Special thread: Vikaragosi vya Masoud Kipanya

Povu lote hili la nini ndugu? Nani kakuambia mimi ni Lumumba?
Hiyo ni tafsiri yangu, kama hujakubaliana nayo, ni ok tu kwangu, maana mimi kuna uzi nyingi sikubaliani nazo hapa JF, ila siendi kutoa povu wala matusi kwa walioanzisha
Nikisema Kipanya amemkejeli Magufuli simchongei kipanya, kwani hata akimkejeli sio kosa kumkejeli rais, Rais pia anakejeli watu..tatizo ni nini?
Mambo madogo haya, tuache kupanic
 
Umempa ukweli mtupu yani kikatuni hakihusiki na magufuli kabisa. Nakuunga mkono acha Raisi awateue upinzani Wana mawazo chanya kuliko hao wanaoendekeza upuuzi
Huyo kapanic tu, yeye ana matatizo ya kutafsiri pia kisha anatukana na mipovu mingi..Eti nimetokea Lumumba, sijui mpumbavu blah blah blahh...
Nimeanzisha uzi kwa tafsiri yangu na maoni yangu, kama wengine wafanyavyo hapa JF, wewe kama una tafsiri yako kwa nini unitukane? Si utoe hiyo ya kwako pia?

Eti namchongea kipanya,kwani ni kosa kumkejeli rais hadi nimchongee...?
 
Wewe umeandika kwa hisia kumfanyia masoud uchochezi na unajua awamu hii watu wanapotezwa kwa Kuwa na maoni tofauti, mimi sijaona masoud akimu mention magufuli hapo ni wewe tu na interpretation zako.
 
Wewe umeandika kwa hisia kumfanyia masoud uchochezi na unajua awamu hii watu wanapotezwa kwa Kuwa na maoni tofauti, mimi sijaona masoud akimu mention magufuli hapo ni wewe tu na interpretation zako.
Of course ni interpretation yangu, mtu mwingine anaruhusiwa kuwa na interpretation yake pia..Hii ni JF haimaanishi kila kinachowekwa hapa ni fact, nyingi ni opinion za watu.

Kama ni kumpoteza kipanya hawaitaji mimi kuwatafsiria ili wampoteze, sio wajinga , wanaweza kutafsiri pia na kama kumpoteza wakampoteza.
 
Lakini kwanini umlishe kipanya maneno maana mimi nilivoingia kusoma uzi na title ni vtu viwili tofauti kabisa.

Hafu humu JF watendaji wengi hupita na kufanyia kazi sasa mwenzako akitekwa, Ben saanane uzi wake ulimpoteza mazima.

Humu JF hupitiwa na watu wengi hafu uongo ukiachwa hugeuka ukweli
 
Una uhakika gani kama ni kejeli au ww ndo unaleta uchonganishi au Una mgogoro na ki-mouse?
 
Nimemlishaje maneno sasa, amechora katuni mimi nikatafsiri nilivyoelewa, Mchora katuni anajua katuni yake inaweza ikatafsiriwa tofauti na ndio maana hawaziweki katuni zao zikawa na maana ya wazi sana.
Halafu hiyo katuni nimeiona twitter, instagram na facebook na maoni ya watu karibu wote wametafsiri pia hivyo,
 
Hyo sio tafsiri ulikusudia kumchongea mwenzako eti kamdhihaki Raisi. Bora hata angemchora na bichwa Lake lakini mtu kazama kabisa hapo ungesema hata muogeleaji inge sound better. Wrong interpretation kabisa
 
Hakimu wa kazi ya sanaa yoyote ile ni hadhira! So usilazimishe mtazamo wako ndio mtazamo wa watu wote, mwingine anaweza akasema "mfa maji haachi kutapatapa"
 
Mtu hawezi wajibika kwa ulichoelewa anawajibika kwa alichomaanisha hapo wapi imeonesha ni Magufuli? Usituaminishe ulichoelewa ww
 
Hyo sio tafsiri ulikusudia kumchongea mwenzako eti kamdhihaki Raisi. Bora hata angemchora na bichwa Lake lakini mtu kazama kabisa hapo ungesema hata muogeleaji inge sound better. Wrong interpretation kabisa
Dah, sijasema kamdhihaki, nimesema kamkejeli..Na kumkejeli mtu hata kama ni Rais sio kosa, kumkejeli rai sio kumtukana wala sio kosa la jinai..Tatizo liko wapi?

Kejeli ni kumsifia mtu lakini ukimaanisha kumkosoa, mfano nikisema leo umejitahidi kuwahi, lakini umechelewa kuliko siku zote hiyo ndio kejeli,
 
Kila mtu atatafsiri kulingana na hali aliyomo...kama wewe unaona ndo hivyo..sawa tu....Mwingine ataweka ccm hapo, mwingine Chadema etc
 
kipanya katisha sana. kiukweli kuna haja ya watanzania kuungana na kuupinga huu muswada hauna manufaa kwa taifa siku za mbeleni.
siasa inamgusa kila mtu hata kama haujihusishi nayo. Huu muswada unaenda kuwa chanzo cha kupotea kwa amani na umoja uliopo Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…