Spika Ndugai sasa ni kama anafanya kazi zilizoachwa na Lissu na Mnyika Bungeni. Tumerudi kwenye Bunge la chama kimoja

Bila wa Tanganyika kukubali kufia wanachokiamini , bado tutaendelea kufanyiwa viini macho kama ya kina Ndugai & johnthebaptist . WANAFIKI
Kumwaga damu zao ?!!

Ndio ukombozi wautakao utakuja na kusimama milele?!!

Hivi kule Ethiopia walipigana mara moja?!!!

Je mapigano ya huko nyuma yamewaletea WALICHOKIPIGANIA kiasi cha kuepusha mapigano haya mapya ya sasa?!!😲🤣

Leo hii Oromia waliodai wanaonewa miaka yote wanaungana na watesi wao wa miaka yote(TPLF) dhidi ya ndugu yao Abiy Ahmed aliyeibadili "status quo".....hapa unajifunza kuwa WANASIASA NA MAKUNDI YENYE NGUVU WAKO TAYARI kuziingiza nchi katika machafuko kwa KAFARA ZA DAMU ZA WALALAHOI NA MASKINI WALIO WENGI.....

#Siempre JMT
#NchiKwanza
 
Kuna nchi iliwahi kupiga hatua kwa kung'ang'ania "Status quo?". Abiy anafail kwa kutaka kurudisha status quo kwa nguvu baada ya kuanza mageuzi bila vision.
Inategemea "status quo" hiyo ni katika eneo lipi.....mara nyingi kubadili status quo ya "mfumo wa utawala" mathalani leo hii kutaka KULETWE SERIKALI 3 badala ya 2 za JMT hakutotuacha salama......
 
Kuna wasiotaka mabadiliko kama Ccm, ndiyo hao hao wanaowaza kuleta machafuko na kuichoma nchi ilimradi masilahi yao bandia wabaki nayo
CCM ndio wanaolinda maslahi mapana ya WATANZANIA wa makundi yote.........

Huo ndio ukweli....
 
Kumwaga damu zao ?!!

Ndio ukombozi wautakao utakuja na kusimama milele?!!

Hivi kule Ethiopia walipigana mara moja?!!!

Je mapigano ya huko nyuma yamewaletea WALICHOKIPIGANIA kiasi cha kuepusha mapigano haya mapya ya sasa?!!

Leo hii Oromia waliodai wanaonewa miaka yote wanaungana na watesi wao wa miaka yote(TPLF) dhidi ya ndugu yao Abiy Ahmed aliyeibadili "status quo".....hapa unajifunza kuwa WANASIASA NA MAKUNDI YENYE NGUVU WAKO TAYARI kuziingiza nchi katika machafuko kwa KAFARA ZA DAMU ZA WALALAHOI NA MASKINI WALIO WENGI.....

#Siempre JMT
#NchiKwanza
Ukileta mabadiliko ya ujanja ujanja mabigano na machafuko hayawezi kukoma . Yataendelea bila kujali ni taifa gani.

Hebu fikiri mwenyewe. Mbona ni mataifa yaliofanya maamuzi ya kweli ndiyo yanaiongoza dunia kiuchumi, kisiasa, kijamii etc. Hapa nazungumzia nchi kama Australia , Japan , Korea kusini, Sweden, Norweig , US nk.

Ukifanya mabadiliko kiujanja ujanja vurugu zitaendelea. Kwa sababu huongozi kuku bali binaadamu wenye uelewa.
 
Bunge bila kambi ya upinzani ni batili. Hapo ni sawa na wako katika vikao vyao vya chama which is non sense kwa mustakabali wa taifa karne hii.
Ndio matakwa ya ccm, kama ingekuwa kinyume chake au wameona umuhimu wa kuwa na wapinzani bungeni basi hizi chaguzi ndogo wangeacha wapinzani WATANGAZWE washindi ili kubalance mambo. Ila still wao ni wao tu.
 
