Speed ya Prof. Tibaijuka yaanza kupata vikinza

Mahakama ndio muamuzi wa mwisho.

Kama alipewa umiliki kwa amri ya mahakama, hakuna anayeweza kubatilisha isipokuwa mahakahama ya juu zaidi

Matumizi ya kiwanja yalibadilishwa na Rais Mkapa, na kubakia eneo la wazi.
 
mimi sijaelewa vizuri maelezo ya muccadam! Kuna mahali amesema kuwa kiwanja hicho kilibinafishwa kwa miaka 99! Sasa imekuwaje kiwe mikoni mwake au miaka hiyo 99 imeshakwisha au alikipata ndani ya huo huo mlolongo wa miaka hiyo 99?!

Naomba kueleweshwa vizuri hapo.

hujaelewa au hujasoma vizuri rudia tena acha matapishi
 
Huy jamaa alikuwa na kesi na wakili Sinare ambae sasa nadhani yupo kwenye uongozi, sijui nani alishinda kesi ile, ilikuwa hii ya mambo ya viwanja.

Jee, Tibaijuka ataomba msamaha au Mucadam kakanyaga mawaya?

Yetu macho.
 
tatizo huyu mama yeye kwake anadhani kazi ya uwaziri alopewa ni ku deal na open spaces tu...yaani sidhani kama ana vision ya kutosha

Man, your argument is too poor, not worthy of any great thinker, unaposema" kudeal na open spaces tu" unataka kumaanisha hakuna shughuli nyingine inayofanyika na wizara zaidi ya hiyo? Au labda kwamba open space siyo area of competence ya wizara yake? Jaribu pia kunieleza una maanisha nini unaposema hudhani kama ana vision ya kutosha. Rudi kwenye tatizo na uliangalie kisheria (kama unaweza) na ulijadili kisheria ambapo kweli inawezekana akawa amekosea au kukawa na ukweli wa kile alichokisema, kama hili suala litafikishwa mahakamani ukweli utajulikana kwa taratibu za kisheria. Mwisho, si sahihi kwako kuishusha vile vision ya Tibaijuka, unaweza usikubaliane na mtazamo wake, au na nafsi yake (kwa chuki binafsi) ila vision yake ni kubwa sana.
 
Prof Anna Tibaijuka naona kawekwa kikaaangoni tayari.......Binafsi naona hakufanya due diligence ya kutosha!! Naona hapa atakuwa kapigwa brake kufuatilia viwanja vingine vya wazi....nchi hii ukiwa na hela uko juu ya sheria. Kitakachofanyika sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya ardhi kumweka chini mama Tibaijuka na kumwelezea the rules of the game. Baada ya hapo mama atarudi kwenye business as usual ya serikali ya Kikwete!
 
Matumizi ya kiwanja yalibadilishwa na Rais Mkapa, na kubakia eneo la wazi.

President akishabatilisha umiliki wa kiwanja hakuna Mahakama inaweza kutengua uamuzi huo. President Mkapa alishabatilisha umiliki huo na kiwanja hicho kuendelea kuwa eneo la wazi kwa mujibu wa Ramani za mji wa Dar es Salaam. Hukumu ya Jaji Mama Chingwile iliyompa ushindi Muccadam ina walakini. Jaji alipashwa kujua Mipaka na Mamlaka ya Mahakama vs President. Lakini hao ndio Majaji wa Mkwere. Eti anatafuta sifa kuwa wanawake wanaweza. Ndiyo wanawake wanaweza wale wenye sifa si kila mwanamke kama ilivyokuwa kwa waanume. Yaani si kila mwanamme anaweza kwa maana ya kuwa jinsi ya Kiume. Inatakiwa sifa za kitaaluma na si jinsia yake.
 
Huy jamaa alikuwa na kesi na wakili Sinare ambae sasa nadhani yupo kwenye uongozi, sijui nani alishinda kesi ile, ilikuwa hii ya mambo ya viwanja.

Jee, Tibaijuka ataomba msamaha au Mucadam kakanyaga mawaya?

Yetu macho.

Prof.Tibaijuka hajakurupuka na haitaji kumuomba Muccadam msamaha. Muccadam kama walivyo akina jitu patel ni washirika wa genge moja la Matapeli. Hapa amekamatwa pabaya. Hayo ni mateke ya farasi anayekaribia kifo. Kumbuka Anna anafanyakazi na Katibu Mkuu Rutabanzibwa. Wote ni watu makini nawaamini. Sasa kazi imeanza. Tuwaunge mkono kwa kuwapelekea taarifa Muhimu.
 
President akishabatilisha umiliki wa kiwanja hakuna Mahakama inaweza kutengua uamuzi huo. President Mkapa alishabatilisha umiliki huo na kiwanja hicho kuendelea kuwa eneo la wazi kwa mujibu wa Ramani za mji wa Dar es Salaam. Hukumu ya Jaji Mama Chingwile iliyompa ushindi Muccadam ina walakini. Jaji alipashwa kujua Mipaka na Mamlaka ya Mahakama vs President. Lakini hao ndio Majaji wa Mkwere. Eti anatafuta sifa kuwa wanawake wanaweza. Ndiyo wanawake wanaweza wale wenye sifa si kila mwanamke kama ilivyokuwa kwa waanume. Yaani si kila mwanamme anaweza kwa maana ya kuwa jinsi ya Kiume. Inatakiwa sifa za kitaaluma na si jinsia yake.

