Spika Job Ndugai: Kutokana na masharti ya Mradi wa Bandari Bagamoyo, ni sahihi Serikali kuusitisha

Bado kidogo tuingie kwenye kundi la watu wasiyo kopesheka
Wananchi tunaolipa kodi tunaaswa tuwe wakweli lakini wanasiasa wanaolipwa kwa kodi zetu wanakuwa vigeugeu! Nina mashaka kama kwa njia hizi deni la taifa halitafika trillion 100 mwakani!
 
Sikubaliani ujenzi wa bandari hapo bagamoyo na pia simuamini anachosema jiwe sababu alishatulisha matango pori kwenye makinikia..nikiusoma mkataba nitatoa maoni kuhusu huo mkataba
 
Hii tabia ya kuacha kusoma masharti yaliyopo kwenye mikataba ndio imeifikisha nchi hapa ilipo kwa sababu mingi ya mikataba hiyo ni mibovu na ndio maana wananchi kupitia wabunge wetu tumeomba miaka nenda rudi mikataba yote iletwe bungeni ipitiwe kabla ya kusainiwa.

Leo hii kama sio umahiri wa Mh. JPM huu mkataba mbovu nao ungesainiwa na kuliingiza taifa kwenye umasikini wa kutupwa.

Nionavyo mimi kanuni ya adhabu kutokana na kosa la kuliingizia taifa hasara yaani uhujumu uchumi ipitiwe upya ili ikibainika wahusika wawajibishwe bila huruma hata ikibidi wafilisiwe na kufungwa muda mrefu.

Nakumbuka wakati fulani nilikuwa nasafiri kwenye ndege nikitokea Amsterdam kuja Dar kuna mzungu mmoja alikuwa kiti cha pembeni yangu alikuwa akisoma mkataba baina ya kampuni yake na serikali ya TZ,cha kushangaza hakulala usiku kucha alikuwa anaupitia kisawasawa kitu ambacho sidhani kama watanzania tunafanya hivyo.

Mungu mbariki JPM Mungu ibariki TZ.
Aliyekwambia mkataba haujasainiwa ni nani? Tofauti yako na Ndugai ni nyadhifa tu lakini wewe ni Ndugai2. Huyo unayemsifu alisaini kwenye baraza la Mawaziria(acc. Anna Abdalla) anajikosha kama mgeni vile.
 
Ko nikwamba nchi yoye na mihimili uake yote aliyeona ubovu wa mkataba tajwa ni magufuri tu
 
Mimi wenda mngenisaidia kitu kimoja kwanza; njia za kuandaa mkataba mpaka inafikia hatua ya kuridhiwa na pande zote yaani serikali ya Tanzania na serikali ya Uchina; je wataalam wa TPA hawausishwi? Katibu mkuu na mawaziri wa wizara ya Ujenzi JPM sijui ni Uchukuzi wakati Mwakyembe hawausishwi?

Tusije tukawa tunalishwa maneno kumbe sign zao zipo kwenye mkataba.
 
Faida gani alizoangalia wakati tayari tuna bandari kubwa 3 yaani Dsm, Tanga na Mtwara?

Spika unaongeaje bila utafiti wala data?!!!
ni wewe kweli au kuna MTU umemwazima Simu yako? Sikuelewi siku hizi kwa jinsi unavyozibadili gia angani!
Kwani imekuwaje unawachapa fimbo jamaa zako?
 
Spika ambaye alisema mradi una manufaa makubwa leo anasema hajui mkataba ulikuwaje,ilikuaje akimbilie manufaa bila kujua mkataba ukoje,ndio watu tunategemea watupeleke uchumi wa kati,kila Siku wanapitisha mikataba wao wenyewe halafu baadae wanaanza kushaangaa,Kisa kasikia Raisi kaukosoa sasa anajua hawezi kusimama kinyume
Hii inaonesha kutokuwa na msimamo katika kile unachokiamini. Unakuwa kama bendera tu kufuata upepo unapoelekea.
 
Ile presentation ilionyesha vitu gani? Na je, hadi hapo hakuwa amepata abc za mkataba? Ok ukiwa unaenda mahali ukapitiliza hiyo sehemu ni kawaida kupiga U turn. A finger could have been pointed to him and forced the U turn
Ko nikwamba nchi yoye na mihimili uake yote aliyeona ubovu wa mkataba tajwa ni magufuri tu
 
Huyo ni zuzu wacha naye maana bila kuwataja wapinzani hawezi kupata posho ya buku 7
Serikali ya Muungano wa CHADEMA na ACT ndiyo iliyoingia mkataba huu! Ni bora uwe unamuuliza mkeo kabla hujakomenti.
 
Vichekesho, kama spika hakuyajua sie wa nanjilinji jee. Hii movie sijui nani mkweli.
 
Mgogo siku zote ni mtu asiye na msimamo kwenye maisha yake kuna siku nikiwa sehemu fulani ugogoni tulikubaliana na jamaa zangu wa kigogo tumpigie kula jamaa mmoja ambaye tulikuwa tunamuunga mkono kwenye uchaguzi ule tukiwa kwenye foleni ya kupiga kula jamaa walibadili msimamo wakati tulikubaliana mwezi mzima kabla ya uchaguzi nikasiki CHISIMSAKA YUNJI
 
Back
Top Bottom