Spika Ndugai: Wabunge watoro warejeshe fedha zote walizolipwa kuanzia Mei 1-17 jumla ya Tsh. Milioni 110

Nilikuwa nashauri upite mchango wa haraka sn kuwachangia wabunge wetu hiyo mill 110
.
Yaani kumbe wanalipwa 340000 kwa siku moja na tayari walikuwa wamewekewa. hela ya wiki moja
 
Hizi zile za matibabu ya ajabu na wasaidizi wako India wewe spika ndio mchezo umekufa? zinatuuma sana sisi walipa kodi! na kufukia hili ndio maana unatumika vibaya hadi bunge limepoteza mvuto kabisa!
 
Ndugai alikuwa na Audit Query ya matumizi mabaya ya fedha kwenye Audit report ya 2016/17. Kama unakumbuka allazwa Hospitali ya India na kutumia Bilions kwa kuwa alikwenda na familia, nurse na mpambe tofauti na sera inataka aende na msindikizaji mmoja.

Aliporudi utakumbuka alitaka kumtunishia kidogo Jiwe kwa kumtetea Zitto Kabwe alipotaka kushikwa ndani ya Bunge. Na kwa kweli alikuwa na nia ya kutaka kusimama kama Spika Huru na Mhimili wake. Jiwe akamtishia kupitia watu wa Usalama kwa kunmuambia akiendelea kupishana naye basi atazianika kashfa zake zilizoibuliwa na CAG. Nakwamba ifikapo 2020 hawatampitisha kuwa Sipka wa Bunge instead watampitisha Tulia Ackson.

Basi baada ya hapo ikabidi asalimu amri na kuanza kumunga mkono.
Spika Job Ndugai amesema wabunge wa CHADEMA ambao hawashiriki vikao vya bunge kwa madai kuwa wapo karantini wanahesabika kama watoro na wanatakiwa kurejesha fedha zote walizolipwa kwa kipindi ambacho hawatakuwepo bungeni.

Pia wamepaswa kufanya kipimo cha Covid19 kabla hawajaingia bungeni
==

TAARIFA ZAIDI
Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Mei 6, 2020 amewataka wabunge wa CHADEMA waliosusia vikao vya bunge kwa kisingizio cha Corona kurudi haraka bungeni

Spika Ndugai amesema endapo watakaidi agizo hilo la kurudi Bungeni basi itawalazimu siku watakayo rudi wawe na cheti kinachoonesha kuwa wamepima ugonjwa wa Corona na majibu yake na kurudisha pesa walizolipwa ambazo ni posho za vikao la sivyo hatua zaidi zitachukuliwa.

"Wabunge hawa ambao ni watoro walipokuwa wanaondoka walilipwa fedha za kuanzia Mei 1-17 Jumla ya zaidi Tsh. Milioni 110, nawaagiza kuanzia Freeman Mbowe kurudisha Tsh. Milioni 2 na elfu 40 na wenzake wote hao, huu ni utoro wa hiari kwa lugha rahisi huu ni wizi na wale wengine wamelipwa Milioni 3 warudishe" amesema Spika Ndugai.

Aidha Spika Ndugai ameongeza kuwa; "Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na tangazo hilo kwa sababu Mbowe hana mamlaka ya kuitisha utoro wa wiki mbili kwa Wabunge, anajaribu kuwa kama Prefect wa Shule ya Sekondari, japo wameambiana kubaki Dodoma lakini wanazurura nchi nzima, wabunge hao popote walipo warudi bungeni haraka sana kuendelea na kazi zao".

 
Back
Top Bottom