Prof. Tibaijuka: Kuna ukiritimba kwenye uchuuzi wa mafuta nchini

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Aliyewahi kuwa Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka ambaye ni mtaalamu wa Uchumi na masuala ya mipango miji amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na ukilitimba wa umiliki wa vituo vya mafuta nchini.

Akizungumza na Radio One Stereo January 24, 2024 amesema kuna watu wachache wanamiliki vituo vya mafuta karibia kila sehemu nchini, amesema kuwa hilo sio jambo baya lakini amedai kuwa inaweza kuwa kikwazo kwa watu ambao Serikali imekuwa ikitaka kujiajiri kushindwa kupiga hatua kutokana na ukiritimba huo.

Amesema kuwa ni muhimu jamii ikafahamu kuwa biashara ya mafuta nchini sio uwekezaji bali ni uchuuzi.

Prof. Tibaijuka ameongeza kuwa ipo changamoto nyingine inayotokana na vituo vya mafuta kujengwa bila kuzingatia mipango miji.

Ikumbukwe hivi karibuni baadhi ya wadau ndani ya JamiiForums wameripoti madai ya vituo vingi vya mafuta kujengwa kwenye maeneo yasiyo rasmi ikiwemo karibu na makazi ya watu hali ambayo imekuwa ikiibua mijadala inayohoji juu ya uwajibikaji kwa mamlaka zinazotoa vibali.
 
Uchuuzi unanunua huku unapeleka pale sehemu nyingine yenye uhitaji wa hiyo bidhaa kwa kuongeza bei kidogo ya bidhaa kutoka kwenye ile ya manunuzi.
 
Mtaalam wa mipango miji

Wakat kwko kwenye mipango miji

Ipo ovyo ovyo

Ova
 
Ila si alikuwa na nafasi ya kuyasemea hayo akiwa Kiongozi?

Why now?
Bila shaka aliyaaema.
Huko akiyasema hayaletwi hadharani.
Lakini sasa ni raia anayasemea uraiani, hana kosa.

Kumbuka alimshauri Kikwete Ofisi za mwendokasi zisijengwe jangwani hakusikilizwa pia
 
Back
Top Bottom