Spika Ndugai sasa ni kama anafanya kazi zilizoachwa na Lissu na Mnyika Bungeni. Tumerudi kwenye Bunge la chama kimoja

Mnooo......

Wakati mwingine kubadili "status quo" ni kukaribisha balaa.....balaa haswaaa......

Hayo ndiyo anayokutana nayo mh.Abiy Ahmed wa Ethiopia na mwishowe "anaitia kibiriti nchi"....

#Siempre JMT
Ya ethiopia achana nayo kwa kuwa inajulikana Wa_tigray yaani " ccm wa ethiopia" wameamua nchi ivurugike kwa kuwa wamepoteza madaraka.
 
WaTigrinya ni kabila.....CCM ni chama.... Ethiopia inatafunwa na SIASA ZA KIMANGIMEZA ZA KIKABILA.....

Kwa hoja yako inakuwaje leo WAOROMO waliotengwa waungane na WATESI WAO wa miaka yote hao Tigrinya dhidi ya Abiy Ahmed?
 
Baada ya mkutano wa Bunge kuanza juzi ambapo kimsingi ni kama vile ni Bunge la CCM watupu Spika Ndugai ameonekana akibeba jukumu la kuikosoa na kuipa ushauri mbadala Serikali kazi ambayo ilikuwa ikifanywa kwa weledi mkubwa na Tundu Lissu, J J Mnyika na Zitto Kabwe walipokuwa bungeni.

Bunge la namna hii ndio kama lile la Chifu Adam Sapi Mkwawa wakati wa chama kimoja.

Juzi kati mzee Msekwa alisema bila kambi rasmi ya upinzani bungeni basi Bunge hilo huwa ni Bunge la chama kimoja kimaamuzi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Sio kwamba MaCCM mmempanga DHAIFU, mnatafuta kuzima kinachoendelea mahakama ya kesi za kutunga uongo kwa tofauti za kiitikadi?!
CCM = Chama maiti.
 
Ndio matakwa ya ccm, kama ingekuwa kinyume chake au wameona umuhimu wa kuwa na wapinzani bungeni basi hizi chaguzi ndogo wangeacha wapinzani WATANGAZWE washindi ili kubalance mambo. Ila still wao ni wao tu.
Si kama ccm wote waliridhia hili jambo bali nani angepinga matakwa ya mwendazake? Katika hili jiwe aliharibu sana, kiongozi msikivu, asikilizae ushauri na maoni ya watu mbalimbali na mpenda watu hili asingeruhusu au kuwa chaguo lake kwa mustakabari wa nchi yake. Jiwe hakuwa na sifa hata moja ya hizo zaidi ya kujaa kiburi, umimi, visasi na kupenda sifa
 
Baada ya mkutano wa Bunge kuanza juzi ambapo kimsingi ni kama vile ni Bunge la CCM watupu Spika Ndugai ameonekana akibeba jukumu la kuikosoa na kuipa ushauri mbadala Serikali kazi ambayo ilikuwa ikifanywa kwa weledi mkubwa na Tundu Lissu, J J Mnyika na Zitto Kabwe walipokuwa bungeni.

Bunge la namna hii ndio kama lile la Chifu Adam Sapi Mkwawa wakati wa chama kimoja.

Juzi kati mzee Msekwa alisema bila kambi rasmi ya upinzani bungeni basi Bunge hilo huwa ni Bunge la chama kimoja kimaamuzi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
subiri posho ikate urudi nyumbani
 
WaTigrinya ni kabila.....CCM ni chama.... Ethiopia inatafunwa na SIASA ZA KIMANGIMEZA ZA KIKABILA.....

Kwa hoja yako inakuwaje leo WAOROMO waliotengwa waungane na WATESI WAO wa miaka yote hao Tigrinya dhidi ya Abiy Ahmed?
Wa_tigray walikuwa watawala kama walivyo ccm sasa. Kama wanavyoleta vurugu ethiopia hata hawa ccm ndivyo ambavyo watafanya.
 
Tunasherehekea miaka 60 ya uhuru bila kuwa na Bunge. Hivi sasa tunajivunia nini? Maana nchi hujivunia kuimarika kwa taasisi kama Serikali, Mahakama na Bunge. Sasa siku hivi mahakamani kwenyewe wamejaa wauza Mbege tu
 
Si kama ccm wote waliridhia hili jambo bali nani angepinga matakwa ya mwendazake? Katika hili jiwe aliharibu sana, kiongozi msikivu, asikilizae ushauri na maoni ya watu mbalimbali na mpenda watu hili asingeruhusu au kuwa chaguo lake kwa mustakabari wa nchi yake. Jiwe hakuwa na sifa hata moja ya hizo zaidi ya kujaa kiburi, umimi, visasi na kupenda sifa
Mkuu, siamini kama yalikuwa maamuzi ya Jiwe peke yake. Rejea uchaguzi wa jimbo la Konde kule zanzibar na chaguzi ndogo za marudio zilizofanyika baada ya jiwe kuondoka. Still ni maamuzi ya wakubwa
 
Ni kweli usemalo bwashee!
 
Back
Top Bottom