Mwaka 2035 satellite zitaanguka na kuua watu

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
SpaceX.jpg

Nchini marekani imetoka repoti kupitia shirika la utawala wa shirikisho la Anga (federal Aviation Administration), wanasema kuanzia miaka ijayo kutakua na hatari ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa kwa kuangukiwa na satellite.

Kama kampuni ya SpaceX itaendelea kurusha satellite angani basi takribani ya vipande 28,000 ya vyuma vikubwa vya uchafu wa satellite vitarudi duniani ifikapo mwaka 2035.

Inasemekana Kwamba sio vyuma vyote vitaungua na kupotea angani itapelekea baadhi yake kurudi duniani na kuleta maafa kwa watu kwa kujeruhi au kuua kabisa.


Kampuni ya SpaceX ndo inaoongoza kurusha satellite kila mwaka imepewq onyo ya kupunguza urushaji wa satellite angani kwani mpaka kufikia hivi Sasa Elon musk na kampuni yake ya SpaceX imerusha takribani ya satellite 5000 angani.
 
Huko juu si tunaambiwa kua hakua gravitation force?

Wataalamu mje mtupe elimu hapa,hizo Satellite zitafikaje huku ardhini?
 
Back
Top Bottom