharau wananchi na ikabakia madarakani.
Whenever there is a showdown between the rulers and the people; the people must always rule supreme. Because sovereignty belongs to the people not to the president or prime minister.
Kitendo cha sisi wabunge kuendelea kufuatilia kita backlash lazima maana ukisoma tena ile ripoti kuna siasa nyingi sana mle na kazi haikwisha.
then jadilini Bungeni, toaneni ngeu, na mrarueni; msiogopane. Kama kazi haijaisha au kina Mwakyembe waliboronga ni Bunge tu lina uwezo wa kutengua maamuzi yake siyo? so.. go ahead tengueni yaliyofanywa na kina Mwakyembe, pigeni kura kumrestore Lowassa na kuipa Richmond haki yake. Tutaheshimu uamuzi wenu.
Mfano - kwa nini leo Mwakyembe anasema gazeti la Matanzania watwambie Richmond ni nani. Tulimlipa 438m tshs ili atwambie hivyo.
well.. mkabeni Koo Mwakyembe juu ya hilo.. ndio maana ya kuwa wawakilishi wetu. Jenga hoja Bungeni, pigeni kura hata ikibidi kumng'oa spika lakini Katiba lazima iheshimiwa hata kama ina matobo kuliko ya mapakacha.
Kwa nini Mwakyembe alisema kuna mambo hawakusema ili kuficha aibu ya serikali?
Kama haya waliyoyasema yameshaiabisha hivi hayo mengine si tutaitisha mapinduzi. Lakini, kama wabunge mnaweza kupitia tena maamuzi ya Richmond na kutengeneza kilichoharibiwa na kama kina Mwakyembe walivunja taratibu au sheria ya Bunge, Bunge linaweza kuwaadhibu. Sielewi kinachongojewa ni nini? mnawaogopa hawa kina Mwakyembe?
Kwa nini kwenye vikao vya CCM na wabunge mwakyembe anasema wanaomtetea Lowasa waache maana yakifunuka mengine Lowasa atafungwa jela!
Labda kuna ukweli; Na believe me wanaopush kumsafisha Lowassa they have no idea what is in store for them. Siku moja yatakapotokea kuna watu watawashukuru kina Mwakyembe kwa kutokusababisha wao kuishia Jela. Lakini kama watu wanaamini kuwa Mwakyembe na timu yake wana vitu hawajavisema basi wawalazimishe hata mahakamani au Bungeni kufanya hivyo au wao ndio wapelekwe jela!
Kama Lowasa aliiba mahala pake ni Jela tu na sio pengine. Kwa nini kina mwakyembe walificha na katika ripoti yao walisema "PM APIME"
oh well.. walimpa ushauri wa kuamua kujitetea au kuondoka. Yeye baada ya kupima akaona haya maji mazito akajiuzulu. Well.. siyo kosa la Kamati Teule kuwa Lowassa aliamua kujiuzulu kwa kashfa.
Ukitulia na kuangalia mambo ya nchi yetu kwa jicho la 'objectivity', utachanganyikiwa tu! hatuchanganyikiwi kwa sababu hivi sasa uchambuzi wetu umeegemea makambi na prejudices. When we come back to senses, tutasema ahaaa
Kuna ukweli mkubwa sana hapo.