Bunge bila kambi ya upinzani ni batili. Hapo ni sawa na wako katika vikao vyao vya chama which is non sense kwa mustakabali wa taifa karne hii.
Mbinu ya chama kimoja ikianza kubuniwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, wakaweka CCM watupu, ukaja uchaguzi mkuu ukaweka Bunge batili tunaloliona sasa. Spika amesimama nafasi ya upinzani kukosoa serikali, jambo ambalo ni upuuzi mtupu. Kwa kifupi ni bunge batili kwa dunia ya leo.
 
Ukileta mabadiliko ya ujanja ujanja mabigano na machafuko hayawezi kukoma . Yataendelea bila kujali ni taifa gani.

Hebu fikiri mwenyewe. Mbona ni mataifa yaliofanya maamuzi ya kweli ndiyo yanaiongoza dunia kiuchumi, kisiasa, kijamii etc. Hapa nazungumzia nchi kama Australia , Japan , Korea kusini, Sweden, Norweig , US nk.

Ukifanya mabadiliko kiujanja ujanja vurugu zitaendelea. Kwa sababu huongozi kuku bali binaadamu wenye uelewa.
Hizo nchi usemazo zina mengi tunayotofautiana nayo.....

Mathalani hiyo Korea Kusini wana viwanda vingi vinavyotengeneza LCDs ,Photovoltaics ,OLEDs , Semiconductors n.k .....

Wanauza NJE...wana soko kubwa NJE.....

Huwezi kuwekeza katika TEKNOLOJIA bila ya kuwa na SOKO la hiyo TEKNOLOJIA ......

Je unajua kuwa nchi za MAGHARIBI (Waitwao mabeberu) wana mchango mkubwa sana wa maendeleo hayo ya KOREA KUSINI?!!!
 
Nimependa picha ya kipanya, ila ukweli unabaki pale pale Tanzania tumeshindwa kufanyakazi na wapinzani. Ila tutakavyoenda sitashangaa kutokea kitu kama cha akina Njelu Kasaka group. Be a single part does not entirely remove resistance or avoid changes. Hata china walikuja na mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kiutawala ndani ya chama kimoja. Hata issue ya katiba lipo ndani ya CCM ni suala la muda tu. Hata Mh. Kikwete alilianzisha kutuliza wana ccm wenzake ingawaje kimagumashi. Na shida kubwa ipo kwenye muungano na muundo wake. Sidhani hata ccm wanafurahia uchaguzi, kwani unapokaribia ni shida kwani wanashinda kwa gharama kubwa kupita kiasi inapoteza hata maana halisi ya uchaguzi kwani will of people haiheshimiwi tena. Utumiaji wa hila hata mtendaji linamsumbua. Kuumiza Watanzania wenzao kwa kigezo cha upinzani pia hakifurahishi hata kidogo. Huku kunapelekea kutokuleta utengano wa kitaifa na umoja wetu, hili ni la maana sana kwa mstakabali wa nchi.
 
Bila ya CCM nchi hii ingejaa UKANDA NA UKABILA....

Huo ndio ukweli wenyewe.....

#SiempreJMT
Unajipima na kipi ?!. Hapa kwetu kuanzia 2010 mpaka 2020 kulikuwa na halmashauri ziliongozwa wa wapinzani wa Ccm . Je walipata fursa ya kufanya walioyaahaidi kwa wananchi ?!. Zaidi waliishia kuvurugwa na hiyo inayojiita muhimili uliojichimbia . Kwa kawaida walitakiwa wapate nafasi ili watu waone tofauti ya Ccm na wao. Sasa hapo ni uongozi shirikishi kivipi ?!
 
Hizo nchi usemazo zina mengi tunayotofautiana nayo.....

Mathalani hiyo Korea Kusini wana viwanda vingi vinavyotengeneza LCDs ,Photovoltaics ,OLEDs , Semiconductors n.k .....

Wanauza NJE...wana soko kubwa NJE.....

Huwezi kuwekeza katika TEKNOLOJIA bila ya kuwa na SOKO la hiyo TEKNOLOJIA ......

Je unajua kuwa nchi za MAGHARIBI (Waitwao mabeberu) wana mchango mkubwa sana wa maendeleo hayo ya KOREA KUSINI?!!!
Kama hao South Korea wamefaidika na mabeberu . Tanganyika anashindwa nini ?! Wakati 1960s tulikuwa sawa nao kama siyo kuwazidi kabisa hao South Korea, China , Singapore etc.

