Therefore Professor is like a dog?Matusi kwa Professor ni sawa ila udhaifu wa Bunge Ni kosa la jinai.Hii imekaaje wadau?Spika wa Bunge Job Ndugai, leo Aprili 14 atazungumza na waandishi wa habari jambo muhimu kuhusu bunge.
Mazungumzo hayo yatafanyika katika ofisi ndogo ya bunge jijini Dar es salaam majira ya saa sita na nusu mchana.
=====
UPDATES:
View attachment 1071319
=> Spika Ndugai: CAG anaposema mbele ya umma kuwa ataendelea kutuita 'dhaifu' wakati ni jina ambalo hatulipendi na tumelikataa, tunashindwa kumuelewa kama analipenda sana ajiite yeye. Sasa kusema unaendelea kutumia endelea na nitakuita tena na safari hii itakuwa mbaya zaidi"
=> Spika Ndugai: "Namwambia ndugu yangu Prof. Assad hilo neno aliache, sisi taarifa tumeipata na tutaifanyia kazi. Msisitizo wetu ni mmoja, kwakuwa bunge lilishapitisha uamuzi wa kutofanya kazi na Prof. Assad ni uamuzi halali"
=> Spika Ndugai: "Sina chuki binafsi na Prof. Assad, yule ni ndugu yangu na ni mtanzania mwenzangu tatizo ni lugha anayoitumia na nisinhependa itufikishe hapa kama taifa."
=> Spika Ndugai: "Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au laaa!. Maana tushamwambia hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais
=> Spika Ndugai: Zipo njia za kumaliza mambo kama haya, mojawapo aende kwa Rais akajieleze kwamba mimi nimepima nimeona nimekosea hapa na pale. Maana Rais ni sehemu yetu sisi (Bunge) hatuwezi kupitisha sheria bila yeye kupitisha mkono wake,
=> Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amewahakikishia watanzania kuwa bunge linaendelea vizuri na kazi yake ya kutunga sheria, uwakilishi, kuisimamia Serikali pamoja na mipango ya nchi ikiwemo suala la bajeti ambalo linaendelea bungeni.
=> Spika Ndugai:“Sasa kumekuwa na ufafanuzi usiokuwa sawa sawa, kilichowekwa mezani ni ‘Audit Queries’ …kilichowekwa mezani sio ukweli wenyewe kwamba aliyetajwa mule sasa huyo mwizi… ‘Audit queries’ zile zikishawekwa mezani kazi yetu ni kuwaita mezani na kuwasikiliza
=> Spika Ndugai:Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au la! maana tushamwambia hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais
=> Spika Ndugai:Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Profesa Mussa Juma Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.
=> Spika Ndugai:Sisi kama Bunge hatutaki hilo neno dhaifu, kwa sababu Bunge kama Bunge halifanyiwi tathmini na ofisi ya CAG ila wanaofanyiwa tathmini ni watendaji wa Ofisi hiyo hivyo hawakupaswa kudhihakiwa na lugha hiyo inayotajwa kuwa ya kihasibu.
=> Spika Ndugai: “Hata katika maisha ya kawaida, we unamuita mtu jina flani, anakwambia bwana tafadhali jina hili silipendi, lakini unaendelea kumuita na kuahidi utaendelea kulitumia, ni ustaarabu duniani?”
=> Spika Ndugai: “Katika kutekeleza majukumu yake #CAG hakupaswa na hapaswi kulitukana #Bunge kwa lugha zile za rejareja. Bunge huangalia taratibu zake na kuendesha mambo yake kufuatana na kanuni za Bunge…lile Bunge lenyewe hawezi kulikagua”
=> Spika Ndugai: Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Profesa Mussa Juma Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.
=> Spika Ndugai: “Sasa kumekuwa na ufafanuzi usiokuwa sawa sawa, kilichowekwa mezani ni ‘Audit Queries’ …kilichowekwa mezani sio ukweli wenyewe kwamba aliyetajwa mule sasa huyo mwizi… ‘Audit queries’ zile zikishawekwa mezani kazi yetu ni kuwaita mezani na kuwasikiliza”
"Nilipokuwa sipo kuna mambo mengi yamezungumzwa, na mengine yameandikwa kuhusu Ripoti ya CAG. Nitakapokuwa Dodoma nitaagiza ripoti ipelekwe kwenye kamati za PAC na LAC"
Zaidi soma.....
Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad akamwone Rais John Magufuli ili mzozo wake na Bunge uishe.
Kauli ya Spika inakuja wakati tayari Bunge limeshapitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad bali ofisi ya CAG.
Spika Ndugai aliyekuwa ziarani nchini Sweden wiki iliyopita ameyasema hayo leo Jumapili Aprili 14, 2019 akieleza kusikitishwa na hatua ya Profesa Assad kurudia neno udhaifu kwa Bunge alipotoa taarifa yake hivi karibuni.
"Zipo njia za kumaliza mambo kama haya, mojawapo aende kwa Rais akajieleze kwamba mimi nimepima nimeona nimekosea hapa na pale. Maana Rais ni sehemu yetu sisi (Bunge) hatuwezi kupitisha sheria bila yeye kupitisha mkono wake," alisema Ndugai.
Ameongeza kuwa hata bajeti inayojadiliwa na Bunge lazima ipitishwe na Rais. Amesema kwa kuwa Bunge limeshapitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Mussa Assad alitakiwa ajiuzulu.
"Kwa kuwa Bunge likishaaamua kuwa halifanyi kazi na mtu, ni uamuzi halali. Katika nchi zote Bunge likishakosa imani na wewe unajiuzulu," amesema.
Ameongeza, "Sasa hatumfundishi kazi Mussa Assad, anampa wakati mgumu Rais tu. Tutafanya kazi na ofisi ya wananchi."
Spika Ndugai amemsifu Profesa Assad kwa ujasiri wake huku akiufananisha na ujasiri wa mbwa kumtukana mtu anayemlisha.
"Unatukana hadi mkono unaokulisha, inahitaji ujasiri na jamaa ana ujasiri. Ila ni ujasiri ule wa mbwa anayemtukana anayemlisha," amesema.
Hata hivyo, Ndugai amesema hana chuki binafsi na Assad bali tatizo ni lugha tu aliyotumia ya kuliita Bunge dhaifu.