This is business baanaa! kampun haiwezikufanya biashara ya dini, sikuzote wanataka kunyang'anya chochote wanacho weza kupata kutoka kwa watumiaji. Kiukweli speed ya internet hutegema vitu kadhaa, kwanza location, kama unaishi kwenye miti mingi au mabonden ni ukweli usio pingika RCP level itakua mbaya na hata speed itakua si yakuridhisha sana.
Pia kama kama unaishi eneo lenye mnara moja uliokaribu na watumiaji wengi pia speed lazima ipungue kwakua bandwidth hua haiongezeki kwenye mnara kadri watumiaji wanapo ongezeka katika eneo hilo, pia jinsi ya uungaji hivyo vifurushi, usitegemee upate speed nzuri wakati umeweka unlimited ya mwezi, kwahali yakawaida kampuni ingekua imeshafirisika kama ingeruhusu hiyo speed, wanaruhusu vifurushi vidogo ili uweke mara kwa mara ufaidishe kampun.
Alafu sio mahala wanafunga mitambo ya 3G ni gharama sana na hasa kama gharama zao hazita rudi mapema katika eneo hilo. Me hua natumia kifurushi cha siku cha airtel kwaajili kubrowse tu, speed yake ni kichekesho sana lakini ndio biashara lipia kadiri utumiavyo, lakini ni fair kidogo tofauti na zamani tulipokua tunapanga mistari kwenye cafe!