Zungumza mambo ya kuelimisha watu yaani an independent analysis kuhusu mwenendo mzima wa vita unavyo kuwa conducted pamoja na maoni yako baada ya kupitia sources ambazo ni very
reliable na sio tabloid paper sources hicho ndicho kinacho takikana ili watu wapewe habari/taarifa za kuaminika, kwa bahati mbaya naona mwenzetu badala yake unakimbilia ku-manufacture "tirades" tuuu zisizo kuwa na mantiki hata kidogo - mara ooh Warusi wa Buza,mara ooh Warusi wa Magomeni - mambo ya kitoto toto tu na ku-copy copy na ku-paste kutoka kwenye highly questionable sources, mnashindwa hata kutofautisha between CGI generated video clips and digitally manipulated photos, nyinyi mnadhani vyote hivyo ni real stuff, halafu mnakwenda mbali zaidi mnazijengea hoja, just emulating Zelensky Military propaganda to the letter!!
To drive point home, kuna sehemu nilicommet kwamba si rahisi jeshi la Zelensky likazingira jeshi la Urusi wakati Urusi ina miliki formidable Air force, badala ya kuni hoji na maanisha nini naona mwenzetu badala yake unasema haiwezekani, mbona Urusi imeshindwa kumiliki anga la Ukraine - unacho sahau ni kwamba Urusi amekwisha haribu takribani asili mia 85% za Airforce ya Ukraine, hivi sasa Russia ina uwezo wa kufanya lolote kwenye anga la Ukraine by flying their fighter planes and bombers at higher altitude ili kukwepa shoulder fired MANPAD,kitu kinginev Russia haitumii airforce sana nchini Ukraine anaziweka/park kwenye hangar ili zije kutumika kama NATO/USA watahamua ku-attack Russia whether by accident au delibarately - ndio maana Russia haitumii sana ndege zake kwenye vita ya Ukraine badala yake anatumia:
1) Missiles.
2)Artillery.
3) MRLS.
4) DronesKamikaze/Kalashnikov.
5) MANPAD.
6) Konnet ATGM.
Hizo ndio zilikuwa sababu zangu za kusema jeshi la Russia aliwezi kuzingirwa kirahisi wakati wana helicopter gunships, Sukhoi 24 tank buster na fighter bombers and jetfighters chungu mzima that is what I meant, lakini nyinyi badala ya kuleta maoni mbadala mna target members fulani kwenye forums hii hasa wenye maoni mbadala ambao si bendera fuata upepo, mna waporomoshea maneno ya shombo, wakati mwingine mnawatukana kabisa, mnafikia mpaka hatua ya ku-question akili za watu kama ziko sawa, just to get even bila sababu zozote za msingi zaidi ya EGO zenu za ajabu - sasa swali ni: kawapa nani mamlaka ya ku-run JM as if nyinyi ni kama ma-share holders-yaani forums nzima imekuwa turned up side down and inside out!! Mvuto wa zamani wa JF umeanza ku-decay exponentially kabisa kutokana na unbecoming behaviours zenu.
Maneno mengi yasiyokua na mantiki ushabiki tuu na tenzi za mahaba
Ni ukweli kuwa Russia inaweza fanya lolote kwenye anga la ukraine kwa sasa ? Jiulize ndege ngapi na helcopter ngap zimedondoshwa had sasa.
Jiulize ni makombora mangap ya Russia yamedunguliwa hadi sasa?
Drone ngap zimedunguliwa had sasa?
Kulingana na data kutoka Global Firepower, VKS - jeshi la anga la Urusi - ni la tatu kwa ukubwa ulimwenguni, likizidiwa tu na zile za Amerika na Uchina.
Mwanzoni mwa mzozo, Moscow ilikuwa na ndege za kivita 1,391 (ikilinganishwa na 132 za Ukraine) na helikopta 948 (Waukraine walikuwa na 55 tu).
Lakini jeshi la ukraine na uchache huo wameweza kulinda anga lao kwa zaid ya asilimia70.
Twende kwenye point kumiliki anga tafsiri yake ni kuweza kurusha ndege na helcopter bila kuwa na upinzani wowote wenye madhara.Leo hii Russia hawez peleka ndege yake ukrainne au helkopter kadhaa zikarud salama , ila wewe kimahaba unadai umemiliki anga,
Ukraine anarusha ndege zake na helkopter ,kimahaba unadai unamiliki anga.
Rada zenu na mifumo yenu ya kisasa ya kuzuia makombora inalipuliwa kirahisi kimahaba unatuambia unamiliki anga.
Mkuu mahaba weka chini acha maneno mengi hii vita siyo rahisi kwa russia kama unavyorahisisha .
Hii vita imemgharimu puttin sana na kumvua nguo .
Nikwambie wazi tuu US kamwe hatokubali kushindwa hii vita ,US wa vietnam siyo huyu aliyejiimarisha duniani kote kijeshi,kiuchumi na kisiasa.