Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,446
- 7,817
Wakati Waziri Mkuu akiahirisha Bunge baada ya hotuba ya Waziri Mkuu, Spika Ndugai ameongelea suala la uaminifu wa watanzania hasa kwa vijana na kudai wawekezaji wengi wamekuwa wakilalamika. Ndugai amesema mtu anaeanzisha mradi atajikuta tu amefilisika asipokuwa makini.
'' Mtu akianzisha labda tuseme 'super market' nisikilizie kama bado utamkuta barabarani miaka mitatu ijayo. Ataibiwa pale si kawaida, hata wewe wekeza halafu njoo bungeni hapa umewaachia miezi sita hujawatembelea, subiri siku utakayoenda upige mahesabu, utakuta umepigwa'' Alisema spika Ndugai.
Aliendelea '' Mswahili humuachii shughuli mkakubaliana usipigwe kwa sababu ya uaminifu, sijui namna gani tutafanyia kazi?''
''Kijana akiwa na fursa kama hiyo akaachiwa asimamie biashara asikuibie, wenzake mtaani wanasema mjinga sana yule, alipewa goli liko wazi kaliacha, mjinga kweli! Jamaa mwaka mzima yuko bungeni kule, yeye kakaa tu lakini uaminifu unalipa sana katika maisha'' Alimalizia Spika Ndugai.