Spika Ndugai, Pascal Mayalla alijiandaa. Kasome upya makala,utaadhirika...

Spika Ndugai, Pascal Mayalla alijiandaa. Kasome upya makala,utaadhirika...

Wabunge wanapoomba kura kwa wananchi wanakuwa wapole wako tayari kutoa hata makalio yao wachapwe viboko na wapiga kura wao ili wapate kura.

Wakishapata wanajigeuza miungu watu wasiotaka Udhaifu wao uhojiwe na wapiga kura wao na kusahau kuwa ndio wale waliokuwa tayari kutoa makalio yao kwa wapiga kura wao wachapwe viboko.
Umesahau na kupiga PUSH UP, PUSH DOWN kwenye majukwaa ya kuomba 'kula' 🙄
 
Mtu yeyote asiyekubali kukosolewa daima hawezi kuwa mtu mzuri kwakuwa anajiona kuwa yuko sahihi wakati wote.

Kwa hali bunge la kukutana Dodoma lisitegemee kuwa bunge bora hata siku moja kwa kuwa wakati wote wanajiona wako sahihi katika mambo yote wakati walioko pembeni wanayaona makosa yao na wanapokosolewa wataki kujichunguza ni wapi wanapokosea wakapatengeneza ili wasiweze kukosolewa.
 
Yaani spika kahukumu tayari kabla hata kamati ya maadili haijakaa. Sasa kazi ya kamati ni nini? Na je hiyo kamati ikibaini kuwa mayalla alikuwa sahihi spika atasemaje? Ndugai anaposema spika hachezewi anamaanisha kuchezewaje? Ni kosa la jinai kulituhumu bunge kama linakiuka misingi yake? Maswali ni mengi sana na ndugai ajue kuwa lile bunge ni la wananchi aisdhani ni mali yake na kijifanya kutunisha misuli kwa vitisho hapa.
Kuna muda tunakosa ustaraabu. Haijalishi kama watuhumiwa wana kosa au la. Ni wazi ya kuwa supika "ndie" anaewashitaki kwenye kamati alio iunda yeye mwenyewe. Sasa cha ajabu yeye amezungumza bila chenga kwamba bunge halichezewi na supika wake na huyo Pasikali anajifanya anajua kushinda bunge zima. Kwa maneno hayo na ubabe wa supika je pasikali atatendewa haki? Naona kule ameshahukumiwa anchofuata ni adhabu. Hakuna fairness (haki) kwenye mchakato huu. Mchakato huu tayari umesha anza kujibu lile swali la Pasikalli.
"Wazungu wametengeneza silaha za kuua watu lakini wameshindwa kuja na silaha ya kuua ukweli" Le Grand Poete Lutumba.
 
Ndungai alipoteza sifa za kuwa mbunge tangu siku ile alipomcharaza bakora mgombea mwenzake hata uhalali wa kumuita Mayalla kwenda kumuhoji bungeni sijui anaupata wapi wakati alitakiwa aihoji serekali ni kwanini alipotenda kosa la jinai hakupelekwa jela.
 
Yaani kaongea kama vile ana ugomvi binafsi na Mayalla. Maneno yale tu yameshaharibu dhana nzima ya kumuita mbele ya kamati kwasababu tayari spika ameshamhukumu kuwa ni mkosaji. Hata Zitto alimtishia hivi hivi nadhani huyu spika anashida sana na Mass communication skills anaongea utadhani yupo kwenye ugomvi kwenye kilabu cha pombe
Mkuu kwani hukumbuki alivyomcharaza mwenzake bakora kipindi kile cha kampeni? Ana jazba sana huyu supika. Yaani nimemcheki anavyotoka povu nikasema hiiiiiiiiiii!!!
 
Back
Top Bottom