Hapa tatizo ni Ccm . Amini usiamini . Kujaribu kuipractice u communist uliofeli pote ulimwenguni .
 
Baada ya mkutano wa Bunge kuanza juzi ambapo kimsingi ni kama vile ni bunge la CCM watupu Spika Ndugai ameonekana akibeba jukumu la kuikosoa na kuipa ushauri mbadala Serikali kazi ambayo ilikuwa ikifanywa kwa weledi mkubwa na Tundu Lissu, J J Mnyika na Zitto Kabwe walipokuwa bungeni.

Bunge la namna hii ndio kama lile la Chifu Adam Sapi Mkwawa wakati wa chama kimoja.

Juzi kati mzee Msekwa alisema bila kambi rasmi ya upinzani bungeni basi Bunge hilo huwa ni Bunge la chama kimoja kimaamuzi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Mnaupiga mwingi bungeni kwa miaka zaidi ya 10 mwisho wa siku mnakuja kufanya huu upuuzi.
images (20).jpeg

Hii laana inawatafuna.
 
Nimependa picha ya kipanya, ila ukweli unabaki pale pale Tanzania tumeshindwa kufanyakazi na wapinzani. Ila tutakavyoenda sitashangaa kutokea kitu kama cha akina Njelu Kasaka group. Be a single part does not entirely remove resistance or avoid changes. Hata china walikuja na mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kiutawala ndani ya chama kimoja. Hata issue ya katiba lipo ndani ya CCM ni suala la muda tu. Hata Mh. Kikwete alilianzisha kutuliza wana ccm wenzake ingawaje kimagumashi. Na shida kubwa ipo kwenye muungano na muundo wake. Sidhani hata ccm wanafurahia uchaguzi, kwani unapokaribia ni shida kwani wanashinda kwa gharama kubwa kupita kiasi inapoteza hata maana halisi ya uchaguzi kwani will of people haiheshimiwi tena. Utumiaji wa hila hata mtendaji linamsumbua. Kuumiza Watanzania wenzao kwa kigezo cha upinzani pia hakifurahishi hata kidogo. Huku kunapelekea kutokuleta utengano wa kitaifa na umoja wetu, hili ni la maana sana kwa mstakabali wa nchi.
Waweza kuwa sawa. Lakini si kuwa na watu kama G 55 ambao mwisho wa siku huitwa na kamati za maadili ya chama na kuishia kudhibitiwa. Ukumbuke mwenyekiti wa chama ni Rais .
 
Waweza kuwa sawa. Lakini si kuwa na watu kama G 55 ambao mwisho wa siku huitwa na kamati za maadili ya chama na kuishia kudhibitiwa. Ukumbuke mwenyekiti wa chama ni Rais .
Mr Odiambo group historia inaweza isitudhibitie hilo kwani group jingine likawa limejikita kwenye kitu tofauti chenye mashiko makubwa zaidi au form tofauti likawa gumu kulitatua na hapo kuleta uasi kupelekea kukubali kuondoka chama Tawala na kuunda chama kipya. Nafiki unaona utitiri wa uanjishaji wa vyama vipya. Msajili anasema anamaombi 17 au 18 huu wote unaweza kuwa ni different form of Njelu Kasaka group.
 
Baada ya mkutano wa Bunge kuanza juzi ambapo kimsingi ni kama vile ni Bunge la CCM watupu Spika Ndugai ameonekana akibeba jukumu la kuikosoa na kuipa ushauri mbadala Serikali kazi ambayo ilikuwa ikifanywa kwa weledi mkubwa na Tundu Lissu, J J Mnyika na Zitto Kabwe walipokuwa bungeni.

Bunge la namna hii ndio kama lile la Chifu Adam Sapi Mkwawa wakati wa chama kimoja.

Juzi kati mzee Msekwa alisema bila kambi rasmi ya upinzani bungeni basi Bunge hilo huwa ni Bunge la chama kimoja kimaamuzi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Kidumu Chama Cha Mapinduzi. Kazi iendelee.
 
Back
Top Bottom