Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,734
- 6,292
Maeneo yanayozalisha injini na ‘ammunitions’ yalilengwa, Wizara ya Ulinzi inasema
Jeshi la wanaanga la Urusi limeshambulia viwanda vya roketi mashariki mwa Ukraine na kuharibu makao makuu ya mamluki, Wizara ya Ulinzi imesema.
Wizara ilisema katika muhtasari wake wa kila siku mnamo Ijumaa kwamba kiwanda cha injini za makombora huko Pavlograd kiligongwa, pamoja na ‘floor’ tatu za duka za kiwanda cha Kommunar huko Kharkov ambazo zilitengeneza vifaa vya kurushia roketi nyingi.
Ndege za Urusi na vikosi vya ardhini pia vilishambulia ‘command centres’ tano na kufanya shambulio la kombora kwenye makao makuu ya "moja ya vitengo vya mamluki wa kigeni" karibu na mji wa kusini wa Nikolaev, wizara hiyo ilisema.
Imeongeza kuwa kombora tisa zilizorushwa kutoka kwa mifumo ya M142 HIMARS zilizotengenezwa Marekani na tatu zilizorushwa kutoka kwa mfumo wa BM-27 Uragan ziliharibiwa angani katika Mkoa wa Kherson nchini Urusi.
Moscow iliongeza mashambulizi mjini Kyiv na kwingineko nchini Ukraine mwezi uliopita, na kuharibu mitambo ya nishati ya joto na njia za umeme, kati ya malengo mengine.
Rais Vladimir Putin alisema kushadidi kwa mashambulizi hayo ni kulipiza kisasi kwa "mashambulizi ya kigaidi" ya Kyiv katika ardhi ya Urusi, ikiwa ni pamoja na shambulio la lori lililoharibu daraja la kimkakati linalounganisha Rasi ya Crimea na Bara la Urusi.