Spika Ndugai, Pascal Mayalla alijiandaa. Kasome upya makala,utaadhirika...

​

Je Bunge linajipendekeza?

"Naomba nisilijibu swali hili nisije kuitwa mbele ya kamati ya haki,kinga na madaraka ya bunge na kuambiwa nimelikashifu Bunge"
Mwisho wa kunukuu sehemu ya makala inayolalamikiwa.

Mheshimiwa spika kwa heshima na taadhima ningependa kuchukua nafasi hii kukupa ushauri wa bure,licha ya kufahamu kuwa wewe ni nguli wa sheria na ni mbabe lakini katika hili umekurupuka utadharilika mapema na asubuhi.

Nilikusikiliza ulivyokuwa ukitoa povu kuwa bunge ni mhimili na spika sio mtu wa mchezo mchezo na jinsi ulivyokuwa ukimsikitikia pascal kwa kitendo chake cha kuandika makala chonganishi kati ya serikari,wananchi na bunge!
Katika hili mheshimiwa umeshindwa vita kwenye hatua ya maandalizi,au umeanguka kabla hujasimama.

Nenda upitie hoja hizi utafakari na ufanye marejeo kwenye maamuzi yako:-
  1. Ni katika aya ipi Pascal katoa hitimisho kuwa "Bunge linajipendekeza"
  2. Katika mifano aliyoitoa Pascal upi ni wa uongo?
  3. Ni sheria au kanuni ipi inayoruhusu ripoti ya kamati ya Bunge kuwasilishwa kwenye muhimili mwingine?
  4. Hukujua kuwa kwa kuwasilisha ripoti ya kamati ya Bunge kwenye muhimili wa serikali(Rais) ulikuwa ukikiuka kanuni za bunge na kulidharilisha Bunge?
  5. Je Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali nae amelisingizia Bunge kuwa halitekelezi wajibu wake wa kuisimamia serikali?
  6. Ni shetani gani ameliingilia Bunge lako na kuiacha serikali itumie fedha za umma bila kuidhinishwa wala kuleta marejeo ya bajeti? Na Bunge lako likikaa kimya kana kwamba hakuna kinachotokea!
  7. Ndio kwaza unasikia toka kwa mayalla kuwa bunge lako ni butu kuliko bunge lolote katika historia ya Tanzania? Na je mtu kusema ukweli nalo ni kosa? Na hata hivyo unataka kukataa kuwa wabunge wengine wamebaki kutoa huduma za kijamii (kibinadamu)na kuacha majukumu yao ya kimsingi ya kuisimamia serikali na kutunga sheria? Au wewe umelichukuliaje neno "huduma za kibinadamu" Ni mbunge gani hajawahi kufuatwa na wapiga kura wake toka jimboni kwake hadi Dodoma wakihitaji huduma za kibinaadamu(kijamii) ? je Wabunge hawatoi misaada kama ya maziko usafiri na rambirambi kwa wapiga kura wao, vitu kama magari ya wagonjwa,msaada wa karo nk? Si kweli kuwa wabunge hawaishi kulialia bungeni serikali iwatizame kwa jicho la huruma ili wapatiwe maji,hospitali nk, wakati huo huo wakisahau serikali inaendeshwa bila kuzingatia bajeti?
  8. Unadhani wananchi walikuwa usingizini wakati unapewa maelekezo ya kuwakomoa wabunge wenye kihelehele na wenye kidomodomo ndani ya Bunge na kuwa uwatimue na wakija nje muhimili mwenza uwaahughurikie? Unadhani wananchi ni vipofu hawakuona kilichotokea?
  9. Je cheo cha uspika ulicho nacho ni cha kudumu? Kama sio unaenda kuacha nini nyuma yako!
  10. Historia huwa haikosei, niambie toka Bunge la kwanza la Tanzania ni Bunge lipi liliwahi kukumbwa na vituko,ubabe,hatari na visasi kama hili la kwako?
Mwisho nakushauri mheshimiwa Muungwana akivuliwa huchutama,ingawa kuchutama si utamaduni wa serikali ya awamu hii lakini wewe katika hili chutama Pascal hutamuweza,utaadhirika.

Pia soma > Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Pasco Mayalla Yuko Sawa Kabisa!
 
