Newzfid
Member
- Feb 23, 2018
- 5
- 34
Baada ya kuirusha roketi ya Falcon 9 toka California jana, SpaceX walitumia neti kubwa kujaribu kuidaka pua au 'nose cone' ya roketi pale itakapo dondokea bahari ya Pacific. Kwa mara ya kwanza jaribio liligonga mwamba, kipande kimoja cha pua kilikoswa na neti ambayo ilifungwa kwenye meli na kudondokea pembeni hivyo kikapotelea baharini.
Sehemu hiyo ya roketi pia inaitwa 'payload fairing', ile pua yenye umbo la cone inakaa mbele ya roketi, kulinda mzigo wa ndani ya roketi wakati wa kurushwa kwenda hewani. (Tazama kuanzia dakika 2: 24 kwenye video ifuatayo uone pua ya roketi ikikatika na kuwa vipande viwili)
Mara baada ya roketi kufika angani, pua hiyo inavunjika kuwa vipande viwili na kurudi tena duniani. Kikawaida, makampuni hayapotezi akili na mda wa kutaka kukomboa au 'recover' vipande hivyo, Lakini kwa CEO wa SpaceX, Elon Musk anaonyesha shauku ya kutaka kuvirejesha duniani vikiwa vizima. "Fikiria unakuwa na $6 million kwenye kibegi kikielea hewani lakini kinakuja kupotelea baharini" Musk alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari mwezi machi,2017. "Hivi utajaribu kuokoa? Ndio. Ndio lazima utafanya hivo"
SpaceX wamekuwa maarufu kwa kuzifanya roketi zao zitue tena duniani baada ya kurushwa ili zirushwe kwa mara nyingine tena.
Lakini njia ambayo wanataka watumie kuokoa pua za roketi ni kitu cha tofauti na kile wanachofanya kwenye mhimili wa roketi. Booster za Falcon 9 huwa zinawasha injini zake zinapokuwa zikirudi duniani, ili kupunguza spidi yake na kuipa mwongozo mzuri wakati wa kutua. Pua za roketi za kawaida hazina injini wala chochote kile. Lakini SpaceX wameweka mfumo na injini ndogo zinazoiongoza pua ya roketi wakati ikishuka toka angani kitaalamu zinaitwa 'Thrusters'
Pale vipande vikiwa viko karibu na uso wa dunia, mwavuli au parachute ndogo zinafunguka kupunguza kasi ya kuanguka. Kwenye uso wa dunia, ambao ni bahari kunakuwepo meli ya SpaceX inayoitwa Mr. Steven ambayo inajaribu kudaka vipande kwa kutumia neti kubwa kama makucha.
Kwa bahati mbaya, meli hiyo ikashindwa kudaka ingawa pua hiyo haikuharibika kwa kuwa haikudondoka kwa kasi sana. Bila kujali jaribio hilo, Elon Musk kasema kuwa ndani ya miezi sita atahakikisha wanaweza kukomboa pua za roketi zao