Kwa nini awe Jaji wa "Mkwere" wakati hukumu ilitolewa mwaka 2000! Mijitu mingine bwana hata haya haioni. Kama chuki, basi mtazame wapi pa kuziweka. Hukumu ilitolewa wakati wa Mkapa.
 
Nani kakudanganya kaka mbele ya pesa?mama kuwa mwangalifu tu hawa watu hawafai hatakidogo,

Ona hii....."The Minister of Lands, Housing and Human Settlement Prof Anna Tibaijuka has ordered all people illegally occupying open spaces to surrender them before what she termed ‘land ranger operation' starts. The Minister insisted that she was going to use existing laws to ensure that land problems were dealt with clearly, while warning people against using financial muscle to grab public open spaces."I will follow and respect the rule of law and not otherwise in dealing with issues falling under my ministry. I will never tolerate any person using money to occupy an open space," she stressed." Chanzo Prof. Tibaijuka serves notice on open spaces | Mrs Anna Kajumulo Tibaijuka
 
Kwa nini awe Jaji wa "Mkwere" wakati hukumu ilitolewa mwaka 2000! Mijitu mingine bwana hata haya haioni. Kama chuki, basi mtazame wapi pa kuziweka. Hukumu ilitolewa wakati wa Mkapa.
Ebu rejea post hapo juu uelewe nini nasema. Kwa rejea yako soma hii hapa.

........Aliendelea kueleza kuwa mwaka 2000, kiwanja hicho kilifutwa kwa makosa na suala hilo likapelekwa Mahakama Kuu na kufunguliwa kesi namba 70/2004.
Baadaye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilipendekeza mgogoro huo umalizwe nje ya mahakama.
Aliendelea kueleza kuwa wizara na Manispaa ya Ilala vilishindwa kutekeleza makubaliano hayo hivyo ilimlazimu kufungua kesi nyingine Mahakama Kuu namba 107/2006."

Hii ndiyo kesi ambayo Jaji Chingwile aliitolea Hukumu Mwaka huu. Kama utakumbuka Muccadam alianza ujenzi hapo Palm beach siku ya Ijumaa tarehe 29/10/2010 akijua watu watakuwa week end na jumapili kwenye uchaguzi. Kama alikuwa anajiamini kwa nini aanze ujenzi kwenye odd dates and days?
 
Prof.Tibaijuka hajakurupuka na haitaji kumuomba Muccadam msamaha. Muccadam kama walivyo akina jitu patel ni washirika wa genge moja la Matapeli. Hapa amekamatwa pabaya. Hayo ni mateke ya farasi anayekaribia kifo. Kumbuka Anna anafanyakazi na Katibu Mkuu Rutabanzibwa. Wote ni watu makini nawaamini. Sasa kazi imeanza. Tuwaunge mkono kwa kuwapelekea taarifa Muhimu.

Naomba iwe hivyo kwani huyo jamaa hata akitembea utafikiri aneelea kwa mikogo. Huwa anatamba kuwa hajawahi kushindwa kesi hata moja na ni tapeli wa kutupa. Hicho kiwanja kikichunguzwa sana utakuta hata hao wamiliki wa awali hawajamuuzia bali katapeli,

Mama Tibaijuka anzia kuchunguza kama kweli aliuziwa hicho kiwanja au aliwatapeli hao wahindi na pengine wameshakufa kabla ya huo mwaka aliosema kauziwa, kwani babake alikuwa wakili, inawezekana kapitia mafaili yaliyopo kwa babake akakuta opportunity, watu washakufa ndio akaanza umafia wake wa kubadili jina. Na mama ukikuta hiyo, si forgery hiyo? Umlundike ndani aoze hukohuko, maana hafai kabisa huyu fisadi pamoja na wenzake wanaoifasadi hii nchi kwa kupora viwanja vya wazi ambavyo kila mTanzania ana haki navyo.

Huyo kijana ni Tapeli tena Fisadi wa hali ya juu.
 
Personally I think the Hon.Professor will sooner than later realise that it's next to imposible to straighten up things in a corrupt system. She will have either tow the line or else the sooner she quites the better for her.
 
Development ya ardhi inatikiwa kufanywa ndani ya miaka miwili, Hivyo bas1 Tibajuka anaweza kutumia kipengere hicho kulinda eneo hilo!
 
Mods hii kwa nini haoiunganishwi na ile ya tibaijuka kupewa siku 7. Its one and the same
 
Hakimu anaruhusiwa kutengua maamuzi ya Rais! Mmmliki halijui hili? Tutaendelea mpaka lini kuendekeza matumizi ya pesa katika uporaji wa mali za Wtz? Na wengine comment zenu kama mmeshikishwa vile!
 