Magufuli alipokuagiza Uwafukuze Wabunge Ili adeal Nao Mitaani Mbona Hukumkataza Kuchezea Bunge? Wabunge wanavyosingiziwa Mashitaka ya Kijinga na Kukamatwa na Polisi kisha Kunyimwa Dhamana na Polisi hata Baada ya Mahakama Kutoa dhamana Mbona hujawaambia Polisi wasichezee Bunge. Tundu Lissu Kapigwa Risasi Huko Bungeni wakati bado akiwa Mahututi, anazungumziwa kwa kebehi na Mlinga na Lusinde mbona Hukuwapeleka Kamati za Maadili? My Friend wewe ni Msukule wa Magufuli, Najua wewe sio Kibaraka Kama Tulia, Lakini Kuna Unachomwogopea Magufuli.
 
hili bunge badala ya kushughulika na hoja za msingi za watanzania linaanza kuziba midomo watu wanaolikosoa mapungufu yake.hili bunge ni mzigo usiobebeka. watoto wa vyuo vikuu wanabaguliwa katika kupewa mikopo lenyewe liko kimya tu.
 
Makala ya Pascal imekidhi vigezo vya ubora isipokuwa pale aliposema wabunge wengine wanaenda kutoa "huduma za kibinadamu". Ni meneno hayo tu, na hapo upo udhalilishaji hasa kwa wabunge wanawake. Kwa sababu huduma za kibinadamu zingefanyika hata kama wasingekuwa wabunge. Kwani sisi tusiokuwa wabunge hatufanyi? Ningemshauri, Ndugu yangu Pascal, hilo aliombee msamaha kuwa kalamu iliteleza na yale yote yatakayosalia akomae nayo ni kweli.
Pole sana, Ndugu yangu.

Acha kufungia fikra zako kwenye chungu mzee!! Huduma za kibinadamu zipo nyingi sana ndugu, we umekaa kuwaza kujamiiana tu kuwa ndo huduma za kibinadamu??! Kuwapa watu msaada wa chakula, rambi2, kusomesha wasiokuwa na uwezo, kuwajali wazee, zote hizi ni huduma za kibinadamu!! Sasa Paskal aombe radhi kwa lipi hapo???!
 
Duuuuu bunch of fool... Haya mambo ya kuongoza watu yanahitaji busara na upeo mkubwa.. Kabla sijasoma comments nilimuona spika yupo sahihi kumbe ni pumba tuuu
 
Yaan spika anaacha kuimarisha uwezo na makali ya mhimili wa bunge anabaki akijipendekeza pendekeza kwa serikali tuu, kazi kujinyea nyea ktk hoja tuu
Ataendeje kwenye matibabu? Ebu fikiria kila baada ya miezi 6 lazima akatibiwe. Kwahiyo fedha za matibabu na huduma zingine atazipataje asipomsujudia Sizonje? Yaani hakuna janga baya hapa Tanzania zaidi ya Job Ndugai!!
 
Aende tu Na yote aliyojiandaa nayo atakutana Na wajuzi wenzie kule hakuna haja ya kuruka ruka hapa jamii forums
Kuna wajuzi bunge ccm? Au unadhani ule upande wenye akili wataunga mkono huu uchizi wa huyo mgonjwa Ndugai?
 
Umefafanua vizuri. Shida ya sisi Wabongo ni kwamba mambo ya ngono tumeyapa kipaumbele kikubwa na hivyo kila kitu tunakiangalia kwa jicho la ngono kwanza kabla ya kufikiria kintu kingine cho chote. Mnakumbuka kauli ya mama Profesa Tiba ya 'kadri tunavyotanua ndivyo ...'. Mama alisema kwa nia nzuri kabisa lakini wabunge wenzake na wabongo nje ya bunge kilichopewa kipaumbele ni kauli hiyo kuvalishwa fikira za kingono. Ngono, ngono, ngono!!!
Hahahaaaa wanaongozwa na mawazo ya Abdalah kichwa wazi. Hoja yako inasdifu kauli moja kwamba wanatumia kile kiungo cha kukalia kufikiri
 
Nchi hii tutaibomoa wenyewe na tutaijenga wenyewe kwa kutetea wanyonge ndio kauli pendwa ambayo haina uhalisia
 
Pascal ujanja wote mfukoni mikononi mwa Pilato.. Na utueleze ni wabunge gani walikuwa wanatoa huduma za kibinadamu bungeni.. hahahah....kama nakuona unavyotetemeka mbele ya kamati teh teh teh
 
We mwanamke, huu ni muda wa kumpikia mumeo, humu unafanya nn?
 
Back
Top Bottom