Kila aliye mwanamke akimtazama mke wa Roma anavyoongea ni lazima atalengwa na machozi "Yuko wapi mume wangu"
Kila aliye mwanaume lazima atajiuliza "yuko wapi kijana mwenzetu, mtoto wetu n.k"
Tumuombee na tuwaombee wenzie pia huko walipo wawe salama
*Tukio hili la kupotea kwa vijana hawa linashabihiana moja kwa moja na tukio la kivamizi alilolifanya mwenye mkoa wake, na linatiwa chumvi na vyombo vya dola kushindwa kumchukulia hatua mvamizi, kiasi kwamba sasa hivi hali ya kuteka watu inaanza kuonekana kua ni ya kawaida maana hata vibaka na majambazi sasa wanao mfano mzuri toka kwa mwenye mkoa "kwamba unaweza ukavamia sehemu na usichukuliwe hatua zozote za kisheria kama walivyomuacha huyu jamaa" watu hawana woga tena maana binaadamu yeyote huiogopa hukumu ya madhambi yake kuliko dhambi yenyewe
Kwa hali hii tutarajie uvamizi na utekaji kuendelea maana hakuna mfano wa hukumu ya wavamizi wa roho na maisha ya watu iliyotolewa mpaka sasa
MRUDI SALAMA KAKA ZANGU, TUNAWAOMBEA M/MUNGU AJAALIE MKUTANE TENA NA VIPENZI VYENU