Special thread: Vikaragosi vya Masoud Kipanya

Nimekuelewa mkuu, tafsiri mrua kabisaa au wewe ndo kipanya mwenyewe vipi!!!?
Halafu wakati anahangaika na hao wanacheza kwa kifusi wengine wanakuja nyuma ya tinga na vikapu wanarundika tena michanga alikorekebisha Hahahahaha hatari sana
 
Mange hapo sasa ni yupi?

Ok, nimeshamuona kumbe yupo hapo juu ya bullldoza na midole yake juu.
 
You are jinias hahahahhh
 
Waliopo kwenye bulldozer wanafanana rang na dereva hivyo inaonesha ni watu wa kundi moja sio waliotoka chini wakadandia
 
Dereva anasafisha kifusi huku akiwa na watu ambao wangemsaidia kusafisha kifusi(kipanya amewatofautisha na watu wengine wa chini kwa rangi hapa kila mmoja anaweza kuja na theory yake
Mimi nilichofikiria
Yawezekana mmoja akawa anawakilisha viongozi wa dini na mwengine anawakilisha watendaji ndani ya serekali)
Huku dereva akijua alionao kwenye bulldozer watamsaidia ndio kwanza (viongozi wa dini) wanamgeuka na kuwa wapinzani(angalia ishara ya vidole)
Na huku dereva akimuachia jukumu la kuchunga watu wanyuma huyu mtendaji ndio kwanza ametulia akisubiri maagizo na watu wanajichotea kilaini

Huku mbele dereva amechanganyikiwa na makelele mpaka ameachia usukani bulldozer linaenda lenyewe madhara yake litaenda bila ya direction
 
Kuanzia leo naanza kufatilia comment zako!! Maana umetafsiri vizur
 
Mi nimeona Kifusi na Tingatinga!View attachment 735969
Nimeelewa hivi.
Magufuli ana kazi ya kusawazisha hicho kifusi. Shida ni kwamba juu ya kifusi kuna watu ambao hataki waumie pindi anapoendelea kufanya kazi yake. Ameamua kushuka ili awaambie watoke yeye afanye kazi yake. Badala ya hao watu kuondoka eneo hilo, wao ndo kwanza wanaruka sarakasi.

Tafsiri ya hilo ni kwamba hatumcheleweshi magufuli. Bali tunajichelewesha wenyewe.

Huku nyuma ni baadhi ya watu walianza kunufaika na kazi yake ya kusawazisha
 
Huyo aliyekaa kwenye Hilo bulldozer huku akiwa amenyanyua mikono anashangilia lazima atakuwa ni Bashite tuu!
Kweli uoni ni macho, kila mtu ana yake! Kuna aliyekaa na kunyanyua mikono hapo kweli?
 
Kwa kelele zenu mmesababisha nitoke kwenye usukani, mmepanda kwenye kifusi ninachotaka kukifukua, haitoshi mmepanda hadi kwenye karandika kunikebehi, na wengine mnaiba hadi mafuta. Dawa yenu nikuwashukia huko huko niwatandike RUNGU[emoji3]
 
Kwa kelele zenu mmesababisha nitoke kwenye usukani, mmepanda kwenye kifusi ninachotaka kukifukua, haitoshi mmepanda hadi kwenye karandika kunikebehi, na wengine mnaiba hadi mafuta. Dawa yenu nikuwashukia huko huko niwatandike RUNGU[emoji3]
 
Hii nilivyoelewa mm ni kwamba wananchi wanzidi kusukumwa mbaaali na hilo li tingatinga na huyo operator aliye juu ya hilo tingatinga na anatoa maelekezo na kuwafukuza wazidi wasogee huko
Hapana ni kinyume chake wananchi wanaanza kufaidi matunda huku majizi yakilala mbele
 
The Bulldozer hawamsikilizi tena. Hawamwogopi, anapiga nduru wampishe ndo kwanza wanapiga sarakasi.

Wengine wamepanda kabisa tingatinga, ila wachache wanachota mafuta.

Sijui mwisho wake.
Ndivyo inavyokuwa hata ktk Familia baba ukiwa Mali Sana hufikia hatua watoto hukudharau wewe utapiga kelele wao hawakusikilizi tena wao wafuata yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…