Hmmmmm! Kazi kweli kweli!

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Mmiliki Palm Beach ampa Tibaijuka siku saba
Thursday, 16 December 2010 20:51

Nora Damian
Mwananchi
BADALA ya kuendelea na mkakati wake wa kupambana na watu waliojenga klwenye maeneo ya wazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka atalazimika kutumia siku saba kutafakari barua ya mmiliki wa moja ya viwanja hivyo anayetaka aombwe radhi ndani ya muda huo kwa madai kuwa amechafuliwa.

Mmiliki huyo wa kiwanja hicho kilicho karibu na Hoteli ya Palm Beach jijini Dar es Salaam, Taher Muccadam pia ametishia kwenda mahakamani kudai fidia ya Sh2 bilioni iwapo Prof Tibaijuka, hatamuomba radhi.

Kiwanja hicho ni moja ya viwanja kadhaa ambavyo Prof Tibaijuka alisema ni vya serikali lakini wajanja wakavichukua kwa kutumia kisingizio cha viwanja vya wazi na hivyo kutaka virejeshwe serikalini.

Tibaijuka, ambaye aliambatana na katibu mkuu wa wizara wakati wa kukagua viwanja hivyo vilivyo ufukweni mwa Bahari ya Hindi, pia alitoa historia ya kila kiwanja hadi kilipovamiwa na kuwekwa majengo mapya.
Lakini Muccadam alifanya mkutano na waandishi wa habari jana na kuwaeleza kuwa maelezo ya Tibaijuka, ambaye alikuwa mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UNHABITAT), alimvunjia heshima mbele ya jamii na sasa anataka aombwe radhi ndani ya siku saba.

Notisi hiyo ya siku saba iliyotolewa jana na wakili wa kampuni ya Decoram attoneys imeeleza kuwa Waziri Tibaijuka alimvunjia heshima mmiliki huyo kwa kutamka kuwa alitoa rushwa ili kukipata kiwanja hicho.
“Amenivunjia heshima ndani na nje ya nchi na mimi nikiwa kama mwanasheria, nimeumia sana. Naamini sheria ni msumeno na inaweza kutoa haki kwa mtu yeyote,” alisema Muccadam katika notisi yake hiyo.
Muccadam alieleza kuwa alipata kiwanja hicho kihalali kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu baada ya pande zote mbili kufika mahakamani hapo na kuafikiana.

“Hii inaonyesha dhahiri kwamba wizara imekula matapishi yake kwani ndiyo iliyotoa vibali vyote halali, vikiwemo vya kubadilisha ramani na kupima tangu mwaka 1975,” alisema Muccadam.
Katika notisi hiyo Muccadam ameeleza kuwa kama waziri huyo hataomba msamaha katika muda huo aliompa, atamfikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Kiwanja hicho namba 1006 kilicho Upanga jirani na Hoteli ya Palm Beach ni kati ya viwanja ambavyo Profesa Tibaijuka alisema kuwa ni vya wazi na kwamba haviruhusiwi kuwa makazi.
Kwa mujibu wa Muccadam, kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa kwa hati namba 186164/25 iliyotolewa Januari Mosi mwaka 1975 kwa wamiliki wa kwanza ambao ni Shantaben Narottambahi Patel na Nilaben Girishumar Patel.
Alisema kiwanja hicho kilimilikishwa na Manispaa ya Ilala na miliki hiyo ilidumu kwa miaka 99 kabla yeye hajakinunua mwaka 2000.

Aliendelea kueleza kuwa mwaka 2000, kiwanja hicho kilifutwa kwa makosa na suala hilo likapelekwa Mahakama Kuu na kufunguliwa kesi namba 70/2004.
Baadaye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilipendekeza mgogoro huo umalizwe nje ya mahakama.
Aliendelea kueleza kuwa wizara na Manispaa ya Ilala vilishindwa kutekeleza makubaliano hayo hivyo ilimlazimu kufungua kesi nyingine Mahakama Kuu namba 107/2006.

"Niliendelea na malumbano hayo Mahakama Kuu kwa muda wote huo na hatimaye nilishinda kesi na kurudishiwa kiwanja hicho na kwamba, mahakama ilikubali nilipwe fidia ya dola 6 milioni za Kimarekani kama gharama za ujenzi huo," alisema Muccadam.

Muccadam alieleza kuwa alinunua kiwanja hicho ili ajenge jengo la ghorofa 22, lakini tangu wakati huo ameshindwa kuanza ujenzi kutokana na kuwepo kesi mbalimbali mahakamani.

 
huyu muccadam amejenga ukuta siku ya 31/10/2010 na ukuta wote ukaisha kwa siku moja, huu ukuta ni mkubwa na wafanyakazi walikuwa wengi balaa. wakati waut wanapiga kura yeye anajenga ukuta harakaharaka

mama tibaijuka hajakurupuka anajua kinachoendelea
 
Back
Top Bottom