Special kwa wanawake wa JF: Ni kitu gani hupendi kutoka kwa mwanaume?

sipendi mwanaume anayevaa mlegezo, suruali za kuchanika, anayesokota nywele, mwenye tattoo, anayefuga makucha marefu au kile cha mwisho, anayevaa hereni, anayevaa viatu kama mocker bila soksi na visuruali vifupi
hahahahah. Umemaliza wote kudadeq
 
Kuna wanaume/wavulana wanavaa suruali za kuchanika utadhani zimeliwa na panya.. mapaja yote yapo wazi.

Mwingine kaptura fupi, mapaja yote yapo wazi mtoto wa kiume..
Wengine suruali imembana basi hata kutembea vizuri anashindwa mtoto wa kiume anaonyesha umbo lake!

Wengine suruali iko chini ya matako na ile nguo ya ndani almaarufu kama boxer sijui bukta yote inaelea huku nje tena ikiwa chaaafu.

Wengine nywele kichwani vuruvuru kitimtim kimetimuka kweli kweli, mnaita kwenda na fasheni...mwanaume amesuka nywele ama nywele zimesimama kama mahindi kichwani..
Wenyewe mnaita swaga.

Wanaume wachafuwachafuu wasiojipenda.

Mungu awabariki wanaume wote mnaovaa vizuri,

Huwa mnatuvutia hata kabla hamjaongea na sisi.

NB:Sitazungumzia mambo ya uumbaji mf kimo(urefu ,ufupi),rangi(weupe,weusi)
Siwezi kuukosoa uumbaji wa Mungu
Nimejikita zaidi kwenye namna mtu anavyojiweka bila kujali aliumbwaje.
Mabaharia msije mkadanganyika na kauli za huyu dada wengi ndo tunaowaona wanatongozwa na ao ao wanaovaa jinsi za kuchanika ,,,weng wao wamekua single mother kw kupenda wanaume wanaovaa kithug life sasa ww jifanye nice guy nenda na suruali zako za vitambaa alafu kitakachokupata usje kulialia humu ,,kiukwel wanawke wanapenda wanaume wahuni kuliko wale wastarab
 
Nakazia....wawe wananukia pafyum za risasi
 
Back
Top Bottom