Jamani hebu tujadili haya mambo kitaalamu sasa, naona tunabishana tuu na tuna weka kando fact
Swala speed linategemea mambo makuu mawili
Speed anayotoa Service provider wako, na hapa kuna mambo kadhaa ndani yake
Teknolojia inayotumika - EDGE/GPRS, 3G/3.7G/UMTS
Aina ya Bundle, kuna bundle zinabanwa speed na zingine zinaachiwa katika maximum speed inayotolewa na SP
Location uliyopo - unakama signal gani? EDGE au 3G nk
Aina ya modem unayotumia-Modem zinatofautiana upitishaji wa speed kuna za 1MPS hadi 21 Mps
Kuna factors zingine ndogo ndogo kama updates kwa windows yako, uwezo wa pc yako, settings za pc yako na browser yako, mfano utumiaji wa pronx nk
Sasa ili kupata speed unayotajwa hapa ni lazima uzingaatie vigezo hapo juu
Ni ndoto kwako kupata speed nzuri kama unatumia signal za EDGE
Ni ndito kwako kupata speed ya zaidi ya 500KBps kama unatumia modem yenye uwezo wa chini ya 3MBP
Nindoto kwako kupata speed nzuri kama unatumia kifurushi kinachotoa speed ndogo nk nk
Sasa wataalamu watusaidie
Je Airtel kwa minara ya 3g na 3.7g wanatoa speed gani na minara ya edge inauwezo wa speed gani
Je vifurushi vya Aitel vimekaaje kwa upande wa speed, limit yake kwa kila kifurushi
Je kila modem zina uwezo gani kupitisha speed nk nk
Mimi binafsi natumia modem ya vodafone k3570-z yenye uwezo wa kupitisha speed ya 3.6Mbps
Nimeset Join Air dash board ikamete 3G only
Speed ninayopata inacheza 200KBps to 500KBps sizidi hapo kwasababu modem yangu uwezo wake umekomea hapo
But most of time speed yangu ni 200-300KB ps
Facts
Nakamata 3G muda wote
Kifurushi changu hakijabanwa speed
Kama mimi naweza kukamata 500KBps nikiwa na modem inayonilimit 3.6MBps je mwenye modem ya 7MBps kama speed inaruhusu si anaweza kukamata zaidi ya 500KBps?