leonaldo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 2,584
- 3,185
Je Bunge linajipendekeza?
"Naomba nisilijibu swali hili nisije kuitwa mbele ya kamati ya haki,kinga na madaraka ya bunge na kuambiwa nimelikashifu Bunge"
Mwisho wa kunukuu sehemu ya makala inayolalamikiwa.
Mheshimiwa spika kwa heshima na taadhima ningependa kuchukua nafasi hii kukupa ushauri wa bure,licha ya kufahamu kuwa wewe ni nguli wa sheria na ni mbabe lakini katika hili umekurupuka utadharilika mapema na asubuhi.
Nilikusikiliza ulivyokuwa ukitoa povu kuwa bunge ni mhimili na spika sio mtu wa mchezo mchezo na jinsi ulivyokuwa ukimsikitikia pascal kwa kitendo chake cha kuandika makala chonganishi kati ya serikari,wananchi na bunge!
Katika hili mheshimiwa umeshindwa vita kwenye hatua ya maandalizi,au umeanguka kabla hujasimama.
Nenda upitie hoja hizi utafakari na ufanye marejeo kwenye maamuzi yako:-
- Ni katika aya ipi Pascal katoa hitimisho kuwa "Bunge linajipendekeza"
- Katika mifano aliyoitoa Pascal upi ni wa uongo?
- Ni sheria au kanuni ipi inayoruhusu ripoti ya kamati ya Bunge kuwasilishwa kwenye muhimili mwingine?
- Hukujua kuwa kwa kuwasilisha ripoti ya kamati ya Bunge kwenye muhimili wa serikali(Rais) ulikuwa ukikiuka kanuni za bunge na kulidharilisha Bunge?
- Je Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali nae amelisingizia Bunge kuwa halitekelezi wajibu wake wa kuisimamia serikali?
- Ni shetani gani ameliingilia Bunge lako na kuiacha serikali itumie fedha za umma bila kuidhinishwa wala kuleta marejeo ya bajeti? Na Bunge lako likikaa kimya kana kwamba hakuna kinachotokea!
- Ndio kwaza unasikia toka kwa mayalla kuwa bunge lako ni butu kuliko bunge lolote katika historia ya Tanzania? Na je mtu kusema ukweli nalo ni kosa? Na hata hivyo unataka kukataa kuwa wabunge wengine wamebaki kutoa huduma za kijamii (kibinadamu)na kuacha majukumu yao ya kimsingi ya kuisimamia serikali na kutunga sheria? Au wewe umelichukuliaje neno "huduma za kibinadamu" Ni mbunge gani hajawahi kufuatwa na wapiga kura wake toka jimboni kwake hadi Dodoma wakihitaji huduma za kibinaadamu(kijamii) ? je Wabunge hawatoi misaada kama ya maziko usafiri na rambirambi kwa wapiga kura wao, vitu kama magari ya wagonjwa,msaada wa karo nk? Si kweli kuwa wabunge hawaishi kulialia bungeni serikali iwatizame kwa jicho la huruma ili wapatiwe maji,hospitali nk, wakati huo huo wakisahau serikali inaendeshwa bila kuzingatia bajeti?
- Unadhani wananchi walikuwa usingizini wakati unapewa maelekezo ya kuwakomoa wabunge wenye kihelehele na wenye kidomodomo ndani ya Bunge na kuwa uwatimue na wakija nje muhimili mwenza uwaahughurikie? Unadhani wananchi ni vipofu hawakuona kilichotokea?
- Je cheo cha uspika ulicho nacho ni cha kudumu? Kama sio unaenda kuacha nini nyuma yako!
- Historia huwa haikosei, niambie toka Bunge la kwanza la Tanzania ni Bunge lipi liliwahi kukumbwa na vituko,ubabe,hatari na visasi kama hili la kwako?
Pia soma > Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge