Spika Ndugai ndio chanzo cha uozo katika Serikali hii

Habari!

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya spika Ndugai ndilo lililopitisha sheria kandamizi nyingi zaidi kuliko kipindi cha maspika wengine wote.

Serikali (Rais) kazi yake ni kutawala, na katika kutawala kuna mahali panahitajika mkono wa chuma(maumivu) na kuna mahali hapahitaji mkono wa chuma.

Sasa bunge kazi yake ni kuutuliza mkono wa serikali usilete maumivu kwa Wananchi.

Sasa inatika wakati spika Ndugai anawaambia wabunge wapitishe sheria na wasipopitisha bunge litavunjwa. Na kwakuwa wabunge wetu njia walizoingilia bungeni wanazijua wenyewe basi wakisikia kuhusu kuvunjwa bunge wanaufyata.

Kwahiyo adui nambari moja wa Wananchi ni Spika Ndugai na si Rais Samia Suluhu.
Ndugu USIDANGANYIKE,
Spika hawezi kufanikiwa katika UOVU bila ya support ya Rais.
Wale wote ni wamoja katika uovu na ukandamizaji wa haki dhidi ya waTz.
 
... wangepewa titles mpya tu tujue moja - His Royal Highness Prince Job Ndugai; Her Royal Highness Princess Dr. Tulia Ackson Mwang'onda. Ni katika familia za kifalme ukiacha His/Her Majesty, Crown Prince na Crown Princess ndio ambao hawashtakiwi kokote. Bila Katiba Mpya na Bora hatuchomoki kwenye makucha ya hawa watu!
Ndiyo maana ukitaka kufahamu rangi zao waambie tunataka Katiba Mpya! Wataweweseka na kukosa hoja,Mara Watanzania wanataka Maji,elimu,sijui afya nk.
Swali;Katika nchi hii yenye kila aina ya raslimali inakuwaje tukawa hatuna Maji,vituo vya afya na elimu bora hadi leo?Nchi hii ilivyokuwa ya amani kwa miaka yote 60 inashindwa na Rwanda,Uganda au Kenya kimaendeleo.
CCM acheni mzaha,tunataka Katiba yetu tuisuke upya nchi yetu maana imewashinda,full stop.
 
Hayo sio matatizo ya ndugai au spika ila ni tatizo la kikatiba.
Katiba tuliyonayo ya 1977 inampa nguvu kubwa Raisi kuwa yeye ndio supreme leader/kiongozi mkuu hivyo anakua na mamlaka ktk mihimili yote ya serikali(mahakama, bunge na dola) mfano katika bunge Raisi ni sehemu ya bunge kwa hiyo bunge haliwezi kumuwajibisha Raisi,
Raisi ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri ambao ni wabunge hivyo kiutendaji bunge linashindwa kumuwajibisha waziri anapokosea au akileta sheria inayowakandamiza wananchi kutokana na mgongano wa maslahi kati ya bunge na dola kwaiyo ile dhana ya mgawanyo huru wa madaraka kati ya mihimili ya serikali inakua haifanyi kazi ndio maana unaona wabunge wetu wanageuka kuitetea serikali na sio wananchi mfano kwenye suala la tozo na Kodi kandamizi kwa wananchi tunaona wabunge wapo na serikali ila sio wapiga kura wao
Kwahivyo inatakiwa kutolewa elimu ya uraia kwa wananchi wote kuhusu umuhimu wa katiba mpya itakayorudisha mamlaka,wajibu,haki na madaraka kwa wananchi na sio kikundi kidongo Cha watu(serikali)
 
Back
Top